Waziri wa Maji ambaye pia
ni Mbunge wa jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari, hawapo pichani,akielezea mafanikio
mbalimbali yaliyopatikana katika sekta ya elimu na afya katika
katika jimbo lake, mara baada ya kufanya ziara ya kukagua shughuli za
maendeleo hivi karibuni.
Waziri wa Maji ambaye pia
ni mbunge wa jimbo la Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Profesa Jumanne Maghembe
katikati akitoa maelekezo kwa fundi ujenzi, Bw. Norbert Abraham ( kulia) wakati
wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na
serikali katika sekta za elimu na afya katika wilaya ya Mwanga hivi
karibuni, kushoto ni Diwani wa kata ya Kileo Bw. Kuria Msuya.
Na Mwandishi
wetu, Mwanga
Wilaya ya
Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro imeelezwa kupiga hatua kubwa katika sekta
ya elimu kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na
sekta binafsi katika kuinua sekta hiyo.
Waziri wa maji
ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe aliwaambia
waandishi wa habari hivi karibuni kuwa ushirikiano uliojengeka katika ya sekta
ya uma na binafsi umechangia mafakio ya elimu katika wilaya hiyo.
“Nina furaha
kusema kuwa Wilaya ya Mwanga imepiga hatua kubwa katika sekta ya elimu,”Prof.
Maghembe alipotakiwa na waandishi wa habari kuelezea maendeleo ya elimu jimboni
kwake.
Prof.
Maghembe alisema katika ngazi h ya msingi mwaka huu
watoto walifaulu kwa asililia 65 lakini mwaka uliopita kabla ya
mwaka 2012 watoto wa Mwanga walifaulu kwa asilimia 95.
“Wakati nachuku
jimbo hili mwaka 2000, wilaya hii ilikua na shule za msingi 93 tu, lakini hadi
kufikia sasa tunashule zipatazo 118 haya ni mafanikio makubwa sana”, alisema na
kuongeza kuwa ujenzi zaidi wa shule unaendelea.
Prof. Maghembe
alisema kwa muda wa miaka kumi mfululuzo, Wilaya ya Mwanga kwenye matokeo ya
shule za msinginimekuwa katika kapu la kumi bora ‘top-ten’ katika Mkoa wa
Kilimanjaro.
Kwa upande wa shule
za sekondari mpaka sasa, Waziri Maghembe alisema shule zipo 25 na
hivyo kufanya angalau kila kata katika wilaya hiyo kuwa na shule ya sekondari,
japo zipo baadhi ya kata zina shule mbili mpaka tatu kulingana na juhudi kubwa
za wananchi wa kata husika.
“ lengo
la serikali ni kwamba kila wilaya itakua na shule moja yenye kidato cha kwanza
mpaka cha sita katika kila tarafa, hapa mwanga malengo hayo yametimizwa katika
tarafa zetu tano,”alisema
“ Mchango wa
sekta binafsi katika kuendeleza sekta ya elimu katika jimbo hili ni mkubwa sana
na mpaka sasa kuna shule za sekondari zaidi ya 16 katika Wilaya
ya Mwanga,” alisisitiza.
Naye Diwani
wa kata ya Kileo, Bw. Kuria Msuya alisema uhamasishaji mkubwa
uliofanywa na Prof. Maghembe umeleta chachu katika upatikanaji wa mafanikio
makubwa kwenye sekta ya elimu wilayani Mwanga..
“ Mimi kama
diwani wa Kileo nasema kata yangu inatoa kipaumbele kikubwa katika elimu na
mbunge wetu yupo nyuma kuunga mkono jihada zetu na mafanikio yanaonekana na
mwenye macho haambiwi aone,” alisema Bw. Msuya.
Alisema
mbali ya elimu, Bw. Msuya alisema ukaribu unaaonyeshwa na Profesa Maghembe
umeleta mafanikia makubwa katika sekta nyingine mbalimbali muhimu
katika wilaya Mwanga,
“ Tumepiga
hatua katika eneo la afya, elimu, miundo mbinu na sasa suala la maji
linatekelezwa kwa kasi kuhakikisha maji yanakua ya kutosha hapa mwanga,”alisema
Bw. Msuya na kuongeza kuwa wanamwanga wana matumaini makubwa na mbunge wao.
Naye Bi.
Ingia Yoel , mkazi wa Mwanga mjini alisema anashukuru kwa kuwepo na vituo
vingi vya afya katika wilaya hiyo na kuongeza kua kwa sasa suala la afya
limepata suluhisho la kudumu kutokana na huduma kuwa karibu na wananchi.
“ Akina mama
kwa sasa tumepata ahueni ya kutembea mwendo mrefu kupata huduma za afya, vituo
vipo karibu sana na wananchi,”alisema Bi. Ingia na kumshukuru sana
WMaghembe..
Mwisho.
No comments:
Post a Comment