Meneja
wa Tawi la Benki ya Afrika Tanzania (BOA Bank), mkoani Morogoro, Bw. Benedict
Shiwa akimkabidhi tufe Diwani wa Kata ya Kingo Bw. Fidelis Tairo , ambalo
wananafunzi wa shule hiyo watakuwa wakifanyia mazoezi kwa vitendo wakati wa
masomo yao, wanaoshuhudia ni pamoja na mwanafunzi wa sekondari ya
Kingo, Bi. Amina Uliza (kulia) mkuu wa shule hiyo Bi. Mwanzania Jambalaga wa
(pili kulia) pamoja na Afisa Uhusiano wa Benki hiyo iliyopo katika
Manispaa ya Morogoro, Bi. Neema Levi, mara baada ya kutoa msaada vitabu katika
shule hiyo jana.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Benki ya Afrika Tanzania (Bank of Africa
Tanzania) Tawi la Morogoro limekabidhi vitabu kwa shule ya Sekondari ya Kingo
iliyopo katika Manispaa ya Morogoro mjini na kuahidi kuendelea kuchagia pia
sekta nyingine pia.
Akikabidhi vitabu hiyo jana mjinini hapa,
Meneja wa tawi la Benki hiyo mkoani morogoro Bw. Benedict Shiwa, alisema benki
yake imejithatiti kutoa mchango wake katika sekta ya elimu.
“Ni wajibu wetu kuchangia pale inapobidi
na panapokuwa na hitaji nasiyo katika upande elimu bali
pia hata kwenye sekta nyingine mbalimbali,”alisema Shiwa.
Hata hivyo alikiri kuwepo changamoto
mbalimbali ambazo zinazozikabili shule nyingi hapa nchin kama vile ukosefu wa
vitabu, madawati, upungufu wa vitabu pamoja na maabara.
“Changamoto kwa kweli ni nyingi kama
nilivyozitaja ila tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu kufanikisha japo baadhi ya
hizo,”alisema
Aidha aliwataka wanafunzi wa shule hiyo
kuvitunza vitabu hivyo ili wengine wanaobaki na wale wanaokuja wapate kujifunza
zaidi na hivyo kufaulu mitihani yao.
“Utunzaji wa vitabu hivi ni muhimu sana,
mkumbuke kuwa wenzenu wanaokuja watatumia vitabu hivyo,” alisisitiza Bw. Shiwa.
Kwaupande wake, Mwalimu mkuu wa
shule hiyo, Bi. Mwanzani Jambalaga alishukuru Benki hiyo kwa mchango wake
mkubwa na kusema msaada huo umefika kwa wakati muafaka.
“Kwa kweli msaada huu umekuja wakati
muafaka tulikua tuna uhaba mkubwa wa vitabu,”alishukuru na kuiomba benki
kutochoka kuisaidia shule yake.
Bi. Jambalaga alitoa wito pia kwa taasisi
nyingine nchini kuiga mfano wa Benki ya Afrika kwa kutoa mchango au
kuzisaidia jamii ambazo zinazozungunga.
Alisema shule yake inakabiliwa na
changamoto kubwa ya uhaba wa madawati kwa baadhi ya madarasa kwa sasa.
“Bado wanafunzi wetu wanakaa chini, kwa
kweli hii ni changamoto kubwa tulionayo hapa shule ya Sekondari
Kingo,” Mkuu huyo wa shule.
Naye, Diwani wa kata ya kingo Bw. Fidelis
Tairo aliwaasa wanafunzi wa shule hiyo kuzingatia masomo yao ili wafadhili
wanosaidia wasikate tamaa kuona wanasaidia shule ambayo haifanyi
vizuri.
“Mimi ombi langu ni moja mzingatie masomo,
Benki ya Afrika wameleta vitabu nawaomba msome sana,”alisema diwani huyo.
Aidha Diwani Tairo amewataka wazazi wa
shule hiyo kuwa karibu na watoto wao kwani hiyo ni nguzo muhimu ya kufahamu
matatizo ya mwanafuzi na kuweza kumsaidia kwa haraka.
Benki ya BOA ambayo ina matawi 17 sehemu
mbalimbali hapa nchini, imejiwekea utamaduni wa kutumia sehemu ya faida yake
kuchangia maendeleo ya jamii zinazoinguka.
Mwisho
No comments:
Post a Comment