Na Mwa ndishi Wetu, Njombe
Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto
Rufiji (Rubada) imesesisitiza kuwa itaendelea kuweka juhudi zake katika
kuhakikisha inawainua wanawake kupitia kilimo katika wake mpango wa Ukuaji wa
Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).
“Hii ni fursa ya pekee kwa wanawake
walioko katika ukanda huu wa kusini kuchangamkia nafasi hii walioipata
kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi katika kilimo, na sisi kama mamlaka
tutahakikisha tunawasaidia katika kuwajengea uwezo,” Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
hiyo Bw. Alocye Masanja aliyasema hayo hivi karibuni mjini hapa.
Akizungumza katika Mkoa mpya wa Njombe
alipokukutana na watendaji wa ngazi mbalimbali katika wilaya hiyo na kujadili
mikakati ya kuwainua wananchi wa Njombe kiuchumi kupitia mpango wa SAGCOT, Bw.
Masanja alisema kuwa RUBADA itawasaidia wanawake wote watakao changamkia fursa
zipatikanazo katika ukanda huo.
“Wanawake ni sehemu ya kilimo kwanza, hili
nimelisema mara nyingi katika ziara zangu, hivyo mamlaka itahakikisha
inashirikiana kwa karibu na taasisi za fedha kuona jinsi ya kuwainua wanawake
kwasababu asilimia kubwa ya wanawake ndio wanaojishughulisha na kilimo katika
maeneo mengi ya nchi”alisema Masanja
Aliongeza kuwa kwa sasa benki ya wanawake
ipo, na tunachofanya sasa ni kuanza mchakato wa kuingia mkataba na benki hiyo
ili wanawake waweze kukopeshwa kwa riba nafuu ili waweze kulima kilimo cha
kisasa na cha kibiashara kupitia mpango wa ukuaji wa kilimo katika ukanda wa kusini
mwa Tanzania SAGCOT.
“Wanawake ndio wanaoendesha familia
katikla maeneo mengi ya vijijini, hilo halina ubishi, hivyo mamlaka ya
uendelezaji wa bonde la mto rufiji itahakikisha kilimo kwaza na sagcot kinaenea
kwa ukubwa wake katika ukanda wa kusini,” alisisitiza Masanja.
Aidha aliwataka watendaji wa ngazi zote
katika wilaya ya njombe kuwaunga mkono ili mpango huu uweze kufanikiwa kwa
kiasi kikubwa kwa sababu serikali imedhamiria kuweka mkazo katika dhana ya
kilimo kwanza kupitia SAGCOT.
“Serikali kwa sasa inaangalia zaidi kilimo
hasa kupitia mpango huu wa Sagcot, hivyo kama msipofanya juhudi za
kuwahamasisha wananchi wenu katika vijiji, kata na tarafa mtakuwa hamuendani na
dhana ya serikali ya kilimo kwanza na mpango wa serikali yenu ni kuhakikisha
wananchi wake wanakuwa katika mazingira bora ya kimaisha” Aliongeza Mkurugenzi
huyo.
Alisema Bonde la Mto Rufiji ni kubwa sana
hivyo itakuwa si sahihi kama mamlaka kuona fursa nyngi za kimaendeleo kupitia
kilimo kwanza zinapotea pasipo wao kuzisimamia na kuzitekeleza kwa mujibu wa
sheria ya RUBADA, huklu akisisitiza kuwa Sagcot ndio itakuwa mkombozi wa maisha
ya watanzania.
Bonde la Mto Rufiji lina kongani sita,
ambazo zote ziko chini ya RUBADA kwa hiyo sisi tunaimani kubwa kuwa wananchi
waliopitiwa na na bonde hilo watafaidika na mpango wa Sagcot nah ii ndio sera
ya serikali ya kuhakikisha nchi hii inakuwa ya kijani na kuinua uchumi wan chi
kupitia kilimo” aliongeza.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment