Na
Mwandishi watu, Dar es Salaam
Rais
Jakaya Kikwete anatarajia kufungua rasmi kambi yaya kwanza vijana katika kilimo
na maarifa ya Mkongo iliyo katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani Jumamosi wiki
hii.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji Bonde la Mto Rufiji
(RUBADA), Bw. Aloyce Masanja ambao ndio waanzilishi wa kambi hiyo, uanzishwaji
wa kambi hiyo ni moja ya utekelezaji wa kuwashirikisha vijana kwenye kilimo.
“Mpango
huu ni sehemu ya utekelezaji wa mageuzi katika sekta ya kilimo wenye lengo la
kuwabadilisha kimtazamo vijana ili kukubali na kuona kuwa kilimo kinalipa,”
aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Bw.
Masanja alisema kuwa mpango huu unawajengea uwezo vijana ili waweze kushiriki
ipasavyo kwenye shughuli za kilimo na unalenga katika maeneo yaliyochaguliwa
kwa ajili ya Matokeo Makubwa Sasa kwenye bonde la mto Rufiji.
Pia
alisema ni utekelezaji wa mpango wa kukuza kilimo katika ukanda wa kusini mwa
Tanzania (SAGCOT) ambao unalenga kuleta mapinduzi ya haraka ya kilimo kikanda
unaojumuisha jitihada na nguvu za pamoja za wadau mbalimbali.
RUBADA
inatekeleza mpango huu kwa mtindo wa “Hub and Spoke” ambapo mwekezaji mkubwa wa
ndani au wa nje anakuwa “Hub” na wakulima wadogo wanakuwa “Spoke” wote kwa
pamoja wakisukuma gurudumu la maendeleo.
Akifafanua
zaidi alisema mtindo huu unahusu kuanzisha kambi za vijana kwa kila eneo lenye
mwekezaji mkubwa katika bonde zima la mto Rufiji linaloanzia mkoa wa Pwani,
Morogoro, Iringa, Mbeya, sehemu ya Dodoma, Singida, Ruvuma na Lindi.
Bw.
Masanja alisema kufuatana na mkakati sa SAGCOT uliobainisha kongani sita za
Rufiji, Kilombero, Ihemi, Mbarali, Ludewa na Sumbawanga; RUBADA, imeandaa
mpango kabambe wa utekelezaji ambao utashirikisha vijana katika kila kongani.
“Kwa
mwaka huu wa fedha, tunategemea kuwa na vituo vitano vya vijana katika kilimo
na maarifa na kila kituo kitakuwa na vijana wasiopungua 300 ambao watapata
mafunzo katika kipindi cha mwaka mmoja,” alisema.
Vituo
hivyo vya vijana vitakuwa na majukumu ya kutoa mafunzo kuhusiana na utekelezaji
wa kilimo bora chenye tija; kuongeza thamani mazao; matumizi ya vifaa vya
kisasa; utekelezaji wa kilimo bora bila uharibifu wa mazingira; kuandaa andiko
la mradi ili kuweza kupata mikopo katika taasisi za fedha na uundaji wa vikundi
vya ushirika.
Kwa
mujibu wa Bw. Masanja, mafunzo katika kambi hizo yatajikita katika maeneo makuu
matatu yakihusisha uzalishaji wa mazo ya kilimo kwa wingi na yenye thamani
kubwa hasa mazao ya bustani, mboga mboga na matunda; ufugaji wa kisasa wa
ng’ombe na kuku na ufugaji wa samaki pamoja na ujasiriamali.
Kwa
kuanzia, kambi ya Mkongo inaanza na vijana 50 lakini ikiwa na lengo la kuchukua
vijana 300 kwa mara moja ili kituo kiweze kufikia malengo yake.
“RUBADA
inatarajia kuzalisha vijana 600 kutoka kituo cha Mkongo hadi 2015 ambao
watakuwa na utaalamu na ujuzi wa kilimo chenye tija na ufugaji wa kisasa,”
alisema Mkurugenzi huyo.
Kilimo ni
moja ya sekta zinazolengwa katika mikakati mbalimbali ya serikali katika
mapinduzi ya kiuchumi na kufikia malengo ya Milenia na Dira ya Taifa ya
Maendeleo ya 2025.
Kulingana
na sense ya watu ya 2012, asilimia 60 ya nguvu kazi ya Tanzania ni vijana.
Mwisho
No comments:
Post a Comment