Wednesday, October 29, 2014

BBC yaishangaa Rwanda

Kigali, Rwanda
Shirika la Habari la Uingereza (BBC), limeishangaa serikali ya Rwanda kufungia matangazo yake katika eneo la maziwa makuu kutokana na kurusha makala yanayo husu mauaji ya kimbari.

Taarifa iliyotolewa na BBC, ilisema uamuzi wa kufungia matangazo yake haukuzingatia haki ya kupata habari kwa watu wa eneo hilo.

Makala yaliyo rushwa na BBC, kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda, yalizingatia miiko na maadili ya uandishi wa habari ikiwa na pamoja na kushirikisha pande zote.

Taarifa ya BBC, imekuja siku chache baada ya serikali ya hapa kuyafungia matangazo ya BBC, kwa kile ilicho eleza kurusha makala inayohusu mauaji hayo huku ikiwa na makosa na udhalilishaji.


Serikali ilisema matangazo hayo yalikuwa yakihamasisha chuki katika jamii.

No comments: