Wednesday, January 30, 2013

Washindi kumi wa droo ya BOA wapata zawadi


Na Mwandishi wetu
Benki ya Afrika Tanzania imetoa zawadi mbalimbali kwa washindi 10 kati ya washiriki 238 walioingia katika droo ya pili ya shindano la Weka na Ushinde kama njia ya kuhamasisha wateja wao kuzidi kuweka fedha katika sehemu salama.
Meneja Matawi wa Mkoa (Regional Branch Manager), Bw. Nelson Mgonja alichezeha droo hiyo jijini Dar es Salaam katika tawi la Kijitonyama la benki hiyo ambapo washindi wamejinyakulia zawadi mbalimbali.  
 “Kulikuwa na washiriki wengi wenye vigezo katika shindano la droo hii lakini kumi ndiyo waliokuwa na sifa  za kushinda,” na kuongeza kuwa washindi hao ni wa aina mbili yaani wateja wa rejereja na Kampuni za wajasilimali.
Alisema washindi waliopata zawani ni pamoja na UJ. Mwihome & V.J Sasa alipata 1- Phone 4 s, Wu Hua Huang Blackberry, Said Seif vocha ya kununulia mafuta ya gari, Joinven Investments T. ltd vocha ya kununua vitu super market, Mohamed Mzava Spa vocha, Shija Munawwar Dinner Voucher.
Wengine ni pamoja ni Silasi Mbaruku, Said Hamad, Emanuel Mushi, na Aljanah Company LTD wote wamepata gift Hamper (kifurushi chenye zawadi mbalimbali).
Alifafanua kwamba washindi wa rejareja wa benki ili ashinde alitakiwa kuwa na salio kwenye akaunti yake si chini ya sh. 1,000,000 na katika mwezi mmoja awe ameweka sh. 3,000,000.
Mteja wa Kampuni za wajasiliamali (SMe) awe na salio si chini ya sh. milioni 50 katika akaunti yake na kuweka sh.milioni 100 katika mwezi mmoja.
“Washindi wote kumi wameweza kutimiza masharti haya na tumewatangaza rasmi wameibuka washinda katika droo hii na kujinyakulia zawadi mbalimbali,”alisisitiza Bw. Mgonja.
Alisema washindi hao watapigiwa simu popote walipo nchini ambako kuna matawi ya benki kwa ajili ya kupatiwa zawandi zao.
Alitoa wito kwa wateja kungia katika droo ya kila mwezi ambapo kwasasa imebakia na droo ya mwezi February na March mwaka huu na pia kwaajili ya  kupata riba ya asilimia 10 iliyotengwa kwa ajili ya kipindi cha shindano.
Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT)(Gaming Board of Tanzania),Bw.Bakari Maggid alisema shindano la droo hiyo iliendeshwa vizuri na washindi walipatikana kihalali.
“Shindano limeenda vizuri na nimeona majina ya washindi wote na matarajio yangu washindi wote watapata zawadi zao kwa vile wametimiza vigezo vyote ambavyo sisi tunasimamia,”alisema Bw.Maggid.
Benki ya Afrika Tanzania ilianzisha shindano la weka na Ushinde Octoba 29, mwaka huu na linatarajia kufikia ukingoni March 2013 ambapo mshindi wa jumla atapatiwa thamani za milioni 10 au kwenda kati ya nchi ya china na Dubai.
mwisho

No comments: