Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi.
Juliet Kairuki (kushoto) akimkaribisha Mtoto wa Mfalme wa Sweden, Victoria jana
jijini Dar es Salaam aliyeongoza ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji toka
nchi hiyo kutembelea Kituo hicho jana kama moja ya ratiba yao katika ziara yao
hapa nchini.
Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
SERIKALI imeelezea matumaini yake
kuwa ujio wa Malkia Mtarajiwa Princess Victoria wa Sweden utasaidia
kutaitangaza Tanzania kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja kuwekeza katika
sekta mbalimbali za uchumi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu
aliwambia wandishi wa habari mara baada ya kufanya mazungumzo
na malkia huyo na ujumbe wake
wa watu 11 kuwa ujio huo ni fursa pekee kwa Tanzania kunadi vivutio
vya uwekezaji kwa wawekezaji wa nchi hiyo.
“Katika mazungumzo yetu na
Malkia na ujumbe wake tumeweza kuwaeleza fursa mbalimbali zilizopo
hapa nchini zikiwepo katika maeneo ya Kilimo, utalii, madini na
viwanda vya na nishati,” alisema.
Alisema ujumbe huo pia uliambatana na
waziri wa Viwanda wa nchi hiyo,Bi. Ewa Djorling na alivutiwa na fursa hizo na
vivutio mbalimbali ambavyo vinatolewa hapa Tanzania kwa wawekezaji.
“Ujio wa Malkia huyu utaitangaza Tanzania
kwa wasweden kuwa nchi yetu ni kitovu cha uwekezaji na biashara,” alisema na
kuongeza kuwa wameonyesha nia zaidi katika sekta nishati, Kilimo , usafirishaji
na utalii.
Amesema mpaka kufika Desemba 2013, Sweden
ilikuwa na maslahi katika miraji ya uwekezaji iliyosajiliwa kufikia 59 yenye
thamani ya dola za Kimareka 494.16 hapa nchini.
“Ni uwekezaji mkubwa sana na hivyo miradi
hiyo ilikuwa inatarajia kutoa ajira 6,510.26,” alisema na kuongezwa kuwa miradi
hiyo ipo katika maeneo ya Kilimo, mawasiliano,viwanda,usafirishaji na utalii.
Pia Tanzania itapata mitaji na teknolojia
na hii ni kutokana na nchi hiyo imeendelea na wanamitaji ya kuja kuwekeza na
wakiwekeza Tanzania itaboresha ustawi wa watu wake.
Tanzania inapiga hatua katika utalii
maeneo mengi ya utalii sasa ili tuzidi kuboresha tunahitaji wajekujenga hotel
za kisasa ili tuweze kupata watalii wengi toka katika mataifa ya Ulaya, ASSIA
na Amerika.
Alisema pia wamewavutia kuwekeza kwenye
uzalisha bidhaa na kutoa huduma mbalimbali na watazipeleka kuuza katika nchi
zao na hapo Tanzania itakuza biashara za nje na kuongezwa mapato yake.
“Hivi karibuni tumezindua mradi mkubwa wa
Wasweeden wa Kilimo wa EcoEnergy Tanzania wa Bagamoyo wanalima miwa ili badaye
watengene sukari na mabaki ya miwa kutengeneza nishati ya umeme.
Matarajio kuwa ujio wa Malkia huyo na
mradi huo wa Kilimo utawavutia sana wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja kuwekeza
nchini.
Alisema pia wamesema ili waje kuwekeza
nchini wanahitaji miundombinu ya bandari iwe imeboreshwa ili kuwa na uhakika wa
kupeleka bidhaa na huduma nje ya nch.
Pia Tanzania pamoja na kwamba haina
miundombinu ya kutosha, wao wanayofursa ya kuja kuwekeza katika reli ya kati ,
reli ya kaskazini na bandari zetu ili kuwa na ufanisi mkubwa wa kuagiza bidhaa
nje na kutoa nje.
Waziri wa Viwanda na Bishara, Dkt.
Abdallah Kigoda alisema ujio huo uliwapa fursa ya kuzungumza namna ya kuondoka
katika utaratibu wa kupeana misaada na kuingia katika biashara.
“Tunahitajika kuondoka katika mahusiano ya
kupeana misaada na sasa kuingia katika mahusiano ya kibiashara zaidi,” na hii
ndiyo njia pekee ya nchi hii kujitegemea zaidi aliongeza kusemba Dkt. Kigoda.
Katika kufanikisha swala hilo, ni lazima
Tanzania iongeze uwezo wa biashara na uwekezaji ili kuweze kuuza zaidi kupata
mapato yatakayo saidia kukuza ustawi wa jamii.
Pia kunahitajika kuongeza vivutio vya
uwekezaji ili waweze kuwekeza, na katika hili kunahitaji zaidi la kutimiza
vigezo vinavyopimwa na Benki ya Dunia vya usndani wa mazingira bora ya biashara
na uwekezaji.
Alisema vipo vigezo vya kiushindani
ambavyo tayari vimemesha vitimizwa na wanaendelea kufanya hivyo lakini
kunavingine vinahitaji kuwezeshwa.
Alisema mfano vigezo vinayohitaji
teknolojia wanahitajika kuisaidia Tanzania ili kutimiza na hiyo itasaidia
kupata uwezo wa tufanya kazi kwa ufanisi.
MKutano huo uliandaliwa na Kituo cha
Uwekezaji nchi TIC,Bi.Juliet Kairuki na ulihudhuriwa na taasisi mbalimbali za
serikali zinazohisiana na maswala ya biashara.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment