Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA), Dkt. Adelhelm Meru akionyesha
cheti cha ushindi baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapindunzi Zanzibar, Balozi Idd Seif (wa pili kutoka kulia) wakati wa Maonyesho
ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea jijini. Wengine ni Waziri
wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (wa pili kushoto); Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Bi. Sabetha
Mwambeja (kulia) na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mushi ambaye
pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala (wa pili kushoto). EPZA ilipata ushindi katika makundi mawili ya
uendelezaji viwanda pamoja na kukuza biashara na kundi la bidhaa za
mauzo ya nje.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji
nchini (EPZA) imeibuka na ushindi mnono baada ya kupata vikombe viwili
katika Kwenye Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Dar es
Salaam yanayoendelea hapa jijni.
Mamlaka hiyo ilipata ushindi katika
makundi mawili na kupatiwa vikombe na Makamu wa Pili wa Rais wa serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar,Balozi Idd Seif wakati alipokuwa akifungua maonyesho hayo
kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Barabara ya Kilwa jijini
Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt.
Adelhelm Meru alielezea ushindi huo kuwa umekuja kutokana na juhudi za mamlaka
hiyo katika kuzitangaza huduma zake kwa watanzania na wawekezaji
wa ndani na nje ya nchi.
“Ni jambo la kujivunia kwamba tumeibuka na
vikombe viwili na hii inadhihirisha kwamba tunafanya kazi nzuri na zinaonekana
kwa watanzania na wawekezaji,”alisema Dkt. Meru.
Alisema ushindi huo umetokana na
maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa ajili ya kushiriki maonyesho hayo ya
biashara ya kimataifa Dar es Salaam
“ Maeneo tuliyoshinda ni pamoja na kundi
la uendelezaji viwanda pamoja na kukuza au kusaidia kuendeleza biashara na
kundi la la bidhaa za mauzo ya nje,” aliongeza Dkt. Meru kwa furaha kubwa.
Akizungumzia zaidi ushindi
huo, Dkt. Meru alisema mamlaka inauzoefu na ujuzi mkubwa katika
maswala haya hapa nchini na ushindi huo ulikuwa ni haki yao kuupata kutokana na
kazi zinazofanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi na wadau wote wa mamlaka.
Alisema mamlaka imekuwa ikitoa huduma
nzuri daima kwa wawekezaji na zimekuwa zikionekana na ndiyo imekuwa rahisi kwa
washindanishaji kuona na kutoa ushindi huo.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji na
Huduma wa Mamlaka hiyo, Bi.Zawadia Nanyaro alisema mamlaka inashiriki kila
mwaka maonyesho hayo na safari hii wanaendelea kushiriki na kuufahamisha umma
kazi za mamlaka.
“Tumekuja kuonyesha kazi za mamlaka na
hapa tunaonyesha mafanikio yaliyopatikana hadi sasa,” alisema, alisema
Bi.Nanyaro na kuongeza kuwa EPZA siku zote ina amini kwenye kutoa elimu kwa
Umma.
Aliongeza kusema kuwa mamlaka imetumia
fursa hiyo kuonyesha kwa vitendo kazi zake pamoja na viwanda vilivyowekeeza
chini ya mamlaka ambapo vimeshiriki na vionyesha bidhaa za mauzo ya masoko ya
kimataifa na ndani ya nchi.
Alisisitiza kuwa viwanda hivyo vinamchango
mkubwa katika maendeleo ya nchi kwa vile vimekuwa vikichangia uchumi wa nchi na
kutoa ajira kwa watanzania.
“ Tunahitaji watanzaniana waje watembelee
banda letu wajionee kazi za mamlaka ili waweze kujivunia taasisi yao hii kuwa
inafanyakazi kwa faida ya nchi,”alisema.
Pia alisema wawekezaji walioshiriki
maonyesho hayo wafike kwenye banda lao ili kuweza kuzitambua fursa za
kiuwekezaji zilizopo kwenye mamlaka hiyo.
Katika Maonyesho hayo ya 38 ya Biashara ya
kimataifa Dar es Salaam, nchi 33 zikiwemo za Kenya, Uingereaza, Marekani,
Ujerumani, Zimbabwe Japani, China Denmark ,Burundi na Uturuki
zilishiriki.
Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka ambapo
wafanyabiashara hupata fursa ya kuonyesha na kuzitangaza bidhaa zao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment