Maneja wa
Shamba la Kampuni ya EcoEnergy, Bw. Andre’ Fred’ Herbe( wa pili kushoto) akielezea
jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji nchini (TIC),Bi Juliet
Kairuki (wa pili kulia) maendeleo ya shamba la miwa la kampuni ya EcoEnergy
lilopo Bagamoyo hivi karibuni. Wa kwanza
kulia ni Meya wa mji wa Vallejo uliopo katika
Jimbo la California Marekani, Bw. Osby Davis na Meneja mradi wa Kampuni ya
EcoEnergy, Bw. William Burston (kushoto).
Bi. Kairuki na wafanyabiashara hao walitembelea shamba hilo kujionea
mfano halisi wa uwekezaji hapa nchini.
Na Mwandishi Wetu, Pwani
Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesifu Kampuni ya EcoEnergy Tanzania kuwa shughuli zake za
Kilimo zinazolenga kupunguza tatizo la uhaba wa sukari na nishati ya umeme.
Mkurugenzi wa Mtendaji wa kituo hicho, Bi Juliet
Kairuki alisema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea shamba kubwa la miwa
linalomilikiwa na kampuni hiyo katika bonde la mto Ruvu.
“Tumekuja kujionea maendeleo ya shamaba hili ambalo ni
moja ya miradi mikubwa ya kilimo hapa nchini,” alisema Bi Kairuki.
Shamba hilo linazalisha zao la miwa kwa nia ya kuzalisha
sukari na kutengezea nishati ya umeme.
Katika ziara hiyo aliambatana na ujumbe wa wafanyabiashara
kutoka mji wa Vallejo ulipo jimbo la California Marekani ambao walikuwa
wakiongozwa na Meya wao, Bw.Osby Davis.
Alisema wafanyabiashara hao walitembezwa katika mradi wa
shamaba hilo la miwa kwa nia ya kuwavutia kuja kuwekeza nchini katika sekta
mbalimbali ikiwemo ya Kilimo.
“Mradi huu
unatarajia kuajiri watu wengi,”aliongeza kusema Bi. Kairuki akielezea zaidi
mradi huo.
Aliwaambia wafanyabiashara hao kuwa serikali inatoa
vivutio mbalimbali vya uwekezaji, na kufanikiwa kwa mradi wa shamaba hilo la
miwa ni matokeo ya vivutio hivyo.
Alisema mradi huo una manufaa makubwa kwa taifa kwa
kuwa utasaidia kuleta ujuzi na teknolojia kuhusiana na kilimo cha kisasa cha
miwa hapa nchini.
Naye Meya Davis alisifu harakati zinazofanywa na
Tanzania katika kuinua Kilimo na shughuli nyingine za biashara na uchumi
zinazofanyika hapa nchini.
“Tumejionea mradi huu mradi huu wa miwa unavyoendelea...ni
matumaini yangu umewavutia wafanyabiashara toka Vallejo kuja kuwekeza Bagamoyo,”
alisema.
Katika hatua nyingine Meya huyo pia alitumia ziara
hiyo kutembelea shule za Msingi Majengo na Mbaruku za mji wa Bagamoyo na kutoa
zawadi mbalimbali.
“Tunatambua kuwa njia kuu ya kupata maendeleo na
kukuza uchumi ni kuwekeza katika elimu,” alisema na kuongeza kuwa wameamua
kusaidia kuwekeza katika watoto hao.
Alisema misaada hiyo waliyoitoa ni sehemu ndogo tu,
kwa kuwa mji wa Bagamoyo na Vallejo ni marafiki, hivyo uongozi wa mji huo
unalenga kuleta maendelea zaidi ya kiuchumi na kijamii katika mji wa Bagamoyo.
Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kiliandaa ziara ya
ujumbe wa wafanyabiashara kutoka mji wa Vallejo ambao walitembelea miradi
mbalimbali ya maendeleo katika mji wa Bagamoyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment