Friday, October 17, 2014

Kampeni ya chanjo dhidi ya Surua na Rubella kuziduliwa leo

Na Mwandishi wetu,Dodoma

Kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa Surua na Rubella kwa watoto wenye umri wa miezi tisa hadi miaka 15 inatarajia kuzinduliwa leo ambapo watoto milioni 21 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hizo na itadumu kwa muda wa siku saba.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Ofisa Mkuu wa Matching Fund partner Gavi, Dkt. Seth Berkley alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kutoa chanjo itakayozuia milipuko ya magonjwa hayo.

“Chanjo hii itatolewa kwa watoto wote wenye umri wa kuanzia miezi tisa hadi miaka 15 ili kuzuia milipuko yaa magonjwa hayo,”alisema

Alisema chanjo hizo zikifanikiwa kutolewa, Tanzania itakuwa imepiga hatua kubwa ya kutoa chanjo mbili kwa wakati mmoja

“Chanjo hii inakusudia kuwafikia zaidi wavulana na wasichana milioni 600 kwa kuwapatiwa chanjo ya surua na rubella,”alisema.

Alisema taasisi yao inaunga mkono jitihada hizi na inasaidia kampeni na itaendelea hadi mwaka 2020 kwa ajili ya kupunguza vifo vitokanavyo na surua na rubella.

 Alisema kuwa Surua ni gonjwa hatari, zaidi ya muongo mmoja jitihada zimekuwa zikichukuliwa kupunguza idadi ya vifo, lakini kumekuwepo na vifo zaidi ya 120,000 mwaka 2012 sawa na vifo 14 kila baada ya saa moja.

Aliongeza kusema rubella nayo imekuwa ikiambukiza kutoka mtoto mmoja kwenda mwingine na kusabisha vifo, pia madhara wakati wa kujifunmgua na ulemavu kwa mtoto.

Taasisi ya Gavi Matching Fund imeshirikiana na Lions Clubs International kufanya kazi pamoja na serikali na wadau wengine wakiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Watoto (UNICEF) kutoa elimu ya kampeni hiyo na kusaidia wataalamu wa maswala ya afya.

“Hiyo ikiwa ni pamoja na kufanyanao kazi ya kutoa chanjo hizo na kubadilishana taarifa kati ya yao na wazazi na wauguzi,”alisema.

Naye Mwnyekiti wa Lions Club International Fundation,Bw Barry Palmer alisema taasisi yao imejidhatiti kupambana na surua na rubella Tanzania na Duniani kote.

“Tutahakikisha kampeni hii inapata mafanikio yake kwa kushirikiana na Gavi kwa ajili ya kuzuia milipuko ya magonjwa haya,”alisema.

Katika Kampeni hii Taasisi ya India (Serum Institute of India) (SII) imechangia milioni  5.5 kwa ajili ya chanjo hizo ambapo mwaka 2013 walikubali kusaidia milioni 22 kwa  kwa kipindi cha miaka mine.

Pia taasisi ya Gavi’ imekuwa ikisaidia jitihada za kupamabana na magonjwa haya na imekuwa ikishiriki jitihada zinazofanyika za kupunguza vifo duniani.

Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2013 hadi 2013, Tanzania imekuwa na zaidi ya watu 200 waliopatikana na rubella. Rubella na Surua zinatabia zinazofanana.


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando alisema takwimu hizo zimeifanya serikali kutoa chanjo hiyo kwa watoto wa umri wa miezi tisa hadi miaka 15.

No comments: