Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Afrika Tanzania (BOA Tanzania), Bw. Ammish Owusu-Amoah (kushoto)
akijadiliana jambo na wateja wa benki hiyo muda mfupi mara baada ya mafunzo ya
kuwajengea uwezo wa kibiashara wateja na wafanyabiashara Mkoani Arusha mwishoni
mwa wiki.
Wafanyabiashara mbalimbali
na wateja wa Benki ya Afrika Tanzania (BOA Tanzania) wakimsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Ammish Owusu-Amoah, Mkoani Arusha mwishoni
mwa wiki,wakati mafuzo yaliyoandaliwa na benki kwa ajili ya kuwajengea uwezo
wateja wake na wafanyabiashara.
Na Mwandishi Wetu,
Arusha
BENKI ya Afrika Tanzania (BOA Tanzania), imewataka wafanyabiashara nchini kutumia fursa ya mikopo ya muda mrefu ambayo inayotolewa na benki hiyo kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Wabia wa mMendeleo kama Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kuendeleza na kuanzisha biashara na miradi mikubwa ya maendeleo.
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Benki hiyo ,Bw. Ammishadai Owusu- Amoah alitoa wito huo Mkoani Arusha wakati akizungumza katika mkutano wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara na wateja wa benki mwishoni mwa wiki kuwa ni vizuri wafanyabiashara wangezitumia fursa hizo kuimarisha biashara zao.
Bw.Owusu-Amoah aliwaambia wafanyabiashara na wateja wa benki hiyo kuwa katika mpango huo wa mikopo ya muda mrefu, zaidi ya kiasi cha shilingi Bilioni kumi na tano za kitazania zimeshatengwa.
"Kwa wastani benki yetu inaweza kutoa mkopo hadi shilingi bilioni tatu na nusu (Tsh. 3.5 bilioni) kwa mteja wetu ambaye ataomba mkopo chini ya mpango wa kuwezesha wafanyabiashara kupitia mikopo ya EIB,” alisema na kuwahamasisha kutumia fursa hiyo ya mikopo.
Mkurugenzi mtendaji huyo aliongeza kuwa benki yake inatarajia mikopo hiyo ilenge sekta za Kilimo, Biashara, Elimu, Nishati mbadala na sekta nyingine mbalimbali ambazo zimeainishwa katika mpango huo wa mikopo.
“Sambamba na mikopo hii ambayo inalipwa katika kipindi cha miaka minane, pia benki yangu itaendelea kutoa fursa ya mikopo nafuu kwa wafanyabiashara na wawekezaji hapa nchini,” Bw. Owusu-Amoah alisema..
Kwa mujibu wa bosi huyo, benki imeongeza kiwango cha hadi shilingi billion moja (Tsh.1bn/-) kwa hati fungani za kuombea tenda kwa wateja na wafanyabiashara nchin bila dhamana.
"Njooni mpate hati fungani za kuombea zabuni yaani ‘Bid security’ bila dhamana ili mfanye vizuri biashara zetu kwa ufanisi zaidi na kupata faida itakayoimarisha mitaji yenu "alisema.
Hata hivyo ,Mkurugenzi huyo alisema uzoefu unaonyesha kuwa bado wafanyabiashara wengi hapa nchini hawana desturi ya kuweka akibazaidi ili ziweze kuwasaidia wakati wa vipindi vigumu
"Nachukua nafasi hii pia kuwaasa wale wanaochukuwa mikopo na kupata matatizo ya kurejesha mikopo.. hawapaswi kukimbia na kuvuruga biashara zao bali wanapaswa kurejea katika benki na kupewa utaratibu rafiki wa marejesho"alisisitiza.
Warsha hiyo
iliyoandaliwa na benki ili lenga kuwajengea uwezo wateja wake
ilikuwa nao karibu zaidi na kuelewa mahitaji yao pia kutoa fursa kwa
benki kutathmini huduma zake kwa wateja.
Mpango
huu ambao umeanzishwa na kutekelezwa na benki hiyo kwenye maeneo yote nchini
ambako benki ina matawi yake na mpaka sasa ina matawi ishirini ( 20 ) na
imeendelea kujipanua zaidi mpaka kufikia mizania ya shilingi bilioni
425.
BOA- Tanzania ni moja ya benki ilioko katika kundi la mabenki yajulikanayo kama Bank of Africa Group iliosambaa katika nchi 16 Africa, Ufaransa na sehemu mbalimbali Barani Ulaya.
Mwisho
BOA- Tanzania ni moja ya benki ilioko katika kundi la mabenki yajulikanayo kama Bank of Africa Group iliosambaa katika nchi 16 Africa, Ufaransa na sehemu mbalimbali Barani Ulaya.
Mwisho
No comments:
Post a Comment