Nairobi, Kenya
Kenya imeanza kutangaza mpango wa matumizi wa
vitambulisho vya uraia na viza ya pamoja ya kusafiria katika nchi tatu za
jumuiya ya Afrika mashariki (EAC).
Hatua hiyo inatokana na Shirikisho la Utalii
Kenya (KTF) na Kampuni ya Trade Mark East Africa (TMEA), kuhamasisha matumizi
ya viza hiyo katika utalii.
Ofisa mtendaji wa (KTF) Agatha Juma alisema
uamuzi wa kuitangaza viza hiyo unatokana na watu wengi kushindwa kuitumia licha
ya kutambulika kisheria .
Alisema idadi ya watu waliojitokeza katika
nchi tatu za Kenya Rwanda na Uganda kutumia viza hiyo ni ndogo. Agatha alisema
kuanzishwa kwa viza hiyo kulilenga kuwarahisishia wanaAfrika mashariki kutoka
nchi moja kwenda nyingine kwa urahisi.
No comments:
Post a Comment