Meneja
Mwandamizi wa Masoko na Mawasiliano wa Banki ya Afrika Tanzania, Bw. Solomon
Haule (kushoto) akiongea katika shughuli ya kutoa msaada wa vitabu kwa Shule ya
Sekondari ya Mama Salma Kikwete jana jijini Dar es Salaam. katikati ni Meneja wa Tawi la Kijitonyama la
benki hiyo, Bw. Lugano Mwaipyana na Mwalimu Mkuu Msaidi, Utawala, wa Shule
hiyo, Bi. Philomena Julu (kulia). Msaada
huo ni juhudi zinazoendelea za benki hiyo kusaidia serikali katika kuendeleza
sekta ya elimu hapa nchini.
Meneja wa
Tawi la Kijitonyama la Benki ya Afrika Tanzania, Bw. Lugano Mwaipyana (kushoto)
akimkabidhi msaada wa vitabu Mwalimu Mkuu Msaidi, Utawala, wa Shule ya
Sekondari ya Mama Salma Kikwete, Bi. Philomena Julu (wa pili) jana jijini Dar
es Salaam. wengine ni wanafunzi wa shule
hiyo, Catherine Francis (wa pili kulia) na Isaya Christopher (kulia). Msaada huo ni juhudi zinazoendelea za benki
hiyo kusaidia serikali katika kuendeleza sekta ya elimu hapa nchini.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Katika kuhakikisha inaunga mkono juhudi za serikali za
kukuza sekta ya elimu hapa nchini, Benki ya Afrika Tanzania imeendelea kutumia
sehemu ya faida inayoipata kwenye shughuli zake za kibenki kusaidia shule za
sekondari za umma za kata vitabu vya masomo mbalimbali.
Safari hii, benki hiyo imetoa msaada wa vitabu kwa
shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete
iliyopo katika wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
Shule hiyo ina michepuo ya Sayansi, Biashara na yale
ya mchepuo wa masomo ya Sanaa.
Meneja Mwandamizi wa Masoko na Mawasiliano wa benki
hiyo, Bw. Solomon Haule alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa uamuzi wa kuendelea
kusaidia sekta hiyo unatokana na dhamira yao kutaka kuona inaendelea kwa kuwa
moja ya sekta muhimu kwa maendeleo.
“Benki yetu ina sera ya kujenga mahusiano mema na
jamii na mwaka huu wa fedha tumetenga sehemu ya faida kwa ajili ya sekta ya
elimu,” alisema.
Alisema msada huo unalenga kuzijengea uwezo shule za
kata zenye changamato ya vitabu ili kuwasawaidia wanafunzi wapate huduma bora.
Alisema mwezi wa Saba mwaka huu mameneja wa matawi wa
benki yao watapita katika shule mbalimbali za Kata katika mikoa yao na
kuorodhesha shule zenye mahitaji ya vitabu kwa ajili ya kuzisaidia.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Utawala, Bi. Philomena
Julu alisema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto ya vitabu shuleni hapo
na kusaidia kukuza elimu.
“Kwa kweli tunayo changamoto kubwa ya vitabu; serikali
imejitahidi lakini bado kunahitaji hili,” alisema.
Pia alisema msaada huo utasaidia katika kufikia
malengo ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na
kwa kufanya hivyo watoto watapata elimu ya kutosha.
Alisema shule yao inafanya vizuri kila mwaka na vitabu
hiyo ni chachu ya kuzidi kufanya vizuri kitaaluma.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mwanafunzi wa kidato
cha Pili, Catherine Francis alisema anaishikuru benki hiyo kwa kuwapatia
msaiada, na watahakikisha wanasoma na wanafavya vyema katika masomo.
“Tunawaomba walimu wazidi kutusaidia tuweze kuvielewa
ili tuwe na uelwa mzuri na kufaulu,” alisema.
Alisema anaomba wadau wengine nchini kuisadia shule
yao ili iweze kuwapatia elimu bora wanafunzi wake kwa faida ya taifa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment