Wednesday, January 30, 2013

Wajasiriamali ni nguzo ya uchumi wa taifa-TIC


Na Mwandishi wetu, Mbeya
Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesema wajasiriamali nchini wanatakiwa kuongeza nguvu zaidi katika kuendelea biashara kwa kuwa biashara zao ni nguzo ya uchumi wa nchi.
Mratibu wa Mafunzo ya Ujasiriamali wa kituo hicho, Bw.Patrick Chove ambaye pia ni mwezeshaji wa mafunzo ya ujasiriamali alisema hayo mkoani Mbeya kuwa wajasiriamali wana nafasi kubwa ya kuendeleza nchi.
Alisema hayo wakati wa mafunzo ya wajasiriamali katika mkoa huo yaliyotolewa na TIC kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) chini ya  programu ya Business Linkages ya kituo hicho.
“Taifa linatambua mchango wa wajasiriamali ndiyo maana kumekuwa na jitihada nyingi za uwekaji mazingira bora ya biashara,”na kuongeza kusema kuwa ombi kubwa kwao ni kufuata maadili ya kufanya biashara.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa wajasiriamali,TIC inazidi kuendeleza kutoa mafunzo kwa kundi hilo kwa kuwajengea uwezo wa kufanya biashara na wafanyabiashara wa makampuni makubwa.
“Tulianza kutoa mafunzo haya Jijini Dar es Salaam yakaenda Moshi na sasa yameingia Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Mkoa wa Mbeya umekuwa wa kwanza,”alisema Bw.Chove.
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inajumuisha mikoa ya Ruvuma, Iringa, Rukwa, Katavi na Mbeya yenyewe ambapo ofisi ya kanda ya TIC ndiyo inayoratibu mafunzo hayo katika eneo hilo.
Alieleza kuwa matarajio ya mafunzo hayo ni kuwafikia wajasiriamali wote katika kanda hiyo ili waweze kupata mbinu za biashara na kutoa mchango wao kwa taifa.
Alisema katika mafunzo hayo, wajasiriamali  wanafundishwa tabia za kuwa mfanyabiashara ili waweze kuwa kama wafanyabiashara wengine duniani maana tabia zao zinafanana.
Mshauri kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD), Benedict Lema ambaye pia ni mwezeshaji wa mafunzo ya ujasiriamali alisema kampuni kubwa zinashindwa kufanya biashara na wajasiriamali hapa nchini kwa kuwa baadhi siyo waaminifu.
“Badala ya kununua malighafi za wajasilimali wa hapa, wafanyabiashara wakubwa wanaagiza nje ya nchi,” alisema Bw. Lema, na kuongeza kuwa hali hii haifai kwa maendeleo yao.
Alisema ni muhimu kwa wafanyabiashara wa ndani kujitahidi kuwa waaminifu na kujituma ili kufikia viwango vya kimataifa.
Mwisho

New science, tech policy to spur development



The Minister for Communication, Science and Technology, Prof. Makame Mbarawa stress a point during a workshop to discuss on a new policy and law on science, technology and innovation in Dar es Salaam on Wednesday.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati wa mkutano kuhusiana na sera na sheria mpya kuhusiana na sayansi, teknolojia na ubunifu jijini Dar es Salaam Jumatano wiki hii.

By a Correspondent, Dar es Salaam

Tanzania expects to have a new policy and law which will help accelerate the development of science, technology and innovation for the benefit of the country’s socio economic development.

The Minister for Communication, Science and Technology, Prof. Makame Mbarawa said this when opening a one day workshop involving various professionals.

The workshop that took place at the Commission for Science and Technology (COSTECH) on Wednesday in Dar es Salaam involved participants from in and outside the country.

“We want to see how science, technology and innovation can better bring development in our country,” Prof. Mbarawa told journalists.

He explained that the existing policy and law does not talk on innovation and that the aim now is to have one that will put emphasis on innovation for the country’s economic development.

Professionals who participated in the workshop came from higher learning institutions, research bodies, private sector and officials from the governments of Tanzania and South Africa.

The ideas from the workshop’s participants will be taken into account toward formulating the country’s new policy and law that will stimulate science, technology and innovation to another level.

“The sector has so far not contributed much to progress as it should be,” he said, adding that the country will not attain sustainable development without investing in this sector.

He explained that the country’s Development Vision 2025 articulate the need for the country to embrace science and technology for sustainable development.

The Ministry’s Director for Science, Technology and Innovation, Prof. Evelyne Mbede said that the process to have a new policy and law started in 2007 and that President Jakaya Kikwete has been very instrumental in making this happen.

“The President approached UNESCO to help us in this endeavor and we collaborated in preparing a National Background Paper which we use in today’s workshop,” she said.

She said that the National Background Paper report shows where the country come from and where should go and what should be done in terms of developing science, technology and innovation in the country.

“Various institutions in our country should be involved in this process,” she said.

Professor Emrod Elisante from the University of Dar es Salaam said that Tanzania should have a well functioning system that will allow industries to thrive.

“People should be able to start and run industries if we really need to attain development,” he said.

He also noted that the politicians should let researchers implement their findings unhindered because researchers have a very crucial role to play.

On his part, a researcher from the South African based Institute for Economic Research on Innovation (IERI), Dr. Rasigan Mahavajh said Tanzania should heavily invest in science and technology for development.

“This is a very crucial area if the country wants to develop her various sectors,” he said.

Ends 

Sheria itakayoongoza maendeleo sekta binafsi yatakiwa


 The Chairperson of the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Ms. Esther Mkwizu talks to Mr. Aloys Mwamanga (centre) and the TPSF Board Member, Mr. Salum Shamte (right) during the TPSF extra ordinary general meeting held in Dar es Salaam yesterday.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Esther Mkwizu akiongea na Bw. Aloys Mwamanga (kati) na mjumbe wa bodi ya TPSF, Bw. Salum Shamte (kulia) wakati wa mkutano mkuu maalumu wa Taasisi hiyo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. 



The Chairperson of the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Ms. Esther Mkwizu (left) with the Foundation’s Executive Director, Mr. Godfrey Simbeye (centre) and a TPSF Board Member, Mr. Salum Shamte (right) during the TPSF extra ordinary general meeting held in Dar es Salaam yesterday.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Esther Mkwizu (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Bw. Godfrey Simbeye (kati) pamoja na mjumbe wa bodi ya TPSF, Bw. Salum Shamte (kulia) wakati wa mkutano mkuu maalumu wa Taasisi hiyo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Hatua ya kuundwa kwa sheria itakayoongoza ustawi, umoja na ushirikiano wa sekta binafsi Tanzania imetajwa kama muhimu na ya haraka kwa maendeleo ya uchumi hapa nchini.
Pendekezo hili liko kati ya mapendekezo saba yaliyotolewa katika mkutano mkuu maalumu wa wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Akiwasilisha mapendekezo hayo mbele ya wajumbe wa mkutano huo, Mwenyekiti wa kikundi kazi wa kamati ndogo ya wajumbe wa kamati iliyochaguliwa kuangalia jinsi ya kuimarisha sekta binafsi hapa nchini, Bw. Salum Shamte alisema jambo hilo ni muhimu sana kwa maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini.
“Tunapendekeza kuwepo na sheria ya kuendeleza sekta binafsi hapa nchini,” alisema, na kuongeza kuwa jambo hili lifanywe haraka ili kufikia malengo ya taasisi hiyo.
Mapendekezo mengine yaliyotolewa na kamati hiyo ndogo ni pamoja na kupitiwa upya kwa malengo matatu ya awali ya taasisi hiyo kuyafanya kuwa nane yakijumuisha maswala ya majukumu ya kijamii (CSR), usalama na maendeleo ya mazingira pamoja na kuhusishwa kwa wadau toka ushirika wa sekta binafsi na ya umma (PPP).
Pia mapendekezo mengine ni kugawanya wanachama wa taasisi hiyo katika makongano kumi (clusters) ili kuimarisha ushiriki wao katika taasisi hiyo.  Makundi ya kongani hizo ni pamoja na kilimo, uzalishaji, sekta ya madini, viwanda na nishati, utalii na maliasili, benki na huduma za kifedha, huduma, biashara, sekta binafsi za Zanzibar, vyama vya biashara mikoani na wajasiriamali wanawake.
“Hata hivyo makongano haya yanaweza kubadilika kadiri tunavyoendea na uchumi wa nchi unavyobadilika,” alisema Bw. Shamte, na kuongeza kuwa hilo likitokea basi namba ya makongano hayo inaweza kuongezeka na mfumo wake kubadilika.
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, wawakilishi wa makongano haya kumi ndio wataunda bodi ya TPSF, nafasi moja ikiwekwa kwa Mwenyekiti anaemaliza muda wake.  Mwenyekiti na Makamu Mweneyekiti wa taasisi hiyo watatokana na wajumbe hao kumi. 
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, makundi maalum kama wanawake, vijana na walemavu watapewa upendeleo maalum katika muundo mpya wa TPSF.
“Kuna umuhimu wa kuangalia jinsi TPSF itakavyojenga uwigo wa kupata mapato zaidi ili kuimarisha sekta hii muhimu hapa nchini,” alisema Bw. Shamte akiongeza pendekezo lingine ya kamati yake.
Wajumbe wengine wa kikosi kazi cha kamati hiyo ndogo iliyoshughulikia mapendekezo haya walikuwa ni Bw. Felix Mosha, Bw. Ali Mufuruki, Bw. Aloys Mwamanga na Dkt. Gideon Kaunda.
Kwa ujumla, wajumbe wa mkutano huo waliotoka nchi nzima walipitisha mapendekezo ya kikosi kazi cha kamati hiyo ndogo. 
Ilikubalika kwamba marekebisho madogo yaliyochangiwa na wajumbe wa mkutano huo yatazingatiwa.
katika miaka ya hivi karibuni, mchango wa sekta binafsi katika kuendesha uchumi wa nchi umekuwa ukitambulika na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali.
Mwisho 

Wajasiriamali Mbeya washuriwa kuwa wabunifu zaidi



Na Mwandishi wetu, Mbeya
Wajasiriamali wa Mkoa wa Mbeya wameshauriwa kuwa wabunifu katika biashara zao ili kuwaongezea vipato vya kutosha na kutoa ajira kwa watanzania.
Akifungua Mafunzo ya wiki moja ya wajasiriamali hao, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro aliwataka kujenga tabia hiyo katika biashara zao.
“Ubunifu katika biashara ni jambo la msingi sana, ni lazima lizingatiwe,” alisema na kuongeza kuwa katika kufanikisha hilo wanatakiwa kuondoa uoga wa kuthubutu kufanya ubunifu.
Alisema wajasiriamali hao wanatakiwa kuyatumia vizuri mafunzo hayo wanayopatiwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) ili kupata mbinu mpya za biashara.
Bw. Kandoro alisema wajasiriamali hao wanahitajika pia kuvitumia vyombo vya fedha kupata mikopo na kujenga tabia ya kuirudisha kwa wakati ili waweze kukopa tena kwa ajili ya kukuza biashara zao.
Alisisitiza kuwa mfunzo hayo yanalenga kuwaunganisha na makampuni makubwa kwa ajili ya kupata ujuzi, hivyo wana wajibu wa kuhakikisha wanaheshimu mikataba watakayoingia na kujiepusha na tabia ya ubabaishaji katika mahusiano hayo.
Alisema serikali itaendelea kuwajengea misingi mizuri ya kufanya biashara zao ili wote waweze kukua zaidi na kusaidia kutoa ajira na kukuza uchumi wa nchi.
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Daudi Riganda alisema mafunzo hayo yamejumuisha wajasiriamali 30 kutoka Mkoa wa Mbeya.
“Mafunzo haya  yanatolewa kwa mara ya kwanza katika kanda hii na yameanza kwa wajasiliamali wa Mkoa wa Mbeya,” alisema na kuongeza kuwa matarajio ni kuwafikia wajasilimali wote katika kanda yao yenye mikoa ya Ruvuma, Iringa Katavi, Rukwa na Mbeya.
TIC kwa kushirikiana na UNCTAD wanaendesha mafunzo hayo kuwajengea uwezo wajasiriamali hao kwa kuwaunganisha na makampuni makubwa kufanya biashara kwa ufanisi.
Mshauri wa programu hiyo kutoka UNCTAD, Bw.Benedict Lema ambaye pia ni mwezeshaji wa program hiyo, alisema mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wajasilimali kufanya biashara na kampuni kubwa kwa kuwasambazia bidhaa mbalimbali ili waweze kukua na kuongeza vipato vyao.
Naye mmoja wa wajasiriamali hao, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Asaky’s Investment, Bi.Sophia Abdallah alisema wao kama wajasiriamali wapo tayari kuyapokea mafunzo ili waweze kupata ujuzi wa kibiashara.
“Tunayofuraha kubwa kwa ujuzi tunaopatiwa hapa… tutaweza kundeleza zaidi biashara zetu kwa manufaa yetu, jamii na taifa kwa ujumla,”alisema.
Mwisho 

Kilimo Kwanza ni moja ya vipaumbele vyetu—Dkt. Turuka

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia imesema mkakati wa Kilimo Kwanza unaolenga kufikia mapinduzi ya kijani Tanzania ni moja vipaumbele vyake katika juhudi za kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Hii ni kwa sababu sekta hiyo ya kilimo inabeba maisha ya watu wengi hapa nchini na ikiendelezwa vizuri ina uwezo wa kubadilisha maisha ya wananchi wengi katika nchi hii ambayo ina ardhi kubwa yenye kufaa kwa kilimo.
“Tumejipanga kutumia fungu la serikali kwa ajili ya utafiti na maendeleo kusaidia tafiti zitakazosaidia maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla na Kilimo Kwanza ni moja ya vipaumbele vyetu,” Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Florens Turuka aliwaambia waandishi wa habari jana.
Kilimo Kwanza ni mkakati wa serikali unaolenga kutumia kilimo kama daraja la kufikia mapinduzi ya uchumi hapa nchini kwa kukigeuza kilimo kuwa cha kisasa zaidi kwa faida ya watanzania na taifa lote kwa ujumla zikihusishwa sekta binafsi na ile ya umma.
“Tumeamua kutumia fedha hii ya serikali inayolenga utafiti na maendeleo kusaidia tafiti zinazolenga kufanikisha Kilimo Kwanza,” alisema Dkt. Turuka.
Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo yanapewa kipaumbele kama utafiti kuhusu pembejeo na masoko ya mazao.
“Unatakiwa kuwa na soko la uhakika ili kufanikiwa katika kilimo,” alisema, na kufafanua kwamba unaweza kuwa na mazao mengi lakini kama huna soko la uhakika inakua haina faida sana.

Alieleza kwamba hii ndio sababu Wizara yake imeamua kusaidia tafiti zinazolenga kuibua fursa za masoko kwa faida ya watanzania na wadau wote wanaojihusisha na kilimo.

Aliyataja maeneo mengine yanayolengwa kama tafiti zinazohusiana na kuimarisha mnyororo ya thamani na kuongeza bidhaa za kulimo thamani.

Takwimu zinaonyesha kwamba nchi zilizoendelea hutumia hadi dola za kimarekani 180 kuongeza thamani tani moja ya mazao wakati nchi zinazoendelea hutumia dola 40 tu kuongeza thamani katika tani moja ya mazao ya kilimo.

“Eneo hili la kuongeza thamani mazao ni la muhimu sana kufanyia utafiti zaidi…ndio maana tunalipatia kipaumbele,” alisema.

Kwa mujibu wa wataalamu, bado kilimo cha Tanzania kinategemea sana wakulima wadogowadogo na kinachangia asilimia 50 ya pato la taifa na kuendesha maisha ya asilimia 80 ya wananchi wote.

Mwisho

RUBADA kuwainua wanawake kupitia SAGCOT




Na Mwa ndishi Wetu, Njombe

Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (Rubada) imesesisitiza kuwa itaendelea kuweka juhudi zake katika kuhakikisha inawainua wanawake kupitia kilimo katika wake mpango wa Ukuaji wa Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

“Hii ni fursa ya pekee kwa wanawake walioko katika ukanda huu wa kusini kuchangamkia nafasi hii walioipata kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi katika kilimo, na sisi kama mamlaka tutahakikisha tunawasaidia katika kuwajengea uwezo,” Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Alocye Masanja aliyasema hayo hivi karibuni mjini hapa.

Akizungumza katika  Mkoa mpya wa Njombe alipokukutana na watendaji wa ngazi mbalimbali katika wilaya hiyo na kujadili mikakati ya kuwainua wananchi wa Njombe kiuchumi kupitia mpango wa SAGCOT, Bw. Masanja alisema kuwa RUBADA itawasaidia wanawake wote watakao changamkia fursa zipatikanazo katika ukanda huo.

“Wanawake ni sehemu ya kilimo kwanza, hili nimelisema mara nyingi katika ziara zangu, hivyo mamlaka itahakikisha inashirikiana kwa karibu na taasisi za fedha kuona jinsi ya kuwainua wanawake kwasababu asilimia kubwa ya wanawake ndio wanaojishughulisha na kilimo katika maeneo mengi ya nchi”alisema Masanja

Aliongeza kuwa kwa sasa benki ya wanawake ipo, na tunachofanya sasa ni kuanza mchakato wa kuingia mkataba na benki hiyo ili wanawake waweze kukopeshwa kwa riba nafuu ili waweze kulima kilimo cha kisasa na cha kibiashara kupitia mpango wa ukuaji wa kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania SAGCOT.

“Wanawake ndio wanaoendesha familia katikla maeneo mengi ya vijijini, hilo halina ubishi, hivyo mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto rufiji itahakikisha kilimo kwaza na sagcot kinaenea kwa ukubwa wake katika ukanda wa kusini,” alisisitiza  Masanja.

Aidha aliwataka watendaji wa ngazi zote katika wilaya ya njombe kuwaunga mkono ili mpango huu uweze kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu serikali imedhamiria kuweka mkazo katika dhana ya kilimo kwanza kupitia SAGCOT.

“Serikali kwa sasa inaangalia zaidi kilimo hasa kupitia mpango huu wa Sagcot, hivyo kama msipofanya juhudi za kuwahamasisha wananchi wenu katika vijiji, kata na tarafa mtakuwa hamuendani na dhana ya serikali ya kilimo kwanza na mpango wa serikali yenu ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa katika mazingira bora ya kimaisha” Aliongeza Mkurugenzi huyo.

Alisema Bonde la Mto Rufiji ni kubwa sana hivyo itakuwa si sahihi kama mamlaka kuona fursa nyngi za kimaendeleo kupitia kilimo kwanza zinapotea pasipo wao kuzisimamia na kuzitekeleza kwa mujibu wa sheria ya RUBADA, huklu akisisitiza kuwa Sagcot ndio itakuwa mkombozi wa maisha ya watanzania.

Bonde la Mto Rufiji lina kongani sita, ambazo zote ziko chini ya RUBADA kwa hiyo sisi tunaimani kubwa kuwa wananchi waliopitiwa na na bonde hilo watafaidika na mpango wa Sagcot nah ii ndio sera ya serikali ya kuhakikisha nchi hii inakuwa ya kijani na kuinua uchumi wan chi kupitia kilimo” aliongeza.


Mwisho.

Washindi kumi wa droo ya BOA wapata zawadi


Na Mwandishi wetu
Benki ya Afrika Tanzania imetoa zawadi mbalimbali kwa washindi 10 kati ya washiriki 238 walioingia katika droo ya pili ya shindano la Weka na Ushinde kama njia ya kuhamasisha wateja wao kuzidi kuweka fedha katika sehemu salama.
Meneja Matawi wa Mkoa (Regional Branch Manager), Bw. Nelson Mgonja alichezeha droo hiyo jijini Dar es Salaam katika tawi la Kijitonyama la benki hiyo ambapo washindi wamejinyakulia zawadi mbalimbali.  
 “Kulikuwa na washiriki wengi wenye vigezo katika shindano la droo hii lakini kumi ndiyo waliokuwa na sifa  za kushinda,” na kuongeza kuwa washindi hao ni wa aina mbili yaani wateja wa rejereja na Kampuni za wajasilimali.
Alisema washindi waliopata zawani ni pamoja na UJ. Mwihome & V.J Sasa alipata 1- Phone 4 s, Wu Hua Huang Blackberry, Said Seif vocha ya kununulia mafuta ya gari, Joinven Investments T. ltd vocha ya kununua vitu super market, Mohamed Mzava Spa vocha, Shija Munawwar Dinner Voucher.
Wengine ni pamoja ni Silasi Mbaruku, Said Hamad, Emanuel Mushi, na Aljanah Company LTD wote wamepata gift Hamper (kifurushi chenye zawadi mbalimbali).
Alifafanua kwamba washindi wa rejareja wa benki ili ashinde alitakiwa kuwa na salio kwenye akaunti yake si chini ya sh. 1,000,000 na katika mwezi mmoja awe ameweka sh. 3,000,000.
Mteja wa Kampuni za wajasiliamali (SMe) awe na salio si chini ya sh. milioni 50 katika akaunti yake na kuweka sh.milioni 100 katika mwezi mmoja.
“Washindi wote kumi wameweza kutimiza masharti haya na tumewatangaza rasmi wameibuka washinda katika droo hii na kujinyakulia zawadi mbalimbali,”alisisitiza Bw. Mgonja.
Alisema washindi hao watapigiwa simu popote walipo nchini ambako kuna matawi ya benki kwa ajili ya kupatiwa zawandi zao.
Alitoa wito kwa wateja kungia katika droo ya kila mwezi ambapo kwasasa imebakia na droo ya mwezi February na March mwaka huu na pia kwaajili ya  kupata riba ya asilimia 10 iliyotengwa kwa ajili ya kipindi cha shindano.
Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT)(Gaming Board of Tanzania),Bw.Bakari Maggid alisema shindano la droo hiyo iliendeshwa vizuri na washindi walipatikana kihalali.
“Shindano limeenda vizuri na nimeona majina ya washindi wote na matarajio yangu washindi wote watapata zawadi zao kwa vile wametimiza vigezo vyote ambavyo sisi tunasimamia,”alisema Bw.Maggid.
Benki ya Afrika Tanzania ilianzisha shindano la weka na Ushinde Octoba 29, mwaka huu na linatarajia kufikia ukingoni March 2013 ambapo mshindi wa jumla atapatiwa thamani za milioni 10 au kwenda kati ya nchi ya china na Dubai.
mwisho

Tuna uwezo kuwa kitovu cha mawasiliano Afrika—Dkt. Turuka



Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Nafasi ya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za mawasiliano katika Kanda ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini inazidi kuwa kubwa kutokana na kuendelea kuimarika kwa mtandao wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

Tayari Mkongo huo umeunganishwa na mikongo ya baharini ya SEACOM na The Eastern Africa Submarine Cable System (EASSy) na baadaye mkongo wa The East African Marine System (TEAMS).

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki Katibu Mkuu wa Wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Florens Turuka alisema Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umefika makao makuu ya mikoa yote ya Tanzania Bara na baadhi ya makao makuu ya wilaya.

“Hapa nchini, kampuni za simu za Airtel, Infinitty, Simbanet, Tigo, TTCL, Vodacom na Zantel zimeunganishwa katika mkongo huu na zinatoa huduma zake kupitia mkongo huu katika sehemu mbalimbali,” alisema.

Serikali kupitia wizara hiyo na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) tayari imejenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wenye urefu wa kilometa 7,560, ambao unajumuisha kilometa 5,448 mpya zilizojengwa na kilometa 2,112 zilizojengwa na shirika la umeme (TANESCO) katika njia kuu za umeme.

Akifafanua zaidi alisema Mkongo huo umetoa fursa ya kuunganisha na mikongo au mifumo mingine ya mawasiliano ya nchi jirani za Kenya (Namanga, Sirari na Horohoro), Rwanda (Rusumo), Burundi (Kabanga), Malawi (Kasumulu), Zambia (Tunduma), Uganda (Mutukula) na Msumbiji (Mtambaswala).

Alisema kampuni za simu za MTL (Malawi); MTN (Zambia); MTN, RDB, Airtel, KDN, RwandaTel, na BCS (Rwanda); UCOM na ECONET (Burundi) zimeunganishwa katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.


Dkt. Turuka alisema kuwa uwepo wa Mkongo huo unawezesha utoaji wa huduma za mawasiliano katika masuala ya fedha, elimu, afya, kilimo, biashara, utalii kwa njia mtandao.

Serikali imeipa jukumu Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kuendesha, kuendeleza na kusimamia huduma zinazotolewa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa ujumla wake.

Alisema kutokana na mazingira mazuri ya kuendeleza sekta ya mawasiliano, mikongo ya mijini (metro networks) imeanza kujengwa na sekta binafsi ili kutumia vyema zaidi mkongo wa taifa wa mawasiliano katika kutoa huduma za mawasiliano. 

Akitoa mfano alisema ujenzi wa metro network ya Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 90 iliyojengwa na muungano wa kampuni za simu tatu imekamilika na hivi sasa mtandao huo umeanza kutumika.

Inatarajiwa kuwa mikongo mingine ya mijini itajengwa katika miji ya Arusha, Mwanza, Dodoma, Morogoro na Mbeya katika siku zijazo.

Sekta ya mawasiliano imekua ikikua kwa kasi katika miaka ya hivi karibbuni.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, sekta imeonyesha kukua haraka zaidi kwa wastani wa asilimia 21 kwa miaka 5 mfululizo hadi mwaka 2011 ikilinganishwa na sekta nyingine za uchumi.

Mchango wa sekta katika Pato Ghafi la Taifa (Gross Domestic Product) umekua kutoka asilimia 1.7 (2005) hadi kufikia asilimia 2.7 (2009).

Matumizi ya simu hivi sasa ni zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania ikilinganishwa na asilimia 3 katika miaka michache iliyopita.

Kwa upande wa intaneti watumiaji wameongezeka kutoka wastani wa 25,000 kwa mwaka 1999 hadi kufikia watumiaji zaidi ya 4,800,000 mwaka 2012.

Ends

TPA yaongeza ufanisi kitengo cha upakuaji magari



Afisa Utekelezaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini katika Kitengo  cha Magari Bandari ya Dar es Salaam, Principal Operation Officer and Head of Motor Vehicle Section Dar es Salaam Port), Bw. Daniel Sira (wapili kusho) akiwaonyesha stika kwenye moja ya gari ambalo limekidhi vigezo vyote vya kuondoka bandarini. Wengine wanaoshuhudia ni Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Bi. Janeth Ruzangi (katikati), kaimu afisa mawasiliano mkuu, Bw. Peter millanzi (kushoto) na afisa mawasiliano Mwandamizi, Bi. Levina Msia (Kulia). Waandishi wa habari walitembelea kitengo hicho cha jana kujionea shughuli za upakuaji magari.



Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema baada maboresho ya vitendea kazi yaliyofanyika bandari hapo hivi karibuni, kitengo cha magari (Motor Vehicle section) kinauwezo wa kupakua magari 1,000  kwa shifti moja ya masaa nane tofauti na kipindi cha nyuma ilikuwa inapakua chini ya magari 400.
Afisa Utekelezaji Mkuu ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Magari Bandari ya Dar es Salaam (Principal Operation Officer and Head of Motor Vehicle Section Dar es Salaam Port),Bw. Daniel Sira aliwaambia waandishi wa habari waliotembelea kujionea upakuaji wa magari  bandarini hapo jana kuwa huduma ya upakuaji magari ni nzuri na inafanyika kwa haraka.
“Tumefanya hivi kwa nia ya kutaka kutoa huduma nzuri na kwa haraka kwa wateja wetu wanaoagiza magari na wenye meli wasiweze kutumia muda mwingi katika bandari yetu,” na kuongeza kusema kuwa vifaa na ari ya kufanya kazi kwa bidii ndiyo imeongeza ufanisi huo.
Alisema wameboresha upakuaji kwa kuwa na vifaa vya kutosha katika upakuaji ili kuruhusu meli kukaa muda mfupi bandarini sababu meli ikikaa bandari muda mrefu ni ghrama na hii inavutia wenye meli kuzidi kuleta meli zaidi kwenye bandari hii.
Alifafanua kuwa wamefanya hivyo sababu mwenye meli na wenye magari wote ni wateja wa bandari hivyo wanategemea kazi ifanyike kwa haraka ili waweze kuondoka kwa haraka ndiyo maana wamefanya hivyo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wateja wote hao.
Bw.Sira alisema utaratibu wa sasa wa kukaguwa magari wakati wa upakuaji kutoka kwenye meli wafanyakazi wanafanya kwa umakini mkubwa na huweka alama ya stika ya njano kwa magari yasiyo na matatizo ya upungufu wa vyifaa,na alama nyekundu kwa magari yaliyo na vifaa pungufu.
Alisema katika eneo la upakuaji, magari yaliyokamilika vifaa vyote yanaruhusiwa kuondoka katika eneo hilo yakiwa na alama ya stika ya kijani na alama nyekundu kwa yale yenye matatizo kivifaa tangu yakiwa kwenye meli.Shughuli ya ukaguzi huo inafanyika wakati wa upakuaji kutoka kwenye meli ili kuwa na uhakika wa uzima wa magari pindi tu yanapokuwa yanapakuliwa huku wenye meli wakiwa pale kwa ajili ya kukabidhiana.
“Zamani wakati wa upakuaji kulikuwa na ucheleweshaji sababu kila gari likiwa nzima au linamatatizo yote yaliandikiwa formu ya Vehicle Discharge Inspection and Transfer Tally (VDITT) lakini kwa sasa haifanyiki hivyo.
Alisema magari mazima kwa sasa hayaandikiwi fomu hizo, bali yanaruhusiwa kuondoka toka eneo la upakuaji kwa kuwekewa alama ya kijani, na zile zenye matatizo kutoka kwenye meli zinaandikiwa fomu hiyo katika eneo la upakuaji wakati wa makabidhiano na wenye meli ili mamlaka isiweze kuingia garama ambayo haikuhusika.
Alisema pia magari yaliyoshuka ambayo ni mazima lakini yakanyofolewa vifaa bandarini wakati wa makabidhiano na wakala wa mizigo yanaandikiwa fomu ya Vehicle Handover (VHF) ili kuonyesha uharibifu huo umetokea bandarini hapo.
Alisisitiza magari yakiwa na matatizo tangia kwenye meli, wenye meli anakuwa na jukumu la kulipa gharama ya magari kwa wenye magari sababu amesabisha uharibifu huo, na kuongeza kusema kuwa inapotokea magari yamepakuwaliwa yakiwa yamekamilika kivifaa lakini likatokea tatizo la kunyofolewa vifaa yakiwa bandari basi mamlaka inakuwa na jukumu la kulipa gharama hizo kwa wenye magari.
Alisema gari likiwa na stika nyekundu kabla ya mteja kukabidhiwa linakaguliwa upywa kati ya karani wa bandari na wakala wa mzigo, wanasainishana kwa kuangalia vifaa vilichopungua baada ya kushushwa kwenye meli.
“Katika mazingira hayo kama gari limepungua vifaa likiwa kwenye meli mteja anatakiwa kumdai mwenye meli au alikonunua na kama limepungua vifaa likiwa bandarini basi mteja aidai bandari,”.
Pia alitoa wito kwa waagizaji wa magari wauzaji au mtu mmoja mmoja anayeagiza gari kuwa wanatakiwa kudai fomu ya VDITT na VHF ambazo ni nyaraka zinazosaidia kujiridhisha magari yao kama yako salama au vinginevyo.
Alisema wenye magari wanatakiwa kudai fomu hizo kutoka kwa wakala wa mizigo (Clearing and Forwarding Agency) ambao wanakuwa na fomu hizo baada ya makabidhiano kati yao na bandari
Mwisho. 

High optimism as RUBADA receives a Stiegler’s Gorge Power Project proposal



The Chairman of the Rufiji Basin Development Authority (RUBADA) Board of Directors, Prof. Raphael Mwalyosi (second left) receiving a copy of a report and proposal of development of the Stiegler’s Gorge Power project from a Brazilian based Odebrecht International New Business Director, Mr. Fernando Soares in Dar es Salaam over the weekend.  At the centre is RUBADA Director General, Mr. Aloyce Masanja and the Brazilian Ambassador to Tanzania, Mr. Fransisco Luz (extreme left).



By a Correspondent, Dar es Salaam
Implementation of a huge Stiegler’s Gorge Power is becoming a reality after a report and proposal of development of the project has been completed and presented to the government.
The proposal presented over the weekend in Dar es Salaam follows a Memorandum of Understanding (MoU) of the long awaited project between the Rufiji Basin Development Authority (RUBADA) and Odebrecht International, a reputable dam construction company in the world six months ago.
“This is a very crucial stage,” the RUBADA Director General, Mr. Aloyce Masanja told journalists after receiving the proposal in an event that was witnessed by top Odebrecht staffs, some officials from the government of Tanzania and RUBADA’s management and members of the Board of Directors.
According to Masanja, the proposal will now give a clear picture on the implementation of the project.
The proposal touches mainly on Power Market Overview, Engineering Studies and Technical Proposal, Preliminary Social-Environmental Evaluation, Key Stakeholders, Stage 1 Risk Analysis and Financial Structure and Proposed Business Plan.

According to Mr. Masanja, the project financial requirement is at the tune of USD 2 billion but the figure may vary depending on the technology to be agreed at a later stage.
RUBADA, as a public institution is allowed by law to generate and supply hydroelectric power in the basin and will partner with Odebrecht, a private entity in a form of Public Private Partnership (PPP).
“The project is a multipurpose by nature in the sectors of agriculture, energy, fisheries, flood control and tourism,” he said.
Once completed, the project will have the potential to produce 2100 MW.
The Brazilian company reviewed Feasibility Studies that was earlier done by a Norwegian company, NORCONSULT in 1980 on the similar project but shelved later on.
The next stage after reviewing the proposal will be designing and doing Environmental Impact Assessment (EIA) while the third stage will be commencement of construction. 
On his part, the company’s New Business Director, Mr. Fernando Soares said that his company understands the importance of the project, not only for Tanzania but for the whole region.

“We are proud to be part of such important endeavor,” he said.
He said that Odebrecht can provide great value to their clients bringing the necessary engineering, and construction expertise, as well as proven local knowledge and motivation to pursue a well-balanced contractual relationship.

The Chairman of the RUBADA Board of Directors, Prof. Raphael Mwalyosi said the Brazilian company has done a great job.
“We are very happy, they have done a great job according to our expectations,” Prof. Mwalyosi said.
On his part, the Brazilian Ambassador to Tanzania, Mr. Fransisco Luz said that his country is very proud that Tanzania has decided to have a Brazilian experience in the area of dam construction.
It is estimated that the Stiegler’s electricity will be among the smallest production cost in Africa standing at 4 USD Cents per a kilowatt hour, including tax.
“There are more than enough reasons for stakeholders to support this project,” he said.
Odebrecht Company Limited is reputed to be involved in big and successful construction of big hydropower projects in the world.  It was involved in construction of the world’s second power project found in Brazil with the capacity to produce 14,000 MW.
The whole of the Rufiji Basin has the potential to produce 4,000 MW.
Brazil is said to have transformed her economy for the past 30 years from the low income country to a middle economy today.  More than 85 per cent of the country’s power comes from hydro sources.
Its portfolio includes more than 58,500 MW in construction works and services in the power sector.
With more than 65 years of experience, developing projects in 25 countries in 4 continents.  In Africa, Odebrecht has been working since 1984, employs more than 20,000 persons, has successfully delivered projects in 9 countries and has formed long lasting partnerships with various clients.

Odebrecht is ranked in 2012 as number 13 of the top 225 International Contractors and number 2 in Hydropower plants by ENR, one of the most prestigious engineering and construction publication in the World.

Ends

Monday, January 14, 2013

TPA yazidi kuimarisha huduma zake



Kaimu Meneja wa Kitengo cha Makasha wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Bi. Brigita Madolomani( katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani, Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki juu ya ujio wa mashine mpya na za kisasa aina ya' Gott Wald Crane' kwa ajili ya upakuaji na upakiaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na Tanga, kulia ni Kaimu Afisa mawasiliano mkuu Peter Milanzi na Kaimu Meneja Kitengo cha Makasha Bi.Brigita Madolomani.Mashine hizo za kisasa kila moja imenunuliwa kwa Ero milioni 2.6

ACTING Communications Manager of Tanzania Ports Authority (TPA), Ms Janeth Ruzangi stresses a point to  journalists (not in picture) in Dar es Salaam over the weekend on the four purchased modern Gotwald habour cranes meant to increase productivity at the port each crane bought at 2.6 million Euro. Others looking on are acting  Manager of Container Terminal, Ms Brigita Madolomani( left) and the Authority’s Principal Communications Officer , Mr Peter Millanzi (Right). One of the acquired machine will be used at Tanga Port.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Katika juhudi za kuboresha huduma zake, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imenunua vifaa vinne vya kisasa aina ya ‘Gotwald  Harbour Cranes’ kwa ajili ya kuboresha huduma za upakiaji na upakuani mizigo.

Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Bi. Janeth Ruzangi alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo hayo.  Vifaa hivyo vina thamani ya jumla ya Euro 10.4 milioni.

“Vifaa hivi ni vya kisasa na kila kimoja kimenunuliwa kwa thamani ya Euro 2.6 Milioni…vina uwezo mkubwa wa kupakua na kupakia mizigo kwenye meli tofauti na ilivyo kuwa hapo nyuma,” alisema Bi. Ruzangi.

Alisema sasa uwezo umeongezeka katika bandari hiyo kwa kiasi kikubwa na kwamba hatua hiyo ni moja ya mikakati ya kuhimili ushindani katika utoaji wa huduma hiyo katika ukanda huu.
Akielezea zaidi alisema vifaa hivyo  pia vina uwezo wa kuendeshwa kwa rimoti na kufanya kazi kwa ufanisi na kwa umakini katika utoaji wa huduma hiyo kwa jamii.
Alisema ununuzi wa vifaa hivyo pia umeilenga Bandari ya Tanga ambayo imepatiwa kifaa hicho kimoja wakati vitatu vimebaki Dar es Salaam.
“Wakala wa meli sasa walete meli zao kwa wingi katika bandari yetu,” alisema na kuongeza kuwa wateja wote wanaotumia bandari ya Dar es Salaam hawana budi kuzidi kutumia bandari hiyo kwa vile huduma imezidi kuwa nzuri.
Kaimu Meneja Kitengo cha Makashi (AG Container Terminal) wa Mamlaka hiyo, Bi. Brigita Madolomani alisema kabla ya kuja vifaa hivyo vipya mwezi Octoba mwaka 2012, vifaa vilivyokuwepo vilikuwa na uwezo wa kupakua na kupakia kontena 216 kwa kipindi cha saa 24.
“Lakini baada ya vifaa hivyo vipya kununuliwa, mwezi Novemba mwaka 2012 jumla ya kontena 283 ziliweza kushughulikiwa kwa saa 24 na idadi hiyo kupanda hadi kontena 315 kwa saa 24 kwa mwezi Disemba,” alifafanua, Bi. Madolomani. 
Alisisitiza kusema kuwa maendeleo hayo makubwa ni hatua muhimu katika kuleta tija ya utoaji wa huduma katika bandari hiyo muhimu katika ukanda huu wa Afrika.
Bandari ya Dar es Salaam ni moja ya bandari ambayo hutegemewa na nchi jirani zikiwemo Zambia, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), Rwanda na Burundi.
Mwisho