Mkurugenzi Mtendaji wa
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bi. Juliet kairuki (kushoto) akizungumza na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara Tanzania (TANTRADE), Bi.
Jacqueline Maleko (kulia) wakati wa kongamano la uwekezaji kanda ya kaskazini
mwishoni mwa wiki mjini Tanga. Katikati
ni afisa mwandamizi toka TIC, Bw. Patrick Chove
Gavana wa Anjouan, Bw. Anissi Chamasidine (kulia) akibadilishana nyaraka za makubaliano
ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji na mkuu wa mkoa wa Tanga, Bi. Chiku
Gallawa wakati wa kongamano la Uwekezaji mwishoni mwa wiki mjini Tanga. Kisiwa hicho kimefikia makubaliano hayo na
mikoa minne ya kanda ya kaskazini.
Wengine katika picha ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdalah
Kigoda (wa pili kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na
Uwekezaji, Dkt. Mary Nagu (wa pili kulia).
No comments:
Post a Comment