Mkurugenzi wa Uhamasishaji na huduma wa
Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Bi.Zawadia Nanyaro akitoa mada juu ya eneo maalumu
la uwekezaji la mamlaka hiyo lililopo katika mji wa Bagamoyo wakati wa mkutano
na wafanyabiashara wa mji wa Vallejo uliopo Jimbo la California nchini Marekani
na wale wa mji wa Bagamoyo jana.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Huduma wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa
Uwekezaji nchini (EPZA), Bi.Zawadia Nanyaro (kulia) akimkaribisha Meya wa Mji
wa Vallejo uliopo Jimbo la California nchini Marekani, Bw. Osby Davis, wakati
alipofanya ziara ya kutembelea eneo maalumu la uwekezaji la mamlaka hiyo
lilolopo katika mji wa Bagamoyo jana.Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Huduma wa Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Bi.Zawadia Nanyaro (kushoto) akimmwonyesha eneo maalumu la Uwekezaji la mamlaka hilo lililopo Bagamoyo Meya wa Mji wa Vallejo uliopo Jimbo la California nchini Marekani, Bw. Osby Davis (kati) na Rais na Ofisa Mkuu Mtendaji wa Globetrend Group kutoka mji huo Bw.Edem Elvis Akpokli (kulia)jana.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Huduma wa
Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Bi.Zawadia Nanyaro kati
akiwafafanulia jambo wafanyabiashara wa Mji wa Vallejo uliopo Jimno la
California nchini Marekani wakati walipofanya ziara ya kutembelea eneo maalumu
ya mamlaka hiyo lililopo katika mji wa Bagamoyo jana.
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
Mamlaka ya Ukanda Maalumu ya
Uwekezaji (EPZA) imesema mradi wa uendelezaji wa maeneo maalumu ya uwekezaji katika
mji wa Bagamoyo ukikamilika utasaidia mji huo kuwa jiji kubwa la viwanda na
biashara na kuchangia shughuli za maendeleo ya nchi.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Huduma wa
Mamlaka hiyo, Bi. Zawadia Nanyaro, aliuambia ujumbe wa wafanyabiashara kutoka mji wa Vallejo uliopo Jimbo la California
nchini Marekani ambao ulifanya ziara kwenda kujionea fursa mbalimbali za kibiashara katika
eneo hilo kuwa mji wa bagamoyo utakuwa
wa viwanda na biashara.
“Serikali imetenga eneo la hekali 22,000
sawa na heka 9,000 katika eneo hili maalumu la uwekezaji hapa Bagamoyo na
tunahamasisha wawekezaji kama wa mji wa Vallejo kuja kuwekeza hapa,” aliuambia
ujumbe huo ambao umeongozwa na Meya wa Vallejo, Bw.Osby Davis.
Bi. Nanyaro alisema kwa sasa serikali
inayomipango ya kujenga miundombinu mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafs,
hivyo wafanyabiashara hawanabudi kuchangamkia fursa hiyo kwa kuanzisha viwanda
na biashara na huduma mbalimbali.
“ Mji wa Bagamoyo kutokana na eneo
maalumu la uwekezaji kutajengwa bandari
kubwa ya kisasa kupita zote nchini ili kuunganisha na maeneo mengine ya nchi na
nje ya nchi,” alisema mkurugenzi huyo na kuongeza kuwa Bagamoyo itakuwa ni kiungo kikubwa kwa biashara
nchini.
Alisema kuna mradi pia wa kujenga uwanja wa ndege wa
kisasa na reli itakayounganishwa na reli ya kati na Tazara na miundombinu yote
hiyo inalenga kuweka mazingira bora ya kibiashara na uwekezaji.
Ugeni huo wa wafanyabiashara hao kutoka mji wa Vallejo
walitembelea maeneo hayo ya uwekezaji likiwemo eneo la heka 300 la Kamal
Industrial Estate linalomilikiwa na mtu binafsi.
“ Ujumbe wa wafanyabiashara hawa
wengi wao walionyesha kufurahishwa na serikali ya Tanzania ya kutenga maeneo
kama hayo kwa ajili ya viwanda na biashara,” aliongeza mkurugenzi huyo na
kuongeza kuwa wako tayari kuja nchini ili kuitumia fursa waliyoiona Bagamoyo kwa
ajili ya maendeleo ya nchi hizi mbili.
Naye Mwenyekiti wa Black Chamber of
Commerce na Mkurugenzi Mtendaji wa chamber hiyo ya Mji wa Vallejo,Bw. Carl
Davis, Jr alisema wao wanahitaji kufanya
biashara katika mji wa Bagamoyo kwa
faida ya miji hiyo miwili.
“Hii ni fursa kwetu kuja kufanyabiashara
hapa Bagamoyo iwe ya ushirikiano kati yetu sisi zote au kuja kuwekeza
mojakwamoja sisi wenyewe,” alisema Bw. Davis, Jr na kuongeza kuwa shughuli za biashara zikiimarishwa
zitasaidia sana mji wa Bagamoyo.
Alisema ujio wao umelenga kuona fursa
zilizopo katika mji wa Bagamoyo na pia wanapenda kuwekeza katika sekta
mbalimbali ikiwemo ya kilimo.
Bw. Davis, Jr alisema wafanyabiashara
wa mji wao wanamahusiano mazuri ya kibiashara na nchi za Afrika na tayari
wanafanya biashara katika nchi ya Ghana, Kenya na Misri na matarajio yao
kuingia Bagamoyo.
“Sisi tumejidhatiti kufanya biashara
hapa na ziara yetu imetuunganisha na nyie na tutaenda kuwa mabalozi wazuri juu
ya fursa za Bagamoyo na tutarudi tena kibiashara zaidi,” alisisitiza.
Alisema pia mji wao wa Vallejo na
Bagamoyo ni miji dada na mahusiano yaliyopo yanalenga kuendeleza mahusiano hayo
na kuingia zaidi katika biashara.
Mwisho .
No comments:
Post a Comment