Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania Bw. Ammish Owusu –
Amoah akizungumza na viongozi mbalimbali kutoka katika jumuiya za kiislamu,
makampuni pamoja na wateja wa benki hiyo wakati walipoandaa futari , katika
Hotel ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni
kujumuika pamoja na kuzungumza nao wakati wa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa
ramadhani ambapo waislamu duniani kote wakiwa huwa
kwenye mfungo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania Bw. Ammish Owusu –
Amoah (kulia) akizungumza jambo na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw.
Juma Reli, muda mfupi mara baada ya kupata futari iliyoandaliwa na Benki hiyo
kwa wateja wake mbalimbali, katika Hotel ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini
Dar es Salaam lengo likiwa ni kujumuika na wateja wao pamoja na viongozi kutoka
jumuiya mbalimbali za kidini wakati wa kipindi hiki cha mwezi
mtukufu wa ramadhani ambapo waislamu duniani kote wakiwa
huwa kwenye mfungo.
Na Mwandishi
Wetu
MKURUGENZI
Mtendaji wa BANK of Africa Tanzania , Bw. Ammish Owusu-Amoah,
amezungumzia amani, umoja, upendo, mshikamano wa pamoja
na kutokua na ubaguzi wa dini ni vitu pekee vilivyochangia kujenga uchumi imara
na kuleta maendeleo miongoni mwa watanzania.
“Ninastaajabu
sana kuona dini hapa Tanzania zinawavuta watu pamoja badala ya
kuwagawanya kama ilivyo sehemu nyingine duniani,” Bw. Owuso-Amoah
alitoa dukuduku hiyo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na
viongozi mbalimbali kutoka katika jumuiya za kiislamu, viongozi
kutoka makamuni mbalimbali na wateja wa benki hiyo
wakati futari jioni iliyoandaliwa na benki juzi usiku.
Amesema
anatambua kuwa ramadhani ni kipindi ambacho waislamu wanafunga kwa
ajili ya kufanya toba na kuomba kwa ajili ya wale wenye shida na kuonyesha
upendo hata kwa wale ambao ni maadui zako.
“Watanzania
hawana budi kulinda na kuimarisha misingi ambayo
imeshajengwa ya kuendelea kuheshimiana na kushirikiana kwa madhehebu
ya dini zote bila kubaguana,” alisema.
Bw.Owusu-Amoah
ambaye pia raia wa Ghana, alisema anashangaa kuona jinsi gani wanatanzania
wanashirikiana na kuweka kando tofauti zao za kidini jambo ambalo inabidi
kuingwa katika sehemu nyingine katika bara la Afrika.
Ameongeza kuwa
wao kama benki wameliona hilo na kuamua kuwakutanisha watu ili kula nao pamoja
katika kipindi hiki ili kuendeleza umoja, amani na mshikamano uliopo
miongoni mwa watanzania
Kwa upande
wake Sheikh Issa Othman Issa wa msikiti wa Mansour ulioko
upanga jijini Dar es Salaam, amesema siku 29 walizofunga wameweza kujizuiya
hivyo ni vema wakatumia fursa hiyo kujizuiya mwaka mzima ili kuendelea
kupmpendeza mungu kwa yale mazuri.
Ameongeza kuwa
kipindi hiki kimekua ni kipindi cha kheri kutokana na watu wengi kuwa karibu na
familia zao na hivyo kusaidia kuongeza upendo katika kaya mbalimbali ndani na
nje ya nchi.
“Kipindi hiki
cha mfungo ni kipindi muhimu sana kwa waislamu kati kutekeleza na kulinda nguzu
muhimu ya dini ya kiislamu,” alisisitiza na kusema kuwa Watanzania ni wamoja
siku zote.
Hafla hiyo ya
futari iliyofanyika kwenye Hotel ya Kililimanjaro Hyatt Regency ilihudhuriwa
pia na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Bw. Juma Reli.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment