Thursday, September 19, 2013

Mzumbe, Ubelgiji zaimarisha ushirikiano

Na Mwandishi wetu, Morogoro
 Serikali ya Ubelgiji imesema kuwa itaendeleza ushirikiano wake na Tanzania kusaidia maeneo mbalimbali yatakayochangia kuchochea kasi ya ukuaji uchumi yenye tija kwa nchi zote.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Balozi Koenraad Adam wakati akizindua Mradi wa programu za utawala bora na ujasiriamali kupitia tafiti, elimu na teknolojia uliofanyika katika chuo kikuu Mzumbe ukishirikisha taasisi za elimu ya juu za ndani na nje ya nchi jana.

“Mradi huu una faida kwa nchi zetu kupata na kubadilshana uzoefu ya namna gani tunaweza kuunganisha nguvu zetu ili kujiletea maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizopo”, alisema.
Alisema kuwa taasisi za elimu ya juu zina mchango mkubwa kusaidia maendeleo ya jamii kwa kutafuta suluhu ya changamoto za kijamii na kiuchumi kupitia tafiti mbalimbali hivyo kuwa na njia mbadala za utatuzi wa changamoto hizo.

Alongeza kuwa pamoja na mambo mengine mradi huo utahusisha ufadhili wa masomo katika ngazi za shahada ya kwanza, ya pili, uzamili na uzamivu hivyo kuzijengea uwezo taasisi za elimu juu nchini kuwa na wataalamu watakaosaidia kuandaa wahitimu katika fani mbambali ili kusaidia kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Mradi huu utahusisha kubadilshana wanataaluma na kufanya tafiti mbalimbali katika nchi zetu”, na kuongeza kuwa hiyo itasaidia kugundua na ktatua changamoto mbalmbali zinaoikabili jamii. 
Alisema kuwa utawala bora katika rasilimali utasaidia kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali kwa vizazi vya sasa na vujavyo.

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe(Taaluma) Prof.Josephat Itika alisema kuwa utekelezaji wa programu hiyo una manufaa makubwa sio tu kwa chuo bali pia jumuhiya katika ngazi za halmashauri, kata hadi vijiji.

“Programu hii inajenga uwezo wa chuo kuwa na wataalamu katika meaneo ya utawala bora, tafiti, ujasiriamali,na tenkolojia na habari” alisema.

Aliongeza kusema kuwa maeneo hayo ni muhimu kwa ajili ya kufungua fursa za ujasiriamali, kuondoa umaskini na kukuza uchumi nchini.

Akitolea mfano wa  Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) alisema kuwa programu hiyo inagusa maeneo yote muhimu na kubainisha kuwa taasisi za elimu ya juu zinawajibu katika kufanikisha utekelezaji wa mpano huo.

“Taasisi za elimu ya juu zina jukumu la la kusaidia juhudi za serikali kujenga mazingira yatakayosaidia wahitimu waweze kuchangia kwenye kasi ya kuleta matokeo makubwa kwa haraka”,alisema.
Aliongeza kusema kuwa programu hiyo itawawezesha wanafunzi watakaohitimu na kuwa na uwezo wa kufungua fursa za kuibua miradi mbalimbali amabayo itachangia kukuza uchumi hivyo kupunguza umaskini.

Kwa mujibu wa balozi wa Ubelgiji mradi huo utahusisha vyuo vikuu viwili amamabvyo ni Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela kwa gharama kwa bajeti ya Euro billion 1.5 kila chuo kwa miaka sita hadi hadi 12 amabayo inaweza kuongezwa.


Mwisho

No comments: