Kaimu Meneja wa Kitengo cha Makasha wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Bi. Brigita Madolomani( katikati) akizungumza na waandishi
wa habari hawapo pichani, Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki juu
ya ujio wa mashine mpya na za kisasa aina ya' Gott Wald Crane' kwa ajili
ya upakuaji na upakiaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na Tanga,
kulia ni Kaimu Afisa mawasiliano mkuu Peter Milanzi na Kaimu Meneja Kitengo cha
Makasha Bi.Brigita Madolomani.Mashine hizo za kisasa kila moja imenunuliwa kwa
Ero milioni 2.6
ACTING
Communications Manager of Tanzania Ports Authority (TPA), Ms Janeth Ruzangi
stresses a point to journalists
(not in picture) in Dar es Salaam over the weekend on the four purchased modern
Gotwald habour cranes meant to increase productivity at the port each crane
bought at 2.6 million Euro. Others looking on are acting Manager of Container Terminal,
Ms Brigita Madolomani( left) and the Authority’s Principal Communications
Officer , Mr Peter Millanzi (Right). One of the acquired machine will be used
at Tanga Port.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Katika juhudi za kuboresha huduma zake,
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imenunua vifaa vinne vya kisasa
aina ya ‘Gotwald Harbour
Cranes’ kwa ajili ya kuboresha huduma za upakiaji na upakuani mizigo.
Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mamlaka
hiyo, Bi. Janeth Ruzangi alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo hayo. Vifaa hivyo vina thamani ya jumla ya
Euro 10.4 milioni.
“Vifaa hivi ni vya kisasa na kila
kimoja kimenunuliwa kwa thamani ya Euro 2.6 Milioni…vina uwezo mkubwa wa
kupakua na kupakia mizigo kwenye meli tofauti na ilivyo kuwa hapo nyuma,”
alisema Bi. Ruzangi.
Alisema sasa uwezo umeongezeka katika
bandari hiyo kwa kiasi kikubwa na kwamba hatua hiyo ni moja ya mikakati ya
kuhimili ushindani katika utoaji wa huduma hiyo katika ukanda huu.
Akielezea zaidi alisema vifaa
hivyo pia vina uwezo wa
kuendeshwa kwa rimoti na kufanya kazi kwa ufanisi na kwa umakini katika utoaji
wa huduma hiyo kwa jamii.
Alisema ununuzi wa vifaa hivyo pia
umeilenga Bandari ya Tanga ambayo imepatiwa kifaa hicho kimoja wakati vitatu
vimebaki Dar es Salaam.
“Wakala wa meli sasa walete meli zao
kwa wingi katika bandari yetu,” alisema na kuongeza kuwa wateja wote wanaotumia
bandari ya Dar es Salaam hawana budi kuzidi kutumia bandari hiyo kwa vile
huduma imezidi kuwa nzuri.
Kaimu Meneja Kitengo cha Makashi (AG
Container Terminal) wa Mamlaka hiyo, Bi. Brigita Madolomani alisema kabla ya
kuja vifaa hivyo vipya mwezi Octoba mwaka 2012, vifaa vilivyokuwepo vilikuwa na
uwezo wa kupakua na kupakia kontena 216 kwa kipindi cha saa 24.
“Lakini baada ya vifaa hivyo vipya
kununuliwa, mwezi Novemba mwaka 2012 jumla ya kontena 283 ziliweza
kushughulikiwa kwa saa 24 na idadi hiyo kupanda hadi kontena 315 kwa saa 24 kwa
mwezi Disemba,” alifafanua, Bi. Madolomani.
Alisisitiza kusema kuwa maendeleo hayo
makubwa ni hatua muhimu katika kuleta tija ya utoaji wa huduma katika bandari
hiyo muhimu katika ukanda huu wa Afrika.
Bandari ya Dar es Salaam ni moja ya
bandari ambayo hutegemewa na nchi jirani zikiwemo Zambia, Jamhuri ya Demokrasia
ya Congo (DRC), Rwanda na Burundi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment