Na
Mwandishi wetu, Mtwara
Zaidi
ya tani milioni mbili za saruji zinatarajiwa kuzalishwa nchini kwa mwaka mara
baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea simenti cha Dangote
katika Mkoa wa Mtwara.
Pamoja
na kiwango hicho cha simenti kuzalishwa, pia inatarajiwa kupatikana kwa ajira
400 za kudumu ujenzi huo utakapokamilika.
Uwekezaji
huu unafanywa na tajiri maarufu raia wa Nigeria, Bw. Aliko Dangote ambaye ana
vitega uchumi vikubwa katika nchi mbalimbali duniani.
Hayo
yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),
Bw. Raymond Mbilinyi alipofanya ziara katika eneo ambapo uwekezaji mkubwa wa
ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dangote unatarajia kuanza Mkoani Mtwara.
“Kukamilika
kwa mradi huu mkubwa katika mkoa wa Mtwara kutazalisha zaidi ya tani milioni
mbili za saruji, lakini pia ajira za kudumu zaidi ya mia nne zitapatikana, hii
itasaidia kukuza uchumi wa watu wa kusini na kuongeza pato la taifa kwa ujumla,”
alisema Mbilinyi mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari mkoani humo.
Akielezea
umuhimu wa ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kinatarajia kukamilika baada ya
miezi kumi na nane, Bw. Mbilinyi alisema uwekezaji wa aina hii si tu utaweza
kuzalisha ajira nyingi kwa watanzania bali utaongeza kasi ya kuchochea
uwekezaji zaidi katika mikoa ya kusini mwa Tanzania.
“Kwa
takwimu tulizonazo, hadi kufikia mwaka 2011 tulikua na upungufu wa zaidi ya
tani milioni moja za simenti, hivyo kiwanda hiki kitasaidia kuondoa upungufu
huu,” alisema.
Alisisitiza
kuwa mazingira mazuri yalijengwa na serikali pamoja na sekta binafsi ndio
yaliyosaidia kumpata muwekezaji huyu mkubwa wa simenti katika Bara la Afrika
kuja kuwekeza hapa Tanzania.
“Juhudi
zetu zote kwa upande wa serikali na kwa upande wa sekta binafsi ndizo
zilizosababisha muwekezaji huyu mkubwa kuja hapa kwetu hasa katika mkoa wa
mtwara na kanda ya kusini kwa ujumla,” alisema na kuongeza kwamba serikali
itaendelea kujenga mazingira bora ya kuvutia wawekezaji, si tu kwa viwanda vya
simenti bali hata kwa viwanda vya aina nyingine.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kanali
Mstaafu Joseph Simbakalia,
alisema ujenzi wa kisasa siku zote unahitaji saruji hivyo uwekezaji huo umekua
mkombozi kwa watu wa mikoa ya kusini na Tanzania kwa ujumla.
“Kukamilika
kwa kiwanda hiki kutakuwa na faida kubwa sana kwa mkoa huu, hasa kiuchumi
kutokana na mtwara kuwa na mafuta pamoja na gesi asilia ambayo inaweza kuongeza
asilimia kubwa ya pato la Taifa na kuondoa umasikini katika nchi,” alisema
Simbakalia.
Bwana
Simbakalia aliongeza kuwa ni ukweli usiopingika kuwa Mkoa wake una ufursa
nyingi sana za uwekezaji na miongoni mwao bado hazijafanyiwa uwekezaji
unaotakiwa.
Naye
mtaalamu wa masuala ya utafiti wa udongo kutoka katika kampuni ya simenti ya
Dangote Bw. John Olalokun,
amesema, wamefanya utafiti wa kutosha na kuona kuwa malighafi nyingi
zinapatikana katika eneo husika na kuongeza kuwa hiyo ni faida kwao katika
kuzalisha simenti kwa wingi mkoani humo.
Aliongeza
kuwa kati ya walivyoangalia kufanya uwekezaji katika mkoa wa Mtwara ni kutokana
na upungufu uliopo wa simenti katika mikoa ya kusini na hii imetokana na
simenti nyingi kuelekezwa katika mikoa ya kaskazini mwa nchi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment