Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya uwekezaji (TCCIA), Bw. Donald Kamori (kulia) akiteta jambo
na mmoja wa wanahisa wa kampuni hiyo, Bw. Arphaxad Masambu wakati wa mkutano mkuu wa tisa wa mwaka wa kampuni
hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Kampuni ya Uwekezaji TCCIA imeelezea kupata faida
zaidi katika mwaka 2014 kulinganisha na mwaka uliopita.
Kwa mwaka huu, kampuni hiyo imepata mafanikio makubwa
ya uendeshaji ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu inatarajia kupata
faida ya Tshs milioni 523, 651, 788 ukilinganisha na Tshs milioni 411,763, 328 iliyopata
mwaka 2013.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Donald Kamori
alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika
kwa mkutano mkuu wa tisa wa mwaka mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
“Mafanikio haya yanatokana na utendaji mzuri na
ushirikiano kati ya bodi na menejimenti yetu... tutaendelea kufanya hivyo kwa
mwaka unaokuja,”alisema.
Alisema mafanikio hayo pia yamechangiwa na uwekezaji
mzuri ambao umefanywa kwenye kampuni zinazojiendesha kwa faida na zinazolipa
gawio la hisa kila mwaka.
No comments:
Post a Comment