Afisa Utekelezaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
nchini katika Kitengo cha
Magari Bandari ya Dar es Salaam, Principal Operation Officer and Head of Motor
Vehicle Section Dar es Salaam Port), Bw. Daniel Sira (wapili kusho)
akiwaonyesha stika kwenye moja ya gari ambalo limekidhi vigezo vyote vya
kuondoka bandarini. Wengine wanaoshuhudia ni Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa
mamlaka hiyo, Bi. Janeth Ruzangi (katikati), kaimu afisa mawasiliano mkuu, Bw.
Peter millanzi (kushoto) na afisa mawasiliano Mwandamizi, Bi. Levina Msia
(Kulia). Waandishi wa habari walitembelea kitengo hicho cha jana kujionea
shughuli za upakuaji magari.
Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA) imesema baada maboresho ya vitendea kazi yaliyofanyika bandari
hapo hivi karibuni, kitengo cha magari (Motor Vehicle section) kinauwezo wa
kupakua magari 1,000 kwa
shifti moja ya masaa nane tofauti na kipindi cha nyuma ilikuwa inapakua chini
ya magari 400.
Afisa Utekelezaji Mkuu ambaye ni Mkuu
wa Kitengo cha Magari Bandari ya Dar es Salaam (Principal Operation Officer and
Head of Motor Vehicle Section Dar es Salaam Port),Bw. Daniel Sira aliwaambia
waandishi wa habari waliotembelea kujionea upakuaji wa magari bandarini hapo jana kuwa huduma ya
upakuaji magari ni nzuri na inafanyika kwa haraka.
“Tumefanya hivi kwa nia ya kutaka kutoa
huduma nzuri na kwa haraka kwa wateja wetu wanaoagiza magari na wenye meli
wasiweze kutumia muda mwingi katika bandari yetu,” na kuongeza kusema kuwa
vifaa na ari ya kufanya kazi kwa bidii ndiyo imeongeza ufanisi huo.
Alisema wameboresha upakuaji kwa kuwa
na vifaa vya kutosha katika upakuaji ili kuruhusu meli kukaa muda mfupi
bandarini sababu meli ikikaa bandari muda mrefu ni ghrama na hii inavutia wenye
meli kuzidi kuleta meli zaidi kwenye bandari hii.
Alifafanua kuwa wamefanya hivyo sababu
mwenye meli na wenye magari wote ni wateja wa bandari hivyo wanategemea kazi
ifanyike kwa haraka ili waweze kuondoka kwa haraka ndiyo maana wamefanya hivyo
kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wateja wote hao.
Bw.Sira alisema utaratibu wa sasa wa
kukaguwa magari wakati wa upakuaji kutoka kwenye meli wafanyakazi wanafanya kwa
umakini mkubwa na huweka alama ya stika ya njano kwa magari yasiyo na matatizo
ya upungufu wa vyifaa,na alama nyekundu kwa magari yaliyo na vifaa pungufu.
Alisema katika eneo la upakuaji, magari
yaliyokamilika vifaa vyote yanaruhusiwa kuondoka katika eneo hilo yakiwa na
alama ya stika ya kijani na alama nyekundu kwa yale yenye matatizo kivifaa
tangu yakiwa kwenye meli.Shughuli ya ukaguzi huo inafanyika wakati wa upakuaji
kutoka kwenye meli ili kuwa na uhakika wa uzima wa magari pindi tu yanapokuwa
yanapakuliwa huku wenye meli wakiwa pale kwa ajili ya kukabidhiana.
“Zamani wakati wa upakuaji kulikuwa na
ucheleweshaji sababu kila gari likiwa nzima au linamatatizo yote yaliandikiwa
formu ya Vehicle Discharge Inspection and Transfer Tally (VDITT) lakini kwa
sasa haifanyiki hivyo.
Alisema magari mazima kwa sasa
hayaandikiwi fomu hizo, bali yanaruhusiwa kuondoka toka eneo la upakuaji kwa
kuwekewa alama ya kijani, na zile zenye matatizo kutoka kwenye meli zinaandikiwa
fomu hiyo katika eneo la upakuaji wakati wa makabidhiano na wenye meli ili
mamlaka isiweze kuingia garama ambayo haikuhusika.
Alisema pia magari yaliyoshuka ambayo
ni mazima lakini yakanyofolewa vifaa bandarini wakati wa makabidhiano na wakala
wa mizigo yanaandikiwa fomu ya Vehicle Handover (VHF) ili kuonyesha uharibifu
huo umetokea bandarini hapo.
Alisisitiza magari yakiwa na matatizo
tangia kwenye meli, wenye meli anakuwa na jukumu la kulipa gharama ya magari
kwa wenye magari sababu amesabisha uharibifu huo, na kuongeza kusema kuwa
inapotokea magari yamepakuwaliwa yakiwa yamekamilika kivifaa lakini likatokea
tatizo la kunyofolewa vifaa yakiwa bandari basi mamlaka inakuwa na jukumu la
kulipa gharama hizo kwa wenye magari.
Alisema gari likiwa na stika nyekundu
kabla ya mteja kukabidhiwa linakaguliwa upywa kati ya karani wa bandari na
wakala wa mzigo, wanasainishana kwa kuangalia vifaa vilichopungua baada ya
kushushwa kwenye meli.
“Katika mazingira hayo kama gari
limepungua vifaa likiwa kwenye meli mteja anatakiwa kumdai mwenye meli au
alikonunua na kama limepungua vifaa likiwa bandarini basi mteja aidai
bandari,”.
Pia alitoa wito kwa waagizaji wa magari
wauzaji au mtu mmoja mmoja anayeagiza gari kuwa wanatakiwa kudai fomu ya VDITT
na VHF ambazo ni nyaraka zinazosaidia kujiridhisha magari yao kama yako salama
au vinginevyo.
Alisema wenye magari wanatakiwa kudai
fomu hizo kutoka kwa wakala wa mizigo (Clearing and Forwarding Agency) ambao
wanakuwa na fomu hizo baada ya makabidhiano kati yao na bandari
Mwisho.
No comments:
Post a Comment