Meneja Mwandamizi wa Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya Afrika
Tanzania, Bw. Solomon Haule (aliyesimama) akielezea jambo wakati wa droo ya
Kwanza ya mwezi ya kampeni ya ‘Weka na Ushinde’ inayoendeshwa na benki hiyo
jana jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Hazina wa benki
hiyo, Bw. Bruno Ngooh; ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bw. Majid
Bakari na Meneja Mwandamizi wa tawi la benki hiyo la Msimbazi, Kariakoo, Bw.
Emmanuel Mwaya (wa pili kulia).
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Wateja watano wa Benki ya Afrika Tanzania wameibuka na
ushindi wa zawadi mbalimbali baada ya kushiriki shindano la droo ya Kwanza ya mwezi
ya Weka na Ushinde zaidi inayoendeshwa na benki hiyo.
Kampeni ya benki hiyo ya
‘Weka na Ushinde’ ilianza mwezi wa Tisa na inatarajiwa kuisha mwezi wa Kumi na
Moja mwaka huu.
Droo hiyo ilichezeshwa na Mkuu wa Hazina wa Benki
hiyo, Bw. Bruno Ngooh katika tawi la Msimbazi Kariakoo ambapo washindi hao
walishinda baada ya kuongeza fedha au amana katika akaunti zao na kupata sifa
za kuingia katika droo hiyo.
“Droo hii ni ya kwanza ya Mwezi ambapo mteja anatakiwa
kuweka fedha katika akaunti yake zaidi ya Tsh. milioni 2 ili aweze kuwa na sifa
ya kushiriki,”alisema.
Alisema katika droo hiyo wateja 551 waliingia katika
shindano hilo na watano wakaibuka washindi na kujinyakulia zawadi mbalimbali.
Mshindi wa kwaza katika droo hiyo ni, Leakey Gathari
aliyepata zawadi ya pikipiki; John Raphael, Simu ya Mkononi aina ya Samsung
Tablet; Ibrahim Agwanda simu aina ya Smart Phone; Mary Mushi, Tshs 500,000 na
Innocent Msigwa, Vocha ya Tsh. 100,000 ya kununulia vitu kwenye duka kubwa
(super market).
No comments:
Post a Comment