Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Suala la uhaba wa dawa na vifaa tiba
katika hospitalini nchini ikiwamo Taasisi ya Saratani ya Ocen Road, limeonekana
kuielemea Wizara ya Afya baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk Seif
Rashidi kuthibitisha, huku akidai kuwa Serikali itapeleka fedha kwa awamu
Bohari ya Kuu ya Dawa ili kupunguza uhaba huo.
Waziri Rashidi alikiri kuwa MSD
inadai Serikali kiasi cha Sh90 billioni, jambo ambalo linafanyika bohari hiyo
kushindwa kununua dawa kutoka kwa wauzaji ndani na nje ya nchi.
“Ni kweli bohari kuu ya dawa
imepungukiwa fedha za kununulia dawa lakini siyo kwa kiasi cha kushindwa kutoa
huduma kabisa kama inavyoelezwa. Kiasi cha pesa kinachotajwa si kigeni na
serikali imekuwa ikitoa kiasi cha fedha kidogo kidogo ili kuongeza uwezo wa
bohari ya dawa kununua na kusambaza dawa,” alisema Waziri
Hivi karibuni kulikuwa na uhaba wa
dawa Taasisi ya ORCI na kufuatiwa na taarifa kutoka shirika lisilo la
kiserekali la Sikika ambayo ilieleza kuwa Serekali haijalipa kiasi cha Sh90
bilioni kwa MSD.
Waziri Rashidi alikiri kuwapo kwa
ukosefu wa matibabu OCRI kutokana na uhaba wa dawa na ubovu wa baadhi ya
mashine za mionzi.
Kadhalika Waziri alionyesha kuwa
suala la ORCI ni zito kwa serikali baada ya kusema kuwa matibabu katika taasisi
hiyo hutolewa bila malipo.
No comments:
Post a Comment