Dar es Salaam
Tatizo la kukatika kwa umeme limekuwa
kero kwa maeneo mbalimbali ya nchi na lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa
shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Maeneo mengi yamekumbwa na kero hiyo
tangu wiki iliyopita mpaka jana huku wahusika wakishindwa kutoa taarifa ya nini
kinachosababisha kero hiyo ya kukatika kwa umeme.
Hali hiyo imesababisha adha hata
katika vikao vya kamati za Bunge vinavyoendelea kwenye Ukumbi wa Karimjee,
iliyosababisha Wajumbe wa kamati kushindwa kuendelea na shughuli zao .
Wajumbe wa kamati hizo walionekana
kuangaika na wengine kufungua madirisha na milango ili kupata hewa,baadhi
wakitoka nje mara kwa mara na wengine wakitumia makabrasha yao kujipepea
kutokana na joto kali.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha
ya Bunge (PAC), Deo Filikunjombe aliyekuwa akiongoza kikao, ilibidi amwombe
radhi Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Philemon
Luhanjo kutokana na kuchelewa kuanza kwa kikao kulikosababishwa na kukatika kwa
umeme.
“Pole sana mzee nimekuona umewahi
kweli lakini shughuli zetu hapa zimekwamishwa na umeme, kwa utaratibu ulivyo ni
lazima majadiliano yaanendelea kwenye vikao vyetu yakirekodiwa kwa ajili ya
kumbukumbu.
No comments:
Post a Comment