Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Joseph Kuzilwa
(kulia) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Prof. Daniel Mkude
(katikati) na Prof. Gerald Monela wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho, kampasi
ya Mbeya mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, kampasi ya Mbeya, Prof. Ernest
Kihange akiwa pamoja mkuu wa chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Andrew
Mbwambo (kushoto kwake) wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho, kampasi ya
Mbeya mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
Na
Mwandishi wetu, Mbeya
Vijana
wahitimu wa vyuo vikuu wameshauriwa kuingia katika soko la ajira wakiwa
wanajiamini na kujipambanua kiuwezo kutokana na elimu waliyopata wakiwa chuoni.
Akiongea
wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Mbeya jijini humo
mwishoni mwa wiki, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Joseph Kuzilwa alisema kuwa
vijana wahitimu hasa toka chuo hicho wanatakiwa kuonyesha kuwa wanaweza kazi
kwa kuwa elimu waliyopata ni bora na iliwatayarisha kukabiliana na changamoto
mbalimbali.
Alifafanuwa
kuwa pamoja na changamoto za ajira zilizopo nchini, bado nafasi zipo ila
kinachotakiwa kwa vijana ni kujiamini na kutumia vizuri elimu waliyopata kwa
faida yao nay a nchi.
“Vijana
waingie katika soko wakiwa wapambanaji na sio watu walioshindwa,” alisema.
Akitoa
ushauri zaidi alisema vijana hao watumie pia fursa za kujiajiri na biashara kwa
kutumia vizuri elimu na maarifa ya ujasiriamali waliyopata chuoni.
Alisema
katika azma ya kutoa elimu bora zaidi na kutoa wahitimu wenye uwezo mzuri
kiutendaji na kifikra, chuo hicho kimeanzisha mikakati ya kuboresha njia za
kielektroniki na kampasi ya Mbeya ikihusishwa.
Alisema
tayari wahadhiri wa kampasi hiyo wamepewa mafunzo kuhusu njia hizo na bado
mafunzo yanaendelea kwa wanafunzi pia.
“Njia
hizi mpya zinafaa hasa kwa kipindi hiki ambacho vyuo vingi sasa vinapanuka kwa
idadi ya wanafunzi,” alisema.
Pamoja
na kuishukuru serikali kwa mafanikio ya kampasi hiyo, pia aliiomba pamoja na
wadau wengine wa elimu ya juu, kuongeza juhudi katika kushirikiana na chuo
kukabiliana na changamoto zinazokabili chuo.
Kwa
upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Prof. Gerald Monela, alisema
uongozi utaendelea kuipanua kampasi hiyo ili kuongeza nafasi zaidi kwa wadau
wengi wanaopenda kupata elimu katika chuo hicho.
Alisema
mpango wa kukamilisha taratibu za umiliki wa eneo la Iwambi kwa ajili ya
upanuzi wa kampasi hiyo unaendelea vizuri na kuwa mara baada ya kukamilisha
taratibu za umiliki, mikakati ya upanuzi itaanza.
“Tunahitaji
sana ushirikiano mkubwa na wananchi wa mkoa wa Mbeya na wadau wengine katika
kutimiza azma hii,” alisema, huku akiushukuru uongozi mzima wa jiji la Mbeya na
wananchi wake kwa kuwapatia eneo hilo.
Aliwaasa
wahitimu wote kujihadhari na janga la ukimwi na madawa ya kulevya ili taifa
lisipoteze nguvu kazi adimu iliyowekezwa ndani yao.
Jumla
ya wahitimu 567 walitunukiwa shahada mwaka huu kulinganisha na 314 mwaka jana
katika programu za astashahada, 235; stashahada, 121; shahada ya kwanza, 173 na
shahada ya uzamili, 38.
Kampasi
ya Mbeya imeendelea kukua kwa idadi ya wanachuo ambayo imeongezeka kutoka 405
mwaka 2006 hadi kufikia 2241 mwaka huu, hii ikiwa ni ongezeko la takribani
asilimia 453.
Mwisho
No comments:
Post a Comment