Thursday, July 26, 2012



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw.Raymond Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Agro EcoEnergy Tanzania Limited, Bw.Anders Berfors wakati alipofanya ziara ya siku moja katika shamba kubwa la kisasa la zao la miwa linalomilikiwa na kampuni hiyo wilayani Bagamoyo jana.

The Tanzania Investment Centre (TIC) Acting Executive Director, Mr. Raymond Mbilinyi (left) listening to the Managing Director, Mr. Anders Berfors of Agro EcoEnergy Tanzania Limited when the former visited the sugar cane plantation owned by the company in Bagamoyo district yesterday.  

TIC yawakikishia ushirikiano wawekezaji


Na Mwandishi wetu, Bagamoyo

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeimwagia sifa kampuni ya Agro EcoEnergy Tanzania Limited kwa maendeleo mazuri yanayolenga kutekelezwa kwa uwekezaji mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji cha zao la miwa katika bonde la Mto Ruvu wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Kwa sababu hiyo, TIC imesema kwamba iko tayari kuisaidia kampuni hiyo na wawekezaji wengine watakao onekana kufanya vyema katika miradi yao kwa faida ya pande zote mbili. 
Mara uzalishaji wa mradi huu unaotarajiwa kuanza mwaka 2014 utakapoanza inatarajiwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za sukari, nishati ya umeme na mafuta aina ya ethanol ambayo yana uwezo wa kuendesha magari.
Sifa hizo zilitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw. Raymond Mbilinyi alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya mradi huo mkubwa wa kilimo cha kisasa cha miwa jana wilayani Bagamoyo.
“Inatarajiwa kwamba mradi huu utazalisha  sukari tani 150,000 kwa mwaka, mafuta ya ethanol pamoja na Megawati 30 za umeme,” alisema.
Kati ya Megawati hizo, 15MW zitatumika kwa ajili ya uzalishaji katika kampuni hiyo na zilizobaki zitatumika kwa ajili ya wakaazi wa jirani.
Alisema jukumu la serikali ni kuhakisha inatoa msaada kwa mradi huo kwa vile ni silimia 60 tu ya sukari inayotumika inazalishwa  hapa nchini wakati asilimia 40 inatoka nje.
Alisema mradi huo ukianza kuzalisha kwa mafanikio utasaidia kupunguza mfumuko wa bei  kwa vile bidhaa hiyo ni moja inayochangia mfumuko wa bei mara pale inapokuwa adimu.
Akifafanua zaidi alisema kati ya bidhaa zinazo changia kuwepo mfumuko wa bei ni sukari na mchele na serikali imeliaona hili na kuwa inajitahidi kukuza uwekezaji katika eneo hilo.
“Tunapenda kasi ya uzalishaji iendelee kuwa kubwa na serikali itahakikisha vikwazo vyote vinatatuliwa ili kuhakikisha malengo ya uwekezaji yanatimia kwa ajili ya maendeleo ya nchi,” alisema. Bw. Mbilinyi.
Alisema kufanikiwa kwa mardi huo kutaleta mafanikio makubwa katika uchumi wa nchi kwa kuwa wakulima zaidi ya 300 watapata ajira na kupata mahitaji mbalimbali.
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Per Carstedt alisema wamekuja kuwekeza katika mradi mkubwa wa kilimo cha kisasa cha umwagiliaji cha zao la miwa kwa ajili ya soko la ndani la nchi.
“Hii itasaidia kupunguza kuagiza nje ya nchi bidhaa mbalimbali kama mafuta na sukari,” alisema na kuongeza kwamba hii itasaidia kutoa mchango kwa maendeleo kwa kiwango kikubwa.
Alisema zao la miwa linachukuwa miezi 12 kukua tangu kupanda na hadi kuvuna na kwamba wanatarajia kuzalisha aina tano za miwa.
Mwisho


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw.Raymond Mbilinyi (kulia) akionyeshwa maendeleo ya shamba la miwa linalomilikiwa na kampuni ya Agro EcoEnergy Tanzania Limited na meneja wa shamba hilo, Bw. Andre’ Fayol ‘Iterbe wakati alipofanya ziara ya siku moja katika shamba hilo wilayani Bagamoyo jana.

The Tanzania Investment Centre (TIC) Acting Executive Director, Mr. Raymond Mbilinyi (right) listening to the Farm Manager of the sugar cane plantation, Mr. Andre’ Fayol ‘Iterbe owned by Agro EcoEnergy Tanzania Limited when the former visited the plantation owned by the company in Bagamoyo district yesterday.  

TIC reassures needed support to promising investors


By a Correspondent, Bagamoyo

Tanzania Investment Centre (TIC) has hailed progress made by Agro EcoEnergy Tanzania Limited toward massive cultivation of sugar cane along Ruvu basin in Bagamoyo district, Coast region.
Because of that, the investment agency assured the company and other good performing investors of the government’s prompt assistance should a need arise.
The TIC Acting Executive Director, Mr. Raymond Mbilinyi praised the company on the progress made so far toward the modern cultivation of sugar cane which will see sugar production, electricity and ethanol for running cars produced.
“We are happy on the progress on the ground,” Mr. Mbilinyi said during a visit to the plantation with over 4,000 hectors yesterday.
It is envisaged that 150,000 tons of sugar will be produced annually after the start of production in 2014.  Also expected will be the production of 30 Megawatt of electricity and ethanol that can be used in running of cars.
Of the 30MW; 15MW will be used by EcoEnergy while the remaining one will be used by the surrounding community.
He said the government though TIC will continue supporting such promising investments in the country for the benefit of both parties.
Taking EcoEnergy as an example, he said once the production starts; it will greatly help the country which has the capacity of producing only 60 per cent and imports the remaining.
He said the government works hard to make sure that it attracts investments in sugar and rice plantations because the availability of the two agricultural products in the country will also help stabilize the economy.
“We will help promote and facilitate good investors in agriculture in a win-win situation,” he said.
He noted that TIC would like to see an increase of investments in the country and that the government will make sure that it do away with unnecessary hurdles to investors but at the same time making sure that such investments benefit the country and people of Tanzania at large.
The investment expects to benefit over 300 farmers who will be contracted to cultivate and eventually sell their products to the company.
The Executive Chairman of the company, Mr. Per Carstedt said his company was serious in undertaking large scale sugarcane irrigation farming in Tanzania for local and international market.
“This will help reduce importation rate for things such as sugar and oil,” he said, adding that will be a major contribution for the economy.
He said that his company plans to produce five types of sugarcane and that he was happy for the good progress of the seedlings they are producing.
Ends


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw.Raymond Mbilinyi (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti Mteandaji  wa kampuni ya Agro EcoEnergy Tanzania Limited Bw. Per Carstedt  (kushoto) wakati alipofanya ziara ya siku moja katika shamba kubwa la kisasa la zao la miwa linalomilikiwa na kampuni hiyo wilayani Bagamoyo jana.  Kati kati ni Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw.Anders Berfors.

The Tanzania Investment Centre (TIC) Acting Executive Director, Mr. Raymond Mbilinyi (right) listening to the Executive Chairman of Agro EcoEnergy Tanzania Limited, Mr. Per Carstedt (left) when the former visited the sugar cane plantation owned by the company in Bagamoyo district yesterday.  At the centre is the company’s Managing Director, Mr. Anders Berfors.

Wednesday, July 25, 2012

Chuo Kikuu Mzumbe chateuliwa kutoa elimu dhidi ya rushwa


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Chuo Kikuu Mzumbe ni moja ya taasisi za elimu kumi duniani zilizochaguliwa kuanzisha mradi wa majaribio wa kufundisha kozi zinasosaidia kujenga maadili ya Kuzuia na Kupambana na rushwa nchini katika ngazi ya shahada ya uzamili.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Andrew Mbwambo alisema hayo jijini Dar es Salaam jana mbele ya waandishi wa habari.
Kozi hiyo itatolewa chuoni hapo kuanzia mwaka ijao wa masomo kwa wanafunzi wa shahada ya uzamili ya masomo ya menejimenti na biashara.
“Mradi huu umeanzishwa na Umoja wa Mataifa na kuvichagua vyuo vya biashara Afrika kuanza kuutekeleza kwa majaribio,” alisema Prof. Mbwambo na kuzitaja nchi nyingine barani Afrika zitakazoendesha kozi hiyo kuwa ni Afrika ya Kusini na Nigeria.
Alisema vyuo hivyo vikiweza kutekeleza kwa ufanisi, mradi huo utasambazwa kenye vyuo vingine Afrika ili kuweza kuwajenga wanafunzi na wasomi wa taaluma ya biashara kuwa na maadili ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Akitoa mfano juu ya swala hilo alisema watu wanasoma taaluma za biashara hawana bodi za kitaaluma kwa ajili ya kulinda maadili yao ya kazi kama ilivyo kwa madaktari, wahandisi na wanasheria ambao wana bodi za kitaaluma, jambo alilosema halitakiwi. 
Akielezea zaidi alisema kwa kuanzia, Chuo hicho kimetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa waandamizi wa jeshi la polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Alisema chuo kwa sasa kinajipanga kupata na kuuangalia mtaala kutoka mpango huo wa Umoja wa Mataifa na kuuingiza katika mtaala wa chuo kwa ajili ya kufundishia wanafunzi na kuanzisha kozi fupi kwa ajili ya kuwapatia mafunzo watu mbalimbali katika sekta ya umma na binafsi wakiwemo wabunge.
Alisema kampasi yao ilipata bahati kwa Mkuu wao wa Kozi fupi na Ushauri ,Profesa Shiv Tripath kushiriki katika kuandaa mtaala huo na chuo kikawa miongoni mwa vyuo vitatu vilivyo chaguliwa Afrika katika mradi wa majaribio.
Mmoja wa waanzilishi wa mpango huo ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha New York, Marekani, Profesa Ronald Berenbeim alisema swala hilo halikuanzishwa kwa kuangalia rushwa iliyoko Afrika, bali lengo lake ni kutoa mafunzo ya kujenga maadili dhidi ya rushwa kwa watumishi wa umma na sekta binafsi.
“Tumekichagua Chuo kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa mradi wa majaribio na vyuo vingine vitatu Afrika ili waweze kuingiza katika mitaala yao swala la vita dhidi ya swala hili la kuzuia na kupambana na rushwa katika taaluma za biashara,” alisema.
Akiongea wakati wa mafunzo kwa jeshi la polisi, Mkuu wa Kitengo cha Maadili cha Jeshi la Polisi, Bw.Patrick Byatao alisema mafunzo hayo yanalenga kuzidi kuwakumbusha juu ya maadili katika kutekeleza majukumu yao pamoja na kwamba wana miiko ya jeshi.
Alisema mafunzo hayo ni muhimu, na yalikuwa yanawakumbusha baadhi ya polisi wanaojisahau na kujiingiza katika vitendo vya rushwa kurudi katika maadili ya jeshi hilo.


Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Andrew Mbwambo (kulia) akiongea wakati wa mafunzo kuhusu maadili yaliyotolewa na chuo chake kwa maafisa wa jeshi la polisi jijini Dar es Salaam jana.  Anaefuatia katika picha ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema, Prof. Ronald Berenbeim toka Chuo Kikuu cha New York, Marekani na Prof. Shiv Tripath, Mkuu wa Kozi fupi na Ushauri toka Chuo Kikuu Mzumbe, kampasi ya Dar es Salaam. 

Wednesday, July 18, 2012

Stiegler’s Gorge Power Project MoU signed


By a Correspondent, Dar es Salaam
At last, a Memorandum of Understanding (MoU) toward the implementation of a huge Stiegler’s Gorge Power Project has been reached.
The MoU of the long awaited project has been reached between the Rufiji Basin Development Authority (RUBADA) and Odebrecht International, a reputable dam construction company in the world in Dar es Salaam recently.
“I am very happy that the MoU has been signed today,” the RUBADA Director General, Mr. Aloyce Masanja said after the signing event that was witnessed by top Odebrecht staffs, and some officials from the government of Tanzania and RUBADA’s management and members of the Board of Directors.
In terms of finance, Odebrecht in collaboration with RUBADA will mobilize financial resources from Brazilian sources (Brazil-Africa line of credit) and any other sources including from the government of Tanzania.
According to Mr. Masanja, the project financial requirements is at the tune of USD 2 billion but the figure may vary depending on the technology to be used, either arch dam or gravity dam.
As part of the agreement, RUBADA as a public institution allowed by law to generate and supply hydroelectric power in the basin will partner with Odebrecht, a private entity in a form of Public Private Partnership (PPP) and operated jointly.
“The project is a multipurpose by nature in the sectors of agriculture, energy, fisheries, flood control and tourism,” he said.
Once completed, the project will have the potential to produce 2100 MW.
The signing of the MoU allows the Brazilian company to start reviewing Feasibility Studies that was earlier done by a Norwegian company, NORCONSULT in 1980 on the similar project but shelved later on.
The second stage after that will be designing and doing Environmental Impact Assessment (EIA) while the third stage will be commencement of construction.  If all goes well it is hoped that the construction stage will start after two years from now.
On his part, the company’s Business Director, Mr. Fernando Soares said it was a tremendous honor for the company to be involved in the development of a project of such an importance for the future of Tanzania.
“We are strongly committed in contributing for the increase of the country’s energy capacity,” he said, adding that Odebrecht has a tremendous relevant experience in developing hydro power projects all over the world, being ranked as the world’s major construction company in that particular field.
He said that the company thanks Tanzanian government and the board of RUBADA for their efforts to make this partnership possible.
The Chairman of the RUBADA Board of Directors, Prof. Raphael Mwalyosi explained the project as ‘a dream come true.’
He appealed for the government and other stakeholders to continue supporting the project for the country’s benefit because hydro power is the cheapest to run once it is constructed.
Odebrecht Company Limited is reputed to be involved in big and successful construction of big hydropower projects in the world.  It was involved in construction of the world’s second power project found in Brazil with the capacity to produce 14,000 MW.
The whole of the Rufiji Basin has the potential to produce 4,000 MW.
Brazil is reputed to have transformed her economy for the past 30 years from the low income country to a middle economy today.  More than 85 per cent of the country’s power comes from hydro sources.
Its portfolio includes more than 58,500 MW in construction works and services in the power sector. 

Makubaliano ya awali ya mradi wa Stiegler’s yafikiwa


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) imetiliana saini ya makubaliano ya awali ya uzalishaji nishati ya umeme kupitia mradi wa Stiegler’s Gorge na Kampuni ya Odebrecht International ya Brazil.
“Leo tunayo furaha kusaini makubaliano ya awali ya kuanza kutekeleza maradi mkubwa wa Stiegler’s ambao una uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2100 katika Bonde la Mto Rufiji na Kampuni iliyobobea katika uzalishi nishati kwa kutumia nguvu ya maji,”alisema Bw. Aloyce Masanja, Mkurugenzi Mkuu wa RUBADA baada ya tukio hilo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Alisema makubaliano hayo yanatoa fursa kufanyika upembuzi yakinifu kupitia ule uliofanywa awali na kampuni ya NORCONSULT ya Norway miaka ya 1980 na kufanyiwa maboresho na  baada ya miezi sita kampuni hiyo itakabidhi ripoti ya kwanza.
Alisema awamu ya pili itahusisha mkataba wa kibiashara  kwa kuangalia maji, teknolojia itakayotumika, vyanzo vya fedha na utunzaji wa vyanzo vya maji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema ni lazima suala la mazingira lipewa kipaumbele kwa sababu mradi wa Stiegler’s upo katika hifadhi ya Selou na bonde hilo pia ni muhimu kwa kilimo.
Alisema hatua ya tatu itakuwa ni kuanza ujenzi wa mradi wenyewe na matarajio ni kuanza baada ya miaka miwili kuanzia sasa.
Alisema mradi unatarajia kughalimu fedha za Kimarekani bilioni mbili ingawa ghara inaweza kubadilika kutokana na teknolojia itakayotumika.
Alisema Bonde la Mto Rufiji linapita katika mikoa nane na linakaliwa na watu milioni nane hivyo kukamilika kwa mradi huo kutakuwa na msada mkubwa katika shughuli za maendeleo.
Mkurugenzi wa Biashara wa Odebrecht, Bw. Fernando Soares alisema kampuni yao imetia saini kutekeleza maradi huo ili kuzalisha nishati ya umeme ambayo itachangia kuimarika kwa viwanda na hatimaye kukuza uchumi wa Tanzania.
“Hatua hii tuliyofikia ni muhimu kwa RUBADA na Serikali ya Tanzania na matarajio ni kuona mradi huu unafanyaka vizuri na kusaidia nchi hii,”alisema Bw. Soares.
Alisema kwa upande wao wamejidhatiti kutokana na ujuzi walionao katika kuzalisha nishati ya umeme kupitia nguvu ya maji na wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa muda mrefu katika mataifa mbalimbali duniani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi RUBADA, Profesa Raphael Mwalyosi aliiomba Serikali na wadau wote wa nishati nchini kuunga mkono jitihada za utelezaji maradi huo mkubwa ambao utaweza kukabili tatizo la umeme nchini.
“Ninawaomba tusiogope kutekeleza mradi huu, kikubwa ni kuwa na mipango ya kulinda vyanzo vya maji na Wakuu wa Mikoa ambao mikoa yao ni vyanzo vya maji yanayoingia katika Bonde la Mto Rufiji wawe makini katika jambo hili,” alisema.
Balozi wa Brazil nchini Tanzania,Bw.Francisco Luz alisema  makubaliano yaliyofanywa na RUBADA na Kampuni ya Odebrecht yanalenga kuzidi kujenga mahusiano na kuchochea shughuli za uchumi Tanzania.
Alisema kampuni hiyo ya Brazil ilifika Afrika miaka 30 iliyopita na kufanya kazi katika nchi mbalimbali na nchi Tanzania imejipanga kutekeleza mradi huo muhimu kwa ufanisi mkubwa.

Govt assures investors of conducive investment climate



By a correspondent, Dar es Salaam
The government has assured domestic and international investors and prospective ones that it will continue creating conducive environment for them and make Tanzania attractive destination.

This was said by the Acting Executive Director of Tanzania Investment Centre (TIC), Mr. Raymond Mbilinyi during the launch of the World Investment Report 2012 in Dar es Salaam recently.

“The government will continue formulating policies geared toward creating conducive environment for investors and ensuring a win-win situation,” he said after the launch of the report titled: ‘Towards a New Generation of Investment policies’

He added: “I am very happy to report that investors are still confident with the effort the government of Tanzania is doing to improve the investment climate thus why we have noted the growth of FDI inflows to Tanzania to 1,095 USD billion in 2011 contrary to the decline experienced by Africa overall 2011 inflows.”

He explained that now the government need to build the capacity of domestic investors to be ready to take advantage of FDI for the sustainable development and inclusive growth. 

According to the report, Africa’s economic growth slowed down to 2.7 percent in 2011 compared to 4.6 percent in 2010, mainly due to political unrest in the North African countries.
Growth in the Sub-Sahara African countries slowed down to 5.1 percent in 2011 compared to 5.3 in 2010.
Tanzania real GDP grew by 6.4 percent in 2011 compared to 7.0 percent in 2010.  The slowdown in growth is largely attributed to drought conditions in some parts of the country which adversely affected agricultural production and electricity outage which contributed to low performance in manufacturing and other economic activities that rely on electricity.
Despite the slowdown in overall growth, communication, financial intermediation, construction and education sub-sector recorded higher growth rates ranging between 6 percent and 19 percent.
The United Nations Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr. Alberic Kacou urged policy makers in Tanzania to use the investment policy framework for sustainable development detailed in the 2012 report, as a reference in formulating national investment policies.

“We believe by using such a framework for investment policies, will benefit all Tanzanians,” he said.

On his part, a renowned investment expert, Mr. Emmanuel Ole Naiko advised the government to seriously consider continuing providing incentives as a way to lure investors to Tanzania and gave the example of China which has attracted a huge number of investors in recent years because of providing attractive incentives.

He noted that this is very important since once a country has many investors, creates a strong base of big tax payers, hence development.

“What is needed is to be strict and follow laws and regulations governing incentives and investment in general,” he said.
  

Benki ya Afrika Tanzania yaimarisha mikopo ya nyumba


Nyumba bora ni kati ya vitu muhimu kabisa kwa binadamu tangu enzi na enzi.  Ndio maana jamii na serikali za dunia hii zinajitahidi kupitia programu mbalimbali kuhakikisha watu wake wanaishi katika makazi bora.  Kama moja ya wadau wa sekta binafsi, Benki ya Afrika Tanzania imekuwa pia ikijitahidi kusaidia juhudi hizi za serikali na watanzania kwa ujumla kuwa na nyumba bora kwa gharama nafuu.  Katika kufanikisha swala hili, hivi karibuni benki ilinunua hisa toka kampuni ya Tanzania Mortgage Refinance Company (TMRC) ili kuimarisha mikopo yake ya nyumba kama mwandishi wetu anavyooelezea…
Malazi, mavazi na chakula ndio vitu vitatu muhimu kwa binadamu.
Ndio maana jamii na serikali mbalimbali duniani zimekuwa zikifanya kila liwezekanalo kuhakikisha mahitaji hayo yanapatikana kwa urahisi na kwa ubora.
Pamoja na kwamba Serikali ya Tanzania inalishughulikia hili kupitia taasisi zake mbalimbali, pia imeruhusu sekta binafsi kusaidia katika juhudi hizo.
Benki ya Afrika Tanzania ni moja ya wadau hao ambao wamedhamiria kusaidia juhudi za kuwawezesha watanzania kuwa na makazi bora na hivyo kusaidia serikali na kufikia malengo ya milenia.
Chombo hiki cha fedha kimejizatiti kutoa mikopo ya nyumba ili kuwawezesha watanzania kuwa na nyumba nzuri kwa makazi ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya watu binafsi na taifa kwa ujumla.
Katika juhudi za kuimarisha mikopo yake ya nyumba benki hiyo imewekeza shilingi bilioni moja na kupata umiliki wa hisa asilimia 9.57 za Tanzania Mortgage Refinance Company (TMRC) ambapo sasa benki itakuwa na fursa ya kukopa fedha kutoka kampuni hiyo ili kuendeleza utoaji wa mikopo ya nyumba kwa mafanikio zaidi.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa uwekezaji huo hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Bw. Ammish Owusu-Amoah alisema hatua hiyo imefikiwa kwa lengo la kuendelea kuboresha huduma ya mikopo kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
“Ninayo furaha kutangaza kuwa sasa tutakuwa na nafasi nzuri ya kuendelea kutoa mikopo ya nyumba kwa vile benki yetu imejiunga na TMRC ambapo tutakuwa na fursa ya kukopa fedha kwa ajili ya kutoa huduma hii muhimu ya mikopo kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla,” anasema Bw. Amoah.
TMRC ni kampuni inayotoa mikopo ya nyumba kwa mabenki ambao ni wanachama wake ili hatimaye benki hizo ziweze kutoa mikopo ya nyumba ya muda mrefu kwa wateja na watanzania kwa ujumla.
Anasema benki inatoa mikopo ya kununua nyumba, kukarabati nyumba, kumalizia kujenga na kuweka nyumba kama amana ya kupata fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Anasema lengo la kufanya hivyo ni kutaka kuwawezesha wateja wao na watanzania kumiliki nyumba nzuri na kuwa na shughuli mbalimbali za maendeleo ili kupiga vita hali duni ya vipato miongoni mwao na wakipata mazingira mazuri ya kuishi itatoa fursa kwa afya zao na kufanya kazi za kujipatia maendeleo kwa bidii.  
“Ni hatua nzuri kuona wadau wengi tunashiriki katika sekta hii ya mikopo ya nyumba na benki yetu haiko nyuma katika mchakato huu ambao ni muhimu kwa maendeleo ya wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla,” anasema Bw. Amoah.
Mkopaji atahitajika kurejesha mkopo wa kununua nyumba kwa muda wa miaka 15 na ule wa kuweka nyumba kama amana ya kupata fedha, kukarabati nyumba na kumalizia kujenga utalipwa kwa kipindi cha miaka 10.
Ushirika uliopo katika sekta hiyo unasaidia wadau wa TMRC kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania kuwa na nyumba bora na kuleta sura mpya kwa watanzania ambao wanakabiliwa na tatizo la kupata fedha kwa mara moja na kujenga nyumba za zinazostahili kulingana na mazingira ya sasa.

Benki ya Afrika Tanzania yasifia nguvu kazi yake.


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Rasilimali watu iliyo bora imetajwa kama moja ya siri za mafanikio ya Benki ya Afrika Tanzania.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Ammish owusu-Amoah wakati wa sherehe ya mwaka ya wafanyakazi wa benki hiyo iliyohusisha pia familia zao hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
“Tunatambua na kujali watu wetu, mafanikio ya benki yetu yamechangiwa sana na utendaji kazi bora wanaouonyesha,” alisema Bw. Amoah.
Alisema sherehe hizo zinahusisha wanafamilia kwa kuwa wana mchango mkubwa sana katika kuwaongezea ari na kuwapatia moyo wafanyakazi wa benki katika utendaji wao wa kila siku.
“Ninawahamasisha kufanya kazi kwa bidii zaidi kwa faida yetu sote na kwa faida ya taifa zima kwa ujumla,” alisema.
Sherehe hizo pia zilishuhudiwa kutolewa tuzo kwa wafanyakazi mbalimbali baada ya kufanya vyema katika nafasi zao za kazi.
Mmoja wapo alikuwa Bi. Sophia Mwema aliyetangazwa kuwa mfanyakazi bora idara ya Rasilimali Watu na Utawala.
“Nina furaha kubwa…sikutegemea,” alisema Bi. Mwema, na kuongeza kwamba hii itamfanya kuongeza bidii zaidi.
Mwingine aliyetambuliwa alikuwa, Bw. Masumbuko Humuli aliyekuwa mfanyakazi bora kutoka idara ya Fedha na Uhasibu ambaye kwa upande wake alitoa wito kwa wafanyakazi wenzake kushirikiana zaidi ili kuifanya benki hiyo kufanikiwa zaidi katika wakati huu wa ushindani mkubwa.
Benki ya Afrika Tanzania imekuwa ikijitahidi kujitanua na kuimarisha huduma zake katika miaka ya hivi karibuni.
Tangu ianzishwe hapa nchini mwaka 2007, imeshafanikiwa kufungua matawi kumi mkoani Dar es Salaam na sita nje ya mkoa huo yakiwepo ya Morogoro, Tunduma, Mwanza, Moshi, Mbeya and Arusha.
Benki hii ni moja ya mtandao wa kibenki unaofanya kazi katika nchi 15 ambazo ni pamoja na Benin, Burkina Faso, Ghana, Ivory Coast, Mali, Niger na Senegal.  Nyingine ni Burundi, Djibouti, Kenya, Madagascar, Tanzania na Uganda.

Pia ina tawi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Bank of Africa Tanzania Managing Director, Mr. Ammish Owusu-Amoah (right) talks to the staff during this year’s Bank of Africa Tanzania Family Day held in Dar es Salaam recently.


Bank of Africa Tanzania Managing Director, Mr. Ammish Owusu-Amoah (right) presenting a certificate of recognition to Mr. Charles Elisante who was announced as the best worker from Ilala Branch during this year’s Bank of Africa Tanzania Family Day held in Dar es Salaam recently.