Friday, February 21, 2014

Sherehe za uzinduzi wa mradi mkubwa wa njia mpya ya mawasiliano unaounganisha Jiji la Dar es Salaan kwa upande mmoja na Unguja na Pemba kwa upande mwingine hivi karibuni huko Mjini Pemba ulivyofana katika picha

Wawakilishi wa balozi mbalimbali na viongozi wa serikali wakiwa kwenye uzinduzi rasmi wa Mradi wa njia mpya ya mawasiliano inayounganisha Dar es Salaam kwa upande mmoja na Unguja na Pemba kwa upande mwingine kwenye sherehe zilizofanyika Pemba hivi karibuni
             Wageni mbalimbali waalikwa wakiwa kwenye uzinduzi huo mjini Pemba.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technolojia, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo muda mfupi mara baada ya  kuzinduzi rasmi wa Mradi wa njia mpya ya mawasiliano inayounganisha Dar es Salaam kwa upande mmoja na Unguja na Pemba kwa upande mwingine kwenye sherehe zilizofanyika Pemba hivi karibuni.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technolojia, Profesa Makame Mbarawa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi wa njia mpya ya mawasiliano inayounganisha Dar es Salaam kwa upande mmoja na Unguja na Pemba kwa upande mwingine kwenye sherehe zilizofanyika Pemba hivi karibuni.

Viongozi waandamizi wa Kampuni kongwe ya Simu Tanzania (TTCL) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Pemba Kusini, Mh.Mwajuma Abdallah Majid,Mkuu wa Mkoa Kusini, Meja mstaafu Juma Kassim Tindwa,Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Bw. Peter Ngota, Mshauri wa Rais wa Zanzibar (Pemba) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya TTCL,Mh.Sheha Mohamed Sheha na Mwakilishi wa Balozi wa Japani hapa nchini,Bw.Kazuyoshi Matsunaga.

No comments: