Na mwandishi wetu, Dar es salaam
Watanzania wamejihizwa kutumia fursa za kufanya biashara
katika kampunia za migodi kama njia moja wapo ya kuwaingizia kipato na kukuza
uchumi wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa udhibiti na Ukaguzi wa
Uzalishaji na biashara ya Madini
Tanzania (TMAA),Mhandisi Liberatus Chizuzu baada ya kuwapo malalamiko kutoka
kwa wananchi wakidai kutonufaika na mapato yanayotokana na migodi hiyo.
Alisenma kuwa wafanyabiashara wa vyakula,matunda na bidhaa
mbalimbali nchini wanaweza kujiimarisha na kupanuka kibiashara kwa kujiunga
mikataba na wawekezaji.
Mbali na hatua hiyo alisema ufanikishaji wa fursa hizo
unahusishwa na wadau mbalimbali kama wizara ya kilimo na viwanda.
Alisema endapo watanzania watatumia fursa hizo, basi fedha
nyingi zitabaki nchini kwa vile wawekezaji hawatakuwa tena na sababu ua kuagiza
vitu kutoka nje ya nchi.
“Vyakula kama mboga, nyama na matunda vinunuliwe nchini ili
pesa ambayo ingetumika kununua vilevya kutoka nje ibaki nyumbani,” Alisema
Alisema katika kipindi cha mgawanyo wa mapato kati ya
mwekezaji na serikali kampuni hizo zimekuwa zikinufaika zaidi kupitia mrejesho
wa gharama za uwekezaji kutokana na ununuzi wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi.
“Milango iko wazi kushiriki fursa za biashara kwenye migodi,
lakini kama kuna miundombinu ya kutosheleza mahitaji ya soko na mwekezaji,”
Aliongezea
Kwa upande wake Profesa Humphrey Moshi kutoka chuo kikuu cha
Dar es salaam(UDSM) alibainisha sababu zinazochangia ukusanyaji wa mapato
kidogo katika migodi hiyo.
Alisema misamaha ya kodi isiyo na ulazima kwa kampuni za
uwekezaji kupitia uingizaji wa bidhaa za uwekezaji,usafirishaji wa madini ghafi
na umiliki wa asilimia 100 kwa wawekezaji wan je ni miongoni mwa sababu zinazowanyima
wananchi mapato ya migodi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment