Mwanzilishi wa Shule ya Sekondari Thomas More
Machrina, Profesa Justinian Galabawa akisisitiza jambo jana jijini Dar es
Salaam kuhusu baadhi ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuinua kiwango cha
ufaulu wa wanafunzi hapa nchini.
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari
Thomas More Machrina,Emmanuel Rweyendela akisikiliza kwa makini maelekezo ya
mwalimu wa somo la kiingereza katika shule hiyo,Bi.Kulthum Asiimwe jana jijini
Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Ushirikiano wa karibu kati ya walimu na wanafunzi na kutumia
muda mwingi kufudisha maudhui yaliyomo katika vitabu kulingana na mitaala
vimetajwa kama vitu muhimu vitakavyorejesha hadhi ya elimu nchini.
Mwanzilishi wa Shule ya Sekondari Thomas More
Machrina, Profesa Justinian Galabawa amesema kuwa mfumo huo ukizingatiwa
utaboresha mfumo wa elimu na wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.
“Tunatakiwa kama taifa turudishe mfumo wa zamani ambao
ulilenga maudhui ya masomo na ushirikiano kati ya walimu na wanafunzi,” alisema
na kuongeza kusema kuwa muda mwingi utumike katika masomo.
Alisema wasomi wengi wa zamani walifaidika na mfumo
huu ambapo walimu walikuwa na ushirikiano mzuri na wanafunzi na muda mwingi ulitumika
kufundisha maudhui ya masomo yenyewe.
Shule ya Sekondari ya bweni Thomas More Machrina ambayo
ni ya wavulana ilianzishwa 2005 na inatumia mfumo huo wa zamani ambao
unaisaidia wanafunzi kufanya vyema katika masomo.
Akiongea jana jijini Dar es Salaam alisema serikali
inatakiwa kuiga mbinu zinazotumiwa na shule za binafsi na kutumia mfumo huo ili
shule zote za umma ziweze kufanya vizuri.
No comments:
Post a Comment