Na Mwandishi wetu, Dar es
Salaam.
Serikali katika mwaka wa
masomo wa 2013/14 imewapangia mikopo wanafunzi wa elimu ya juu 29,754 sawa na
aslimia 94.04% katika malengo yake ya kuwakopesha wanafunzii 31,647.
Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Bw. Cosmas Mwaisobwa aliwaambia
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati akizungumzia utaratibu wa
utoaji wa mikopo hiyo kwa wanafunzi wapya na wanaoendelea na elimu ya juu.
“Uchambuzi wa maombi ya mikopo kwa mwaka huu wa
masomo umekamilika,”na aliongeza kusema lengo la serikali ni kuwawezesha
wanafunzi wa elimu ya juu kwa muda muafaka.
Alisema kuwa mchanganuo wa utuoaji wa mikopo hiyo ulizingatia vigezo
na masharti ya uombaji mikopo na ruzuku.
Alisema kuwa idadi ya waombaji wapya
waliotuma maombi ya mikopo ni 53,239, waombaji wanaoendelea na masomo 43,032,
waombaji waliokuwa na maombi yenye matatizo ni 6,364.
“Wengine ni waombaji waliorekebisha
matatizo kwenye maombi yao 3,151 na waombaji ambao hawakurekebisha matatizo
kwenye maombi yao 3,213”, alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu mchanganuo huo
alisema waombaji wapya 53,630 watakaosoma
ndani na nje ya nchi wamepata mikopo hiyo.
Alisema maombi ya mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea 61,692 ambao
wanasoma ndani na nje ya nchi wamepangiwa kupata mikopo hiyo.
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu inatarajia kutoa mikopo ya sh.306
bilioni kwa ajili ya ukopeshaji wanafunzi wapya na wanaoendelea na masomo.
Alisema mchakato wa upangaji wa mikopo unaendelea vizuri ambapo
hadi sasa umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.
“Matarajio ni kukamilisha mchakato huu kwa asilimia 100 ifikapo
wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kabla ya Vyuo vya Elimu ya Juu kufunguliwa, kwa
mujibu wa Tume ya Vyuo Vikuu”, alisema.
Aliongeza kusema orodha kamili ya waombaji wapya waliopangiwa
mikopo inapatikana kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo (www.heslb.go.tz)
ambapo mwombaji anaweza kutafuta jina lake kwa kutumia namba ya mtihani ya
kidato cha nne.
Alisisitiza kuwa taratibu za kupeleka mikopo
yao vyuoni zinaendelea na kwamba watalipwa baada ya kufanya usajili.
Aidha, ailisistiza umuhimu wa kila mwombaji
kuwa na akaunti ya benki kwa ajili ya kupitishia mikopo hiyo.
Aliongeza kusema kuwa waombaji waliofanikiwa
kupangiwa mikopo wanawajibika kurejesha mikopo hiyo baada ya kuhitimu masomo
yao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment