Mkurugenzi wa Utawala, Rasilimali watu na Mawasiliano wa
Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (DART) Bw. Evodius Katare akizungumza
akisisitiza jambo wakati alipokutana na Maafisa Habari, Mawasiliano ambao
Taasisi zao ni wadau wakuu wa mradi huo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,
wakati wa kujadili na kupanga mikakati ya namna ya kukabiliana na vitendo
vinavyoshimiri vya uharibifu wa miundombinu ambayo imeshakamilika.
Na
Mwandishi Wetu, Da es Salaam
KUSHAMIRI
kwa vitendo vya uharibifu na wizi unaondelea kwenye miundombinu ambayo
imeshajengwa kwa mabasi yaendayo haraka (BRT), Maofisa wa Habari na Mawasiliano
ambao Taaasisi zao zinahusika moja kwa moja na mradi wamekutano jijini mwishoni
mwa wiki ilikupanga mikakati ikiwemo kutoa elimu zaidi kwa jamii juu ya umuhimu
wa kuilinda miundombinu.
Kwa
pamoja, maofisa hao wamekubali kushirikiana kwa pamoja na Wakala wa Mradi wa
Mabasi yaendayo Haraka (DART), kutoa elimu ya kutosha kuhusu mradi, umuhimu
wake na jinsi utakavyoweza kusaidia kupunguza msongamano na nilazima ilindwe.
Akizungumza
mara baada ya kikao na maafisa habari na mawasialiano pomoja baadhi ya wadau
wakuu wa mradi huo, Mkurugenzi wa Utawala, Raslimali Watu na Mawasiliano wa
DART Bw. Evodius Katare alisema mkakati mkubwa uliopo sasa ni kutoa elimu ya
kutosha kwa wananchi ili kuelewa faida na umuhimu wa mradi.
“Kila
mtu anayepita ama kutumia chombo cha moto au kwa miguu katika mradi atakuwa ni
shahidi kutokana na uharibufu mkubwa unaofanywa na watu wasio waminifu wala
uchungu wa pesa zilizotumika kuijenga miundombinu hii ya kisasa,” alisema Katare.
Bw.
Katare aliwaomba wataalumu hao habari na mawasiliano kufanya kazi kwa pamoja
katika kutoa elimu kwa jamii inayozungukwa na mradi na wananchi wote kwa ujumla
juu ya umuhimu wa kulinda miundombinu.
“Miundo
mbinu hii ni ya jamii, hivyo wananchi wenyewe wanapaswa kuelimishwa kuwa mradi
huu ni wa kwao na si wa mtu mwingine,” aliongeza Mkurugenzi huyo.
Alisisitiza
kuwa kila mtu anatakiwa kuwa mlinzi wa mwenzake hakuna haja ya kusubiri vyombo
vya dola ama serikali ianze kukemea uharibifu unaofanywa na baadhi ya watu
wasiopenda maendeleo.
“Naomba
tusisubiri vyombo vya dola ama viongozi wa serikali kukemea hili, tuwe
wazalendo na nchi yetu, kila mtu aguswe na aone kama mradi huu ni wake na kwa
kufanya hivyo tutasonga mbele,” alisisitiza.
Kwa
upande wake Afisa Habari wa jiji Bw.Gaston Makwembe alisema wao kama jiji
wanaomba wananchi waone kuwa mradi huu ni mkombozi kwao hasa kutokana na
changamoto za usafiri zilizopo kwa sasa katika jiji.
“Lengo
la serikali ni kuboresha huduma ya usafiri katika jiji hili na hivyo basi ni
jambo la busara kuitunza na kuingalia miundo mbinu hii mizuri iliyopo
isiharibiwe,”alisema Makwembe.
Aliongeza
kuwa wananchi watambue kuwa kuharibu miundo mbinu ni kosa na ni kurudisha nyuma
jitihda za serikali na kuwakatisha tamaa watanzania wanaopenda kuona sekta ya
usafiri inaboreka.
Nae
Bi. Aisha Malima ambae ni afisa habari kutoa wakala wa barabara nchini
(TANROADS) alisema wananchi wanawajibu wa kujua kuwa miundombinu hii imejengwa
kwa kodi zao wenyewe, wanatakiwa kuwa na uchungu na kile kinachotendeka kwa
sasa.
“
Sisi kama Tanroads tunaona kuwa hii ni hujuma, lakini pia mwananchi
anatakiwa kuwa na uchungu kodi yake ndio imetumika na si vinginevyo,”alisema
Aisha.
Aliongeza
kuwa kutokana na uharibifu unaondelea kufanyika wakala huyo kwa sasa ataanza
kutumia sheria zilizopo ili kuwawajibisha wale wanaokiuka utaratibu wa matumizi
sahihi ya barabara.
No comments:
Post a Comment