Waziri
wa afya na ustawi wa jamii Dkt. Seif Seleman Rashid kulia akifurahi jambo na
msimamizi mkuu wa mradi wa Measles Rubella Tanzania kutoka Klabu
ya Lions International , Bw.Abdul Majeed Khan wakati mara baada ya
kuzindua kampeni ya chanjo zidi ya Suluwa na Rubella inayotolewa kwa watoto
kuanzia umri wa miezi tisa mpaka miaka 15 kwa nchi nzima, klabu hiyo imetoa
jumla shilingi bilioni ishirini ili kufanikisha kampeni hii ya
kutokomeza suluwa na rubella nchini. kulia ni mmoja kati wasimamizi
wa mradi huu.
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Klabu ya Lions
Internation imechangia takribani Shilingi billion 20 ($12 milioni) katika
kampeni shirikishi ya chanjo ya surua-rubela ambayo inalenga kufikia watoto
zaidi ya million 20 nchini kote.
Katika kampeni hiyo ya
siku saba kuianzia tarehe 18 mwezi huu, watoto wenye umri kati ya miezi tisa na
miaka kumi na mitano watapata chanjo hiyo ikiambatana na matone ya vitamin A,
na dawa za minyoo tumbo huku watu wazima wakipata kinga tiba dhidi ya matende,
mabusha, ngiri maji pamoja na minyoo.
Akizungumza na
waandishi wa habari siku ya jumamosi, mratibu wa surua-rubela wa klabu ya Lions
nchini Mr Abdul Majeed Khan alisema ushiriki wa klabu yake ni ishara kuwa
taasisi za huduma nchini zina wajibu wa kuchangia katika kuboresha afya za
watanzania.
“Ni matumaini yetu
kuwa kwa mchango wetu huu, na michango ya wadau wengine wa masuala ya afya kwa
ajili ya kampeni hii, itawezesha kufikia angalau watoto million 21 na kuwakinga
na magonjwa haya hatarishi, “ alisema Bwana Khan ambaye pia ni Gavana wa zamani
wa Wilaya ya 411B ya Klabu ya Lions.
Wilaya hiyo
hushirikisha nchi za Tanzania na Uganda.
Naye gavana mstaafu
mwanzake wa Wilaya hiyo hiyo Bwana Wilson Ndesanjo alisema kuwa kupitia
wanachama wake waliotapakaa duniani kote Lions iliweza kukusanya $7.5 milioni
(sawa na Shilling 12.37 billion) huku kiasi kungine kikichangiwa na umoja wa
Global Alliance for Vaccines and Immunizations (GAVI).
Pamoja na shughuli
zingine klabu ya Lions Tanzania imekuwa ikichangia katika kuboresha sekta ya
maji nchini kwa kuchimba visima mashuleni na vijijini.
No comments:
Post a Comment