Na Mwandishi wetu, Morogoro
Serikali imeshauriwa ipitie upya mitaala yake ya
elimu ili iweze kuendana na ulimwengu wa utandawazi ambao unafanya mwanafunzi
kuwa mbunifu zaidi.
Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi
Ndetembia Matemu, Bw. Joshua Kihaka amesema mjini Morogoro hivi karibuni kuwa
mitaala ya elimu inatakiwa kuangaliwa upya ili iende sambamba na wakati.
“Wanafunzi wanatakiwa kupata maarifa yatakayowafanya
kuwa wabunifu,” alisema.
Alisema pamoja na changamoto hiyo shule ya Ndetembia
Matemu inawandaa wanafunzi wakubalike kitaifa na kimataifa kulingana na
ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Alifafanua kuwa shule hiyo inayofundisha kwa lugha ya
kiingereza pia inafundisha somo la Teknolojia ya Habari na Mawaslianino
(TEHAMA) ambalo linawafanya watoto kwenda na wakati.
Alisema changamoto za kielimu zilizopo nchini lazima
zitatuliwe na serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, walimu na
wazazi.
No comments:
Post a Comment