Monday, May 19, 2014

Benki ya Wanawake kuwahudumia watanzania ughaibuni

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), Bi. Margareth Chacha akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio nchini Marekanin hivi karibuni huko Chicago.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENKI ya Wanawake Tanzania (TWB) imeanziasha utaratibu  au hudama wa kibenki ambayo itawawezesha wanawake wa Kitanzania wanaoishi ughaibuni kuchangia katika shughuli mbalimbali za kijamii na uchumi hapa nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bi. Margareth Chacha,aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuwa hivi karibuni wanawake waishio Washington, Virginia and Maryland (DMV) walituma mwaliko kwa benki yake kwenda kuwaelezea ninamna gani watanufaika endapo watawekeza kwenye benki hiyo..

“Nilikutana nao Chicago na tulikuwa na mazungumzo marefu na yaliyozaa matunda na vilevile niliwahakikishia ni namna gani benki ilivyojidhatiti kuwajengea uweza wanawake na vijana hapa nchini,” aliongeza.

Alisema wanawake hao pia walitaka kujua kama TWB ina sera yeyote ambayo inaweza kuwasaidia wanawake ambao wanaishi ughaibuni na pia kutoa kipaumbele kwa ukombozi wa mwanamke( women empowerment).

Bi. Chacha alisema, Watanzania wengi wanaoishi Marekeni na nchi nyingine za ughaibuni wanashindwa kuunga mkono shughuli mbalimbali za kijamii na maendeleo hapa nchini kwa sababu wanawasiwasi ya kupotea kwa fedha zao.

“Tulijadiliana kwa kirefu na kukubaliana kuwa benki itakuwa inasimamia pesa zao zinafanya kazi ambazo wamekusudia,” aliongeza mkurugenzi huyo mtendaji.

Kwa mujibu wa Bi.Chacha, wanawake hao waishio ughaibuni mara nyingi huwa wanashindwa kununua bidhaa kutoka Tanzania kwa kuhofia gharama na mara nyingine inalazimika kumtuma mtu kuja kuzifuata.

“Tumewathibitishia kuwa Benki ya Wanawake watasimia ununuzi wa bidhaa hizo toka Tanzania na kuzituma Marekani bila kupitia mkononi mwa Dalalali,” alisisitiza Bi.Chacha.

Amesema benki yake imeshafungua mtandao ambao utakaotumiwa na wanawake hao kutoka Tanzania iliwaweze kuingiza na kutoa pesa bila wao kuwepo Tanzania.

“Benki ya Wanawake imeona kuna fursa kubwa endapo watanzania waishio ughaibuni watashirikishwa vilivyo katika kuchangia kwenye shughuli za kijamii na uchumi,” alisisitiza Bi.Chacha.

Bi. Chacha alisema kuwa watanzania wengi aliokutana nao Marekani wameonyesha nia kubwa ya kuja kujenga nyumba/makazi hapa Tanzania na wameiomba benki isimamia mchakato mzima wa upatikanaji wa viwanja.

Tangu kuanzishwa kwake ndani ya miaka minne tu, Benki imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa inamkoa mwanamke mjasirialiamali na kijana katika kukuza biashara na kuongeza kipato. Tayari imeshatoa zaidi ya bilioni ishirini mikopo kwa wajasiriamali wa wanawake na vijana ilikukuza mitaji yao.

Mwisho.

No comments: