Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta
Binafsi Afrika (Africa Enterprise Challange Fund) AECF, Bw. Hugh
Scott kati akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu shindano la
awamu ya tatu ya dirisha la ufadhili wa Kilimo cha biashara, ambapo
watazania wenye mawazo ya biashara katika sekta ya Kilimo wanahamasishwa kuomba
ushiriki.Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Uwekezaji ya mfuko huo, Dkt. Salum
Diwani na kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko huo nchini Tanzania, Dkt. Alexandra
Mandelbaum.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta
Binafsi Afrika (Enterprise Challange Fund) AECF, Bw. Hugh Scott
akibadilishana mawazo na waandishi wa habari na wageni mbalimbali baada ya
kuelezea uzinduzi wa shindano la awamu ya tatu ya dirisha la
ufadhili wa kilimo cha biashara jijini Dar es Salaam jana, Kushoto kwake ni
Mjumbe wa Kamati ya Uwekezeji wa mfuko huo, Dkt.Salum Diwani na kulia ni
Mwakilishi wa Mfuko huu Tanzania, Dkt. Alexandra Mandelbaum.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Watanzania wenye mawazo ya biashara katika
sekta ya Kilimo wamehamasishwa kushiriki shindano la awamu ya tatu
ya dirisha la ufadhili wa Kilimo cha biashara kwa ajili ya
kuendeleza sekta ya Kilimo ambayo inawagusa watu wengi nchini hasa waishio
vijijini.
Mkurugenzi wa Africa Enterprise
Challenge Fund (AECF), Bw. Hugh Scott aliwambia waandishi wa habari jana jijini
Dar es Salaam kuwa mfuko huo umezindua shindano hilo ili kusadia Kilimo
cha biashara kama njia ya kusaidia kukuza sekta hiyo ya Kilimo hapa nchini.
AECF ni mfuko wa sekta binafsi wa dola za
Kimarekani milioni 217 unasaidiwa na baadhi ya wafadhili wakubwa katika fedha
za maendeleo chini ya Muungano wa Mapinduzi ya kijani ya Kilimo kwa nchi
mbalimbali za Afrika (AGRA).
Mkurugenzi huyo alisema shindano hilo la
awamu ya tatu ya dirisha la ufadhili wa Kilimo cha biashara linalenga
kupata mawazo ya biashara katika maeneo mawili yakiwemo ya Kilimo cha biashara
katika mnyororo wa thamani na katika ufumbuzi unaoongeza huduma za kifedha
vijijini katika kusaidia uzalishaji katika kilimo cha kibiashara na sekta
zinazohusiana.
Shindano hilo la dirisha la ufadhili
Kilimo cha biashara maalum kwa ajili ya Tanzania lilizinduliwa tarehe 20,
January mwaka huu na litakuwa wazi hadi hadi Machi 31, 2014.
Bw. Scott alisema awamu hii pia
itashirikisha kufadhili waombaji watakaofanikiwa kupitia mchanganyiko wa ruzuku
na mikopo itakayorejeshwa ya kati ya dola za Kimarekani 100,000 na dola milioni
1.
Alisema waombaji wa shindano hilo
wanatakiwa kuonyesha mawazo ya biashara yenye matokeo ya uhakika kwa watu
masikini vijijini nchini Tanzania, kuongeza ajira na mapato, kupunguza gharama
na kuongeza uzalishaji.
Akifafanua zaidi alisema kampuni
zinazostahili kuomba ni zile zinazohusika na ukulima au uzindikaji, wale
wanaoanzisha mipango ya kilimo cha mkataba, watengenezaji na wasambazaji wa
pembejeo za Kilimo, wachukuzi na wafanyabiashara na watoa huduma wengine katika
sekta binafsi, ikiwemo huduma za taarifa ya soko.
Alisema alisema fomu za kuomba kushiriki
shindano hilo zinapatikana kwenye intaneti kupitia tovuti
http//aecfafrica.org/windows/Tanzania-window.
Kwa upande wake, mjumbe wa kamati ya
uwekezaji ya AECF, Dkt. Salum Diwani alisema matarajio ya shindano hilo ni
kuona ushiriki mpana wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania ili kusadia
sekta hiyo kupiga hatua.
Alisema wenye mawazo yenye ubunifu wachangamkie
fursa hiyo ambayo italeta manufaa kwa maisha ya watanzania
na ukuaji wa uchumi vijijini nchini.
“Hii ni njia muafaka ya kusaidia
mabadiliko katika mfumo wa soko nchini,” alisema na kuongeza kusema kuwa wenye
mawazo bora na bunifu ndiyo wanaolengwa katika shindano hilo.
Akifafanua zaidi alisema si rahisi kwa
wakulima kupata huduma za kifedha duniani kote, hivyo mfuko huo umeamua kufanya
hivyo kukiwezesha Kilimo kukuwa.
Alisistiza kuwa uchumi wa Tanzania na
Afrika utakua kwa kasi kubwa kama sekta ya Kilimo itazidi kuboreshwa na kuwa
hiyo ndiyo dhamira ya mfuko wao.
Awamu ya kwanza ya shindano hilo
ilizinduliwa mwezi Novemba 2011 na kampuni 10 zilipata ufadhili wakati awamu ya
pili ilizinduliwa mwezi Juni 2012 na kampuni 12 zilipata ufadhili.
Mwisho
No comments:
Post a Comment