Mshauri mkuu wa Ufundi wa Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo
Haraka ( DART) Bw. Dieter Schelling(katikati) akijadidiliana
na Mkurugenzi wa Usafiri na Mipango wa Wakala, Mhandisi Serapion
Tigahwa (kulia) na Meneja wa Usalama Barabarani wa Wakala, Mhandisi Mohamed
Kuganda (kushoto) jana wakati walipofanya ukaguzi wa
kutenmbelea baadhi ya maeneo ya mradi huo katika barabara ya Morogoro jijini
Dar es Salaam jana ili kujionea maendeleo ya mradi huo ambao unatarajia
kukamilika hivi karibuni na kukabidhiwa kwa serikali.
Mshauri mkuu wa Ufundi wa Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo
Haraka (DART) Bw. Dieter Schelling (katikati) akijadiliana jambo na
Mkurugenzi wa Usafiri na Mipango wa Wakala, Mhandisi Serapion Tigahwa (wapili
kulia), Afisa Mipango Miji wa Wakala, Bw. Edwin Kema (kulia), Meneja Usalama wa
Barabara wa Wakala, Mhandisi Mohamed Kugando (wa pili kushoto) na Ofisa
Uhjamishaji Makazi, Bw. Deosdedit Mutasingwa (kushoto) ukaguzi wa
kutembelea baadhi ya maeneo ya mradi huo katika barabara ya Morogoro jijini Dar
es Salaam jana hali ya mwenendo mzima wa maendeleo ya mradi huo ambao
unatarajia kukabidhiwa hivi karibuni kwa serikali, kulia ni Mkurugenzi wa
usafirishaji wa Dart Mhandisi Tigahwa Serapion.
Baadhi ya wafanyabiashara ndogondogo wakiendelea kufanya biashara
katika kituo cha mabasi madogo ubungo jijini Dar es Salaam, licha ya kupewa
amri ya kuondoka katika ili kuepusha uharibifu wa miundombinu ya barabara
inayoendelea kujengwa katika eneo hilo, ambalo kwa sasa limegeuzwa na wafanya
biashara kuwa soko na kusababisha usumbufu kwa mafundi wa kampuni ya ujenzi ya
Strabag.
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
Wakala wa Mradi
wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umewataka wafanyabiashara
wanaotumia maeneo ya miundombinu yaliyojengwa kwaajili ya watembea
kwa miguu na baiskeli kufanyiabiashara zao kuondoka maramoja kabla
ya hatua za kisheria hazijafuata.
Aidha Wakala
amewataka wafanyabiashara hao kwenda kwenye maeneo ambayo serikali imeyatenga
kwaajili ya kufanyiabiashara baadala ya kuvamia maeneo ambayo yamejengwa
kwaajili ya mabasi yaendayo haraka.
Hatua hiyo
imekuja baada ya timu ya maafisa kutoka kwa Wakala kufanya
ukaguzi wa kuangalia maendeleo ya mradi huo umbao kwa sasa upo katika hatu za mwisho
kabla Mkandarasi haujaukabidhi rasmi kwa serikali.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika eneo la kimara jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi
wa Usafirishaji na Mipango wa DART, Mhandisi Serapion
Tigahwa, alisema ni vyema wananchi na wafanyabiashara wakatambua
kuwa serikali haimkatazi mtu kufanya biashara lakini yapo maeneo maalumu
yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli hizo.
“Tunatambua
kuwa watu wanajitafutia kipato lakini zipo sehemu zilizotengwa na mamlaka
husika kwa ajili ya kufanyiabiashara,” alisema Mhandisi Tigahwa na kuongeza
kuwa ni vyema wafanyabiashara wakaondoka kwa hiari yao sasa kabla hatua za
kisheria hazijachukuliwa.
Alisema
kmebakimiezi michache ili mradi huo uweze kukabidhiwa na kuanza kufanya kazi,
hivyo ni jambo la aibu kuanza kuharibu mundombinu na kufanya kazi kinyume na
matarajio yaliyokusudiwa.
“Barabara hizi
zimejengwa kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka na si vinginevyo” alisisitiza
Tigahwa na kuongeza kuwa maeneo yaliyojengwa kwaajili ya watembea kwa miguu
yamegeuzwa sehemu za kuegesha pikipiki na bajaj.
“Hatuwezi
kuvumilia hali hii ya uharibifu na matumizi hovyo ya miundombinu kwa hatua kali
za kisheria zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakaye kiuka maagizo hayo na
kuendelea kubaki katika maeneo ya mradi basi hatua kali zitachukuliwa,”
alisema.
Aliongeza kuwa
serikali imetumia gharama kubwa kutekeleza mradi huo wa mabasi yaendayo haraka
hivyo ni vema wananchi wakaunga mkono juhudi hizo kwa kuihafadhi na kuilinda
miundombinu iliyopo.
“Tunaomba
wananchi wainge mkono serikali kwa juhudi hizi inazozifanya kwa kuitunza na
kuilinda miundombinu hii,” Mhandisi Tigahwa alisisitiza.
Mhandisi
Tigahwa a aliwataka pia wananchi kuacha tabia ya kutupa taka hovyo
katika barabara hizo za mabasi yaendayo haraka, huku akiongeza kuwa vitendo
hivyo si vya kiungwana na ni aibu kwa Taifa.
“vitendo kama
hivi kwa kweli ni aibu, na wanaotupa taka si watoto bali ni watu wazima naomba
waache tabia hiyo Mara moja,”alisema
Kwa upande
wake, Mshauri Mkuu wa Ufundi wa DART, Bw. Dieter Schelling ambaye alikuwepo
kwenye ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya mradi alisema jitihada za makusudi
lazima zifanywe au kuchukuliawa ili kulinda miundombinu ya maradi.
“Barabara za
watembea kwa miguu lazima ziheshimiwe nazipo siyo kwa ajili ya maegesho ya
pikipiki, bajaj na kufanyia biashara,” alisema na kutaka wavazi wote kwenye
miundombinu ya mradi kuondolewa.
Bw. Schelling
pia amewaomba madereva kuwa wangalifu wawapo katika barabara ya mabasi yaendayo
haraka ili kuepusha uharibifu wa miundombinu kwenye eneo la mradi jambo ambalo
litasaidia kudumu kwa muda mrefu kwa miundombinu ya barabara hizo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment