Tuesday, May 21, 2013

Lukuvi ahamasisha Nyanda ya Juu Kusini kutumia sayansi na teknolojia


Na Mwandishi wetu, Iringa

Wananchi wa Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini wameaswa kutumia sayansi na teknolojia katika kilimo ili kuchochea uzalishaji katika kanda hiyo ambayo ni moja ya kanda inayotegemewa zaidi nchini katika uzalishaji mazao ya kilimo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu na Bunge, Bw. William Lukivi, amewataka wananchi wa nyanda ya juu kusini kujikita zaidi kwenye technolojia ilikuongeza thamani ya mazao yao yanayotokana na kilimo.

 Akifungua mkutano wa Kanda hiyo wa  Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya wote (Smart Partnership Dialogue) unaoratibiwa na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC)  na yaliyoshirikisha makundi mbalimbali katika jamii, mjini hapa mwisho mwa wiki, Bwana Lukuvi aliwataka wananchi kubadilika kimtazamo ilikufikia maendeleo ya kweli.


"Majadiliano haya yamekuja wakati mwafaka sababu tunataka wananchi watoe maoni yao juu ya matumizi ya sayansi na teknolojia katika shughuli za uzalishaji,"na hii itasaidia sana kuongoza katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Alisema matumizi ya sayansi na teknolojia ni mambo ambayo baada ya kupata maoni ya wananchi yataingizwa katika mikakati ya kitaifa ili yazidi kutekelezwa na kuleta msukumo mpya.

Alisema sekta zote za uzalishaji ziwemo za kilimo, ufugaji na na sekta nyingine mkoani humo zinahitajika kutumia sayansi na teknolojia kuanzia upandaji,uvunaji na upataji wa masoko.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro alisema mkoa wake unazalisha mazao ya Mpunga na matunda mbalimbali hivyo sayansi na teknolojia itumike kuanzia mbegu bora,zana za kisasa,miundombinu ya umwgiliaji na upataji wa masoko ili kuongeza vipato vyao.

"Tunategemea majadiliano haya yataibua hisia za makundi ya wananchi kuwa tunataka teknolojia itusaidie kuleta maendeleona pia kuitumia kwa ajili ya kusindika mazao,” alisema Bwana Kandoro.

Alisema pia katika kuendeleza sayansi na teknolijia ni lazima Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) viwe ni sehemu ya kuzalisha zana dogondogo katika kilimo ili kuchochea uzalishaji.

Alisema bila kuendeleza sayansi na teknolojia kupitia taasisi hizo nchi haitaweza kupiga hatua na itakuwa ni kazi bure katika kukuza sayansi hiyo na teknolojia.

Katibu Mtendaji wa TNBC,Raymond Mbilinyi alisema majadiliano hayo katika kanda hiyo yanalenga kupata maoni kutoka kwa makundi ya wananchi ili yaweze kupelekwa katika mkutano wa kitaifa na kuingizwa katika mikakati ya serikali.

"Mwaka huu kutokana na muda kuwa mfupi tumeamua kufanya majadiliano ya kikanda ili kuwahi mkutano wa kitaifa wa tarehe moja na mbili, Juni 2013 na ule wa kimataifa utakao fanyika Tarehe 28 Juni hadi tarehe moja Julai 2013,"

Alisema mwaka ujao na inayokuja majadiliano hayo yatafanyika kuanzia ngazi ya wilaya na mikoa kisha kanda na taifa.

Alisema kwa sasa TNBC inaendelea na mikatiti yake ya kuboresha Mabaraza ya Wilaya na Mikoa yaweze kufanya kazi zake katika kukuza biashara kwa kushirikiana na sekta binafsi.

kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu CCM alisema mkoa wake una fursa za kilimo na utalii katika Mto Luaha ambapo sayansi na teknolojia ikitumika itsaidia kukuza mapato ya wanachi.

"Katika kuendeleza sayansi na teknolojia hapa nchini lazima kuwe na utarajibu wa kuwatambua wabunifu kwa kuwapatia tuzo na kuwaendeleza,".

Majadiliano ya Nyanda za Juu Kusini yalishirkisha makundi ya wananchi kutoka Mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa lengo la kitaifa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwa 2020/25.ni kufikia uchumi wa kati mwaka 2020/25.

mwisho.

No comments: