Waziri wa maji ambae pia ni mbunge wa jimbo la mwanga
Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) akisisiiza jambo wakati akizungumza na
wananchi wa kijiji cha mriti kata ya mwaniko, wilayani mwanga mkoani
Kilimanjaro wakati alipofanya ziara katika kata za mwaniko
na kilomeni kukagua na kuangalia maendeleo ya miradi mbalimbali
inayotekelezwa na serikali, wengine katika picha ni Diwani wa kata ya mwaniko
Baraka Maradona (kulia) na (katikati) ni mwenyekiti wa kijiji cha mriti
Shabaini Hamis
Na Mwandishi Wetu, Mwanga
Serikali imewataka wananchi wa Kilomeni Wilaya ya Mwanga
Mkoani Kilimanjaro, kuacha tabia ya kuharibu uoto wa asili ikiwa ni pamoja na
kukata miti hovyo jambo linalochangia kuharibu vyanzo vya maji.
Waziri wa maji ambaye, pia ni mbunge wa jimbo la mwanga,
Profesa Jumanne Maghembe, alitoa katazo hilo wakati alipofanya ziara katika
kata za mwaniko na kilomeni kukagua na kuangalia maendeleo ya
miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ambayo tayari imekamilika na ile
inayotarajiwa kuanza kutekelezwa.
“Naomba sana, tuache kuharibu mazingira, watu wanakata miti
hovyo, hii ni hatari kwenu ninyi wenyewe,” alisema Waziri Maghembe.
Alisema miradi inayotekelezwa na serikali imetumia fedha
nyingi sana, ni jkumu la wananchi wa maeneeo husika kuitunza kwa kuacha
kuharibu vyanzo vya maji katika maeneo yao.
“Tukianza kufanya uharibifu huu tutakuwa hatuwatendei haki
watoto wetu kumbukeni misitu hii imekuwepo tka zamani sio jambo zuri kuanza
kuikata,”aliongeza Profesa
Alisisitiza kuwa serikali kwa kushirikiana na wahisani
imetumia fedha nyingi katika kutekeleza miradi hiyo, hivyo ni jukumu la
wananchi kuitunza na kuiona kama ya kwao na si mali ya serikali tu.
No comments:
Post a Comment