Dar es Salaam
Sakata la vigogo wa dawa za kulevya
limezidi kuwaibua watuhumiwa baada ya kigogo mwingine aliyekuwa akisakwa tangu
mwaka 2012, kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias
Nyerere(JNIA), Dar es Salaam.
Hatua hiyo imetokana na kunaswa kwa
watuhumiwa, ambao ni vinara wa kusafirisha na kuingiza dawa za kulevya nchini.
Kigogo huyo aliyekamatwa juzi saa
3.00 asubuhi ni Christine Kighahe, aliyewasili nchini kupitia katika uwanja huo
akitokea Thailand kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya.
Christine, anadaiwa kuwa ni kigogo wa
biashara hiyo, akiwatumia wanawake katika uuzaji na usambazaji wa dawa hizo
nchini na katika miji ya Hong Kong na Guangzong.
Akizungumza Kamanda wa Kikosi cha
Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema mwanamke huyo alikuwa akitafutwa
kwa muda mrefu bila ya mafanikio.
Alisema Christine alikamatwa baada ya
kuwekwa ulinzi mkali katika maeneo mbalimbali nchini na kikosi kazi cha
kupambana na dawa za kuleya.
Kamanda Nzowa alisema baada ya
upelelezi kukamilika, mwanamke huyo atafikishwa mahakamani na kuunganishwa na
vigogo wengine wa biashara hiyo haramu.
No comments:
Post a Comment