Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uendelezaji Bonde la Mto
Rufiji (RUBADA), Profesa Lucian Msambichaka akizungumza kwenye mkutano wa wadau
wa mamlaka hiyo wakati wa kutoa maoni yao jijini Dar es Salaam jana kuhusu
marekebisho ya Sheria Namba Tano ya mwaka 1975 ya mamlaka hiyo ili iweze
kukidhi mahitaji ya sasa ya mamlaka katika kuchangia maendeleo ya uchumi na
ustawi wa jamii, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw. Aloyce
Masanja.
Na
Mwandishi wetu,Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bode la Rufiji (RUBADA) wamependekeza sheria namba tano ya mwaka 1975 ya mamlaka hiyo ifanyiwe marekebisho ili iweze kutoa fursa stahiki ya utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo bila ya kukinzana au kupingana na sheria nyingine kwa ustawi wake.
Wadau mbalimbali wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bode la Rufiji (RUBADA) wamependekeza sheria namba tano ya mwaka 1975 ya mamlaka hiyo ifanyiwe marekebisho ili iweze kutoa fursa stahiki ya utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo bila ya kukinzana au kupingana na sheria nyingine kwa ustawi wake.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw, Aloyce Masanja aliwambia waandishi wa Habari jijini
Dar es Salaam jana mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa kukusanya
maoni kuhusu sheria na Kanuni zinazoiongoza RUBADA ambapo wamependekeza sheria
hiyo namba tano ni vyema ikafanyiwa marekebisho Ilikuwezesha mamlaka kutekeleza
majukumu yake vizuri.
“Wadau
wa maswala yakiwemo ya ardhi, maji,utalii, nishati, viwanda, mabonde na Taasisi
ya sekta Binafsi (TPSF) wamependekeza sheria hii ifanyiwe marekebisho,”
na aliongeza kusema sheria hiyo inamapungufu mengi ambayo wadau wametaka
ifanyiwe marekebisho ili kukidhi mahitaji ya wakati huu na si vinginevyo.
Bwana
Masanja alisema sheria hiyo tangu ianzishwe haijawahi kufanyiwa marekebisho na
tayari nchi imepita katika vipindi mbalimbali ambapo mambo mengi yamebadlika
yakiwemo ya kisera na sheria.
Alisema
sheria hiyo inatoa idhini kwa mamlaka kusimamia, kuhamasisha uendelezaji wa
bonde la mto Rufiji katika sekta za Kilimo, uzalishaji umeme, utalii na
utunzaji wa maji kwa ajili ya maendeleo wananchi na uchumi wa nchi.
"Sheria hiyo kwa sasa haiwezi kufanya kazi vizuri kutokana na kuwepo kwa sheria nyingine ambazo nazo zinahusika na maeneo ya bonde hilo, ikiwemo sheria ya ardhi ya mwaka 1999, sheria Ardhi Vijiji ya mwaka 1999 na sheria za taasisi zingine,"aliongeza.
Aliongeza
kusema kuwa wadau walioshiriki katika kutoa mapendekezo hayo, waliunga mkono
sheria hiyo ifanyiwe marekebisho ili iweze kutoa fursa kwa mamlaka kuendeleza
kusimamia, kuwezesha na kuhamasisha uzalishaji katika bonde hilo.
"Mapendekezo ya wadau yamechukuliwa na yatapelekwa katika Baraza la Mawaziri, na matarajio yetu Bunge litapelekewa mwezi February 2014 ili liweze kufanya marekebisho hayo na hatmaye kupata sheria bora itakayoipa mamlaka utengamano stahili," alisisitiza mkurugenzi Huyo mkuu kwa waandishi wa Habari.
"Mapendekezo ya wadau yamechukuliwa na yatapelekwa katika Baraza la Mawaziri, na matarajio yetu Bunge litapelekewa mwezi February 2014 ili liweze kufanya marekebisho hayo na hatmaye kupata sheria bora itakayoipa mamlaka utengamano stahili," alisisitiza mkurugenzi Huyo mkuu kwa waandishi wa Habari.
Bwana Masanja amesema kuwa marekebisho hayo yakifanyika kwenye sheria Hiyo basi yatachochea uwekezaji na wananchi watapata ujuzi, teknolojia ya uzalishaji katika Kilimo na mazao mengi na kuongezwa vipato vyao.
Naye Mwenykiti wa Bodi wa Wakurungenzi ya Mamalaka hiyo, Profesa Lucian Msambichaka alisema marekebisho hayo yanafanyika ili kuwa na sheria itakayo kuwa na manufaa kwa vizazi vya sasa na vya badaye.
“Ni lazima tuwe na sheria bora, tuweze kuwa na wawekezaji katika bonde na wakulima wetu wazalishe mazao mengi yakiwemo ya mpunga, mahindi, na miwa na tujitosheleze kwa chakula na tuweze kuuza ziada nyingi kwenye masoko ya nje na kupata fedha nyingi za kigeni," alisisitiza Profesa Msambichaka ambaye amebobea katika masuala ya uchumi.
Mwenyekiti huyo wa Bodi aliongeza kuwa Tanzania hainasababu ya kuwa na uhaba wa umeme na kushindwa kuendesha Kilimo cha umwangili kwa kuwa bonde hilo limejaa raslimali lukuki zinazoweza kufanikisha maswala hayo pasipo shaka yoyote ile.
Aidha
Profesa Msambichaka aliwaomba wanasheria kuyakusanya mapendekezo yaliyotolewa
na wadau wote na kuyafanyia kazi kwa ajili kuwa na sheria ambayo itasaidia sana
ustawi na ukuaji wa mamlaka hiyo.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bi. Bertha Swai alisema RUBADA inaendesha Kilimo Ukanda wa Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) katika mikoa ya Pwani, Lindi, Morogoro, Mbeya na Ruvuma na mafanikio yake yanaonekana kwa nchi hivyo marekebisho ya sheria hiyo itaiongezea nguvu mamlaka katika majukumu yake.
“Kwa sasa tunapenda mapendekezo haya yatoe fursa kwa mamlaka hii kwenda hadi Mkoa wa Rukwa kwa sasabu mkoa huu upo katika maeneo yanazalisha mazao ya Kilimo kwa wingi nchini na sheria haitoi fursa mamlaka kufika huko,"aliongeza Bi.Swai.
Katibu Tawala huyo pia alisema kuwa kunakila sababu ya mamlaka hiyo kufanya kazi zake kwa uhuru tena bila ya kukinzana na tasisi zingine kama TANESCO, EWURA, na Utalii.
Mamlaka ya Uendelezaji wa Bode la Rufiji (RUBADA) ilianzishwa kwa mujibu wa sheria namba tano ya mwaka 1975 kwa ajili ya kuendeleza bonde la mto Rufiji.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment