Kutoka
kushoto Afisa Biashara wa Mkoa wa Mbeya ,Bw. Stanley Kibakaya,Kaimu Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bi. Quip Mbeyela,Msajili msaidizi mwandamizi wa BRELA,
Bi Rehema Kitambi na Msajili msaidizi mwandamizi wa alama za biashara BRELA,
Bi. Loy Mhando wakifuatilia mada mbalimbali kwenye mafunzo ya
biashara maalum ya mafunzo ya Biashara kwa wajasiriali wadogo na
wakati ambayo imeandaliwa na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA)
mkoani humo jana.
Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Bi. Quip Mbeyela akizungumza wakati wa uzinduzi
wa programu maalum ya mafunzo ya Biashara kwa wajasiriali wadogo na
wakati ambayo imeandaliwa na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA)
mkoani humo jana.
Na Mwandishi
Wetu, Mbeya
WAKALA wa
Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)imepewa changamoto ya kujitangaza na kutoa
elimu zaidi kwa wafanyabiashara na wajasiriamali nchini kuhusu umuhimu
wa kusajili na kuzirasimisha biashara zao.
Katibu Tawala
wa Mkoa wa Mbeya, Bi. Mariam Mtunguja, alitoa changamoto hiyo jana, mara
baadaya kukutana na wawakilishi kutoka BRELA makao makuu ambao
wapo mkoani humo ilikjutoa elimu mbalimbali kwa wafanyabiashara
kuhusu kusajili biashara.
“Wafanyabiashara
wengi hapa Mbeya hawajasajili biashara zao kutokana na kukosa elimu ya
kutosha na kutojua umuhimu wa kusajili biashara zao,” alisema Bi. Mtunguja.
Katibu Tawala
huyo pia alipongeza uamuzi wa BRELA kuzunguka mikoa kwa lengo la kujitangaza na
kuhamasisha kazi zake kwa wafanyabiashara na wajasiriamali iliwaweze
kujitangaza zaidi.
“Napenda kutoa
rai kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wote mkoani mbeya kushiriki
kikamilifu mafunzo hayo ambayo yana umuhimu katika kukuza biashara zao na
kuinua pato la taifa,”alisisitiza.
Kwa upande wake
Afisa Biashara wa Mkoa wa Mbeya, Stanley Kibakaya amesema ofisi yake
imefarijika na ujio wa BRELA na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo
kusajili na kurasimisha biashara zao,
“ Upo umuhimu
mkubwa sana kwa kusajili biashara kwani utawawezesha
kutambulika zaidi na kuweza kuwafanya kupata huduma zingine za kijamii
,”alisema na kuongeza biashara zao zitambulike zaidi na
kuweza kupata fursa za kupata mikopo na huduma zingine za kitaalam
Naye Msajili
Msaidizi Mwandamizi wa BRELA, Bi.Rehema Kitambi amesema lengo la mafunzo hayo
ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara au wajasiriamali wadogo na wakati wa
mkoa wa Mbeya kuhusu umuhimu wa kusajili biashara zao na kusajili majina ya biashara
zao.
“Mafunzo
yanawalenga sana wafanyabiashara, wajasiriamali wadogo na wakati kuhusu umuhumu
wa kusajili majina ya biashara zao,” alisisitiza Bi. Kitambi na kutoa wito wa
kujitokeza zaidi.
Akitoa ratiba
ya mafunzo kitika mkoa huo, Bi. Rehema amesema mafunzo hayo yatafanyika katika
Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo Mbeya mjini kuanzia leo tarehe 16 na
kesho, tarehe 19 watakuwa Uyole na tarehe 22 watakuwa mbalizi na kumalizia
Tunduma tarehe 25 na 26.
Kwa mujibu wa
Bi. Kitambi sambambamba na mafunzo, usajili wa majina ya biashara utakuwa
unafanyika papo kwa papo kwa gharama ya shilingi 6,000/-.
“ Huduma ya
usajili wa jina biashara imerahisishwa na kufanyika ndani
ya masaa nana tub (8 )ya kazi kitu ambacho kimeshapunguza malalamiko
yaliyokuwepo awali ya ucheleweshaji ambapo ilikuwa si chinin ya siku
saba,” alisema.
BRELA ipo
katika mchakato wa kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki wa kusajili
majina ya biashara popote nchini na nje ya nchi kwa kutumia mtandao.
Mwisho.
|
|
No comments:
Post a Comment