Saturday, December 13, 2014

ZANTEL yatoa misaada kituo cha watoto yatima



Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Katika kuwashirikisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu msimu huu wa sikukuu, kampuni ya simu za mkononi, ZANTEL imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa kituo cha watoto yatima jijini Dar es Salaam.

Kituo hicho kilicho eneo la Kimara Suka, Watoto Wetu Tanzania kilipokea msaada wa vyakula na vitu vingine vikiwemo sukari, mchele, unga, ndoo za mafuta ya kupikia, juisi, soda, maji ya kunywa, nguo, sabuni, dawa za mswaki pamoja na madaftari.

Akikabidhi msaada huo hivi karibuni, Afisa Raslimali Watu Mkuu wa ZANTEL, Bw. Francis Kiaga alisema: “Tunafuraha kuungana na watoto leo hii na kuwakilisha kile tulichokuja nacho,” alisema.

Bw. Kiaga alisema mbali na msaada huo, ZANTEL pia inachimba kisima kwa ajili ya kituo hicho ili kiweze kuwa na maji safi na salama.

Tatizo la maji safi na salama limekuwa ni changamoto ya siku nyingi ya kituo hicho chenye watoto 54.

No comments: