Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mwanga
mkoani Kilimanjaro, Profesa Jumanne Maghembe akisalimiana na baadhi ya vijana
waliofika katika uwanja wa Cleopa David Msuya kushuhudia Uzinduzi wa Mfuko wa
Uwekezaji wa Vijana wa Maghembe hivi karibuni wilayani Mwanga mkoa wa
Kilimanjaro. Mfuko huo una lengo la kuwakwamua vijana kutoka katika
umaskini
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe
akizungumza na wananchi wa jimbo la Mwanga wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa
Uwekezaji wa Vijana wa Maghembe wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro hivi
karibuni. Prof. maghembe ni mbunge wa jimbo hilo.
Na
Mwandishi Wetu, Mwanga
Kujenga uwezo wa maswala ya ujasiriamali kwa vijana kumetajwa kama njia ya uhakika kuwezesha kundi hilo kuondokana na fikra za kutaka kuajiriwa, kujiingizia kipato na kukuza uchumi katika kaya zao.
Waziri wa Maji ambae pia ni mbunge wa jimbo la Mwanga, Profesa Jumanne Maghembe amesema hayo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wakati alipokua akizungumzia mfuko wa maendeleo wa vijana wa wilaya hiyo aliouanzisha ikiwa ni njia mojawapo ya kuwajenga vijana uwezo na kujiajiri wao wenyewe.
“Tumeamua kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa vijana wa Maghembe, ili vijana waweze kukopa na kujiajiri,” alisema Waziri huyo hivi karibuni wilayani Mwanga.
Alisema jumla ya Tshs milioni 100 zimeshawekwa katika benki ya wananchi Mwanga, fedha ambazo zitasaidia kuchochea vijana wengi wanaojishughulisha na biashara wilayani Mwanga kuanza kukopa katika mfuko huo wa Maghembe.
Katika fedha hizo, Waziri Maghembe amechangia Tshs milioni 20 ambapo benki hiyo ya wananchi iliongeza kiasi kilichobaki ili kuutunisha mfuko huo kwa ajili ya kukopesha vijana na kuwawezesha kiuchumi.
“Mfuko huu
wa uwekezaji ni kwa ajili ya vijana wote wa wilaya ya mwanga, hii itasaidia
sana kuwafanya vijana waweze kukopa na hatimae kukuza vipato vyao,” aliwaambia
waandishi wa habari.
Alisema vijana watatakiwa kufungua akaunti katika benki hiyo na kuweka fedha kidogo kidogo na atakaefikisha Tshs 300,000 ataweza kukopeshwa piki piki au pampu ya kusukuma maji kwa ajili ya umwagiliaji kwa kijana atakaefikisha Tshs 200,000.
“Huo ndio msingi mkubwa wa mfuko huu tunataka vijana waondoke katika makundi yasiyofaa katika jamii,” alisema
Alisema vijana wengi wanajishughulisha na biashara ya pikipiki lakini wengi wao sio za kwao, hivyo wameona ni bora kuanzisha mfuko huo ili kila kijana atakaewekeza fedha zake benki apewe boda boda iwe ya kwake kwa kurudisha fedha kidogokidogo.
Alisema vijana watatakiwa kufungua akaunti katika benki hiyo na kuweka fedha kidogo kidogo na atakaefikisha Tshs 300,000 ataweza kukopeshwa piki piki au pampu ya kusukuma maji kwa ajili ya umwagiliaji kwa kijana atakaefikisha Tshs 200,000.
“Huo ndio msingi mkubwa wa mfuko huu tunataka vijana waondoke katika makundi yasiyofaa katika jamii,” alisema
Alisema vijana wengi wanajishughulisha na biashara ya pikipiki lakini wengi wao sio za kwao, hivyo wameona ni bora kuanzisha mfuko huo ili kila kijana atakaewekeza fedha zake benki apewe boda boda iwe ya kwake kwa kurudisha fedha kidogokidogo.
“Hii ndio fursa pekee ya kujikwamua kiuchumi vijana wangu naomba muitumie, hii ndio ajira yenu,” alisisitiza Waziri Maghembe.
Aliongeza kuwa vijana wengi wamekua wakijiingiza katika vitendo vya uvutaji bangi, utumiaji dawa za kulevya na vitendo vingine vya kihalifu kama wizi na ubakaji, hivyo ni bora wakatoka huko na kujishughulisha.
“Vijana wanahitaji kusaidiwa ni watoto wetu, hivyo njia pekee ya kuwafanya waweze kujishughulisha ni kuwajengea uwezo kwa kujiunga katika vikundi kama hivi vya bodaboda,”aliongeza.
Amesema nia ni kuwafanya vijana kuwa na nidhamu katika ufanyaji biashara, kufanya kazi kwa bidii na wakumbuke kuwa viongozi wao wanawajali kwa kila jambo ambalo wanalifanya.
“Mfuko huu si kwa wanaume tu, hata wasichana ambao wanajishughulisha na biashara za kupika vyakula nao wanaweza kukopa pale endapo watafikia vigezo vilivyowekwa na benki ya wananchi,”alisema.
Mwisho
No comments:
Post a Comment