Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mstaafu, Barnabas
Samatta (wa pili kulia) wakati wa mahafali ya 13 ya chuo hicho kampasi ya Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni Kaimu
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Josephat Itika (kulia); Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa
Daniel Mkude (kushoto) na Naibu Makamu
Mkuu wa chuo hicho, Utawala na Fedha, Profesa Faustin Kamuzora (wa pili kushoto
nyuma).
Na Mwandishi wetu, Dar es
Salaam
Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kimeendelea kupata mafanikio ambapo kwa sasa kinaendesha programu 11 za shahada ya uzamili huku mbili kati yake zikiendeshwa kwa ushirikiano na chuo Kikuu cha Bradford cha Uingereza ukilinganisha na programu mbili zilizokwepo wakati kampasi ikianzishwa mwaka 2005.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Josephati Itika alisema katika mahafali ya 13 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kampasi ya Dar es Salaam kuwa hatua hiyo ni fursa nzuri hasa kwa wakaazi wafanyakazi wa jiji hilo ambao wana kiu ya kujiendeleza kielimu.
Katika mahafali hayo
yaliyofanyika katika kampasi hiyo, wahitimu mbalimbali walitunukiwa shahada zao
na Mkuu wa Chuo hicho, Jaji Mstafu, Barnabas Samatta.
“Chuo kimepata mafanikio makubwa
na kinazidi kupanua programu zake ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa jiji la Dar
es Salaam wanaopenda kuendelea na masomo,”alisema.
Alisema programu hizo
zimewezesha watanzania waishio Dar es Salaam kujiendeleza kielimu
huku wakiwa wanafanyakazi.
No comments:
Post a Comment