Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Wito umetolewa kwa Watazania kujenga tabia
ya kununua hisa katika kampuni ikiwemo ya kampuni Uwekezaji ya TCCIA kwa
maendeleo yao na taifa zima kwa ujumla.
Wito huo ulitolewa na wakala wa uuzaji
Hisa wa kampuni ya Rasilimali Limited, Bw. Arphaxad Masambu ambaye pia ni
mjumbe wa kampui ya TCCIA alipokua akitoa semina kwa wanahisa wa kampuni hiyo
hivi karibuni jijini humo.
Mtaalamu huyo alisema wakati umefika wa
watanzania kuelewa maana ya hisa na kuanza kuzinunua.
“Tunatakiwa kubadilika kwa sababu swala
hili limekuwa kama geni kwetu, sasa wakati umefika wa kuchukua hatua na kupenda
kujifunza ili hisa zitusaidie baadaye,”alisema.
Akifafanua zaidi alisema kuwa na hisa
katika kampuni ni ukombozi mkubwa katika maisha sababu fedha zinakuwa katika
mazingira salama na zinaongezeka.
Alisema kampuni ya hisa kazi yake ni
kukusanya mtaji ambao unatokana na hisa walizonunua watu na kwenda kuwekeza
katika makampuni na mashirika yanayojiendesha kwa faida.
“Kampuni ya hisa inaendeshwa kwa mujibu wa
sheria za nchi, hivyo watanzania wasisite kununua hisa katika kampuni
zinazofanya vizuri,”alisema.