Na Mwandishi
Wetu,Dar es Salaam
Tanzania imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika
kutembelewa na ujumbe maalumu wa wafanyabiashara kutoka nchini marekani wenye
nia ya kuwekeza nchini, ikiwa ni matokeo ya mkutano wa kimataifa baina ya taifa
hilo kubwa duniani na Afrika uliofanyika Agosti mwaka huu.
Ujumbe huo wenye wafanyabiashara 18
umejumuisha wamiliki wa makampuni na taasisi za kibiashara wanaokusudia
kuwekeza katika nyanja mbalimbali . Katika mkutano baina ya wawekezaji hao na
wadau wa uwekezaji uliofanyika jijini Dar es Salaam; ujumbe huo ulipokea ripoti
kuhusu hali ya uwekezaji nchini.
Afisa uwekezaji mkuu kutoka Kituo cha
uwekezaji nchini Brendan Maro alieleza hali hiyo akilenga juu ya sera ,fursa na
changamoto zinazokabili sekta ya uwekezaji.
Katika taarifa hiyo alisema kuwa Marekani ina
miradi 231 na imefanikiwa kutengeneza nafasi 50,927. Maro alitoa sababu kumi
kwa nini Tanzania ni miongoni mwa maeneo muhimu ya uwekezaji tofauti na nchi
nyingine. Akifafanua hilo alisema ni pamoja na utawala bora na fursa nyingi za
uwekezaji ukilinganisha na nchi nyingine barani Afrika.
No comments:
Post a Comment