Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Kampuni ya simu
inayoongoza barani Afrika, Asia na Mashariki ya Kati, EtisalatGroup, imeongeza hisa
zake katika kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kufikia asilimia 85.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Zantel jana jijini Dar es Salaam, hatua hiyo ni ongezeko la hisa
hizo kwa asilimia 20 zaidi.
Katika miaka ya hivi
karibuni, Zantel imekuwa ikifanya mapinduzi makubwa katika sekta ya simu za
mkononi Tanzania kwa ubunifu ambao umekuwa ukisaidia kustawisha maisha ya watu.
Baadhi ya huduma hizo
ni pamoja na Z-Kilimo ambayo huwezesha wakulima hata wa vijijini kuweza kupata
taarifa muhimu za jinsi ya kuongeza uzalishaji na hivyo kuendeleza sekta ya
kilimo.
Huduma nyingine ni
Islamic Portal, Discover Tanzania (Tourist Portal) na Reverse Ring Back tone
(RRBT) ambazo zinawasaidia watanzania kwa namna mbalimbali.
Pia Zantel ni moja ya
kampuni za simu za mkononi nchini zilizofikia makubaliano na kampuni nyingine
za simu kuwezesha wateja wao kutuma na kupokea pesa miongoni mwao.
Hii ni huduma ya kwanza
ya aina hiyo Afrika ambapo mteja wa kampuni hiyo wa huduma ya EzyPesa anaweza
kutuma na kupokea pesa kwenda mitandao mingine.
Kwa sababu ya juhudi
zake katika kuokoa maisha ya mama na motto, Zantel imeshawahi kupata tuzo
inayoheshimika ya GSMA kwa mradi wa “Mobile Baby”, wakati mkakati wa “Fight
Against Malaria” ulitambulika na Wizara ya Afya.
No comments:
Post a Comment