Na Mwandishi wetu, Manyara
Majadiliano ya mara kwa mara ya Baraza la Biashara Mkoa
wa Manyara yametajwa kuwa moja ya njia zinazoweza kuibua fursa za biashara na
uwekezaji na kuchochea ajira na ukuaji wa uchumi mkoani humo.
Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Mkoa huo, Bw. Joel
Bendera ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo alisema hayo katika mkutano wa tano wa
baraza hilo kuwa mikutano hiyo ina nafasi kubwa ya kuibua fursa za biashara.
“Mabaraza haya yamesheheni wajumbe kutoka sekta ya
umma na binafsi...yanapokutana yanaibua fursa za biashara na kujenga mtandao
miongoni mwao,”alisema.
Mabaraza ya biashara ya mikoa yanafanya kazi chini ya
Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na yanaundwa na wajumbe wa sekta ya umma na
binafsi katika kuleta majadiliano na kuibua fursa za biashara.
Alisema mkoa huo una fursa nyingi za kibiashara ikiwemo
ya Kilimo na madini hivyo wajumbe wana wajibu wa kuzidi kuibua fursa zaidi na
kuzitangaza watu wawekeze.
No comments:
Post a Comment