Monday, January 27, 2014

Habari picha katika mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika ya Kusini


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (katikati) Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda wa Afrika ya Kusini, Bi. Elizabeth Thabethe(kushoto) na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Bi.Janet Mbene(kulia) wakielekea kwenye chumba cha mkutano ambako mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika ya Kusini uliofanyika Dar es Salaam hivi karibuni na kuaratibiwa na Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) kwa ushirikiano na Wizara.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda  Maalum ya Uwekezaji (EPZA),Dkt. Adelhelm Meru(kushoto) na Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Huduma wa Mamlaka hiyo, Bi. Zawadia Nanyaro wakifuatilia mada mbalimbali wakati mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika ya Kusini uliofanyika Dar es Salaam hivi karibuni. Mkutano huo uliratibiwa na EPZA kwa ushirikiano na Wizara.



Meneja wa Uhamasishaji uwekezaji (ndani) wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kushoto Bw. Mathew Mnali na Meneja Uhusiano wa Kituo hicho, Bi. Pendo Gondwe, wakifuatilia mada mbalimbali wakati mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika ya Kusini uliofanyika Dar es Salaam hivi karibuni. Mkutano huo uliratibiwa na EPZA kwa ushirikiano na Wizara.

No comments: